Shikamoo SUMATRA, kumbe mnaweza!

tatizo zikitokea ajali tunakimbili kudhani zimesababishwa na mwendo kasi tunasahau kuna vitu vingine vinachangia kama ubovu wa barabara, matairi kuwa chini ya viwango, mifumo ya break za magari kuna kipindi marekani waligundua ubovu wa mfumo mbovu wa break wa magari ya toyota ikabidi toyota zote zirudishwe na faini juu na juzijuzi wamegundua udanganyifu uliofanywa na kampuni ya VW wakaipiga faini kubwa.Tutaendelea kudhibiti mwendo lakini bila kuchunguza sababu nyingine bado ajali zitaendelea kutokea
 
Scania...kama "KISBO"...Speed 180 unakuwa ushafuta kibakuli...zhong tong ni 140..
Ha ha ha kisbo mzee kibko aisee,wanazunguka singida lakin yule aliekatiza kati itigi anachelewa zaid yke,,,nawakubali kisbo haajawai kuni let down
 

Kuripuliwa = kulipuliwa
 
Kama kuna kitu sijawahi kukielewa hapa duniani ni EXCUSE ya usalama inayofanya mabasi yasisafiri usiku hapa Tanzania.

Kuwahi kufika ndio kunakotugharimu. Ikiwapo ruksa ya kutembea usiku, madereva wataenda taratibu tu. Mbona saa ya kutukong'ota askari huwa wanatosha lkn saa ya kulinda hawatoshi?
 
people used to die in the, the, the rake
 
Hapo ndio huwa nashanga. Kenya askari hupangwa kila barrier usiku.
Mf kila km 10.
Hapa kwetu ni rushwa. Barrier ni dili.
Kenya kuna tishio la Al shabab lakini mabasi husafiri usiku.

Eti Tz vijambazi tu vimezuia karbu masaa 8 kutotumika!!


RIP DEMOKRASIA
 
Yah, Kenya ni mfano mzuri. Hali yao ni tete lkn wako macho 24/7 biashara zinafanyika. Sisi kama kuku, giza linaamua mwisho wa kutembea.

Kama unafanya kazi ya kuajiriwa na biashara ndio utaona ugumu wa kuwa kuku. Ingekuwa tunatembea usiku, ningetoka Dodoma na basi la jioni baada ya kutoka kazini, nikafika Dar alfajiri, nikafunga bidhaa zangu mchana kutwa na jioni nikakwea basi lingine kurudi Dom. Anayeendesha ni dereva, mm nalala. Alfajiri nikiwa Dom, biashara na kazi viko balanced.

Lkn kwa mtindo giza ndio master, unahitaji 3 days kuja kununua mitumba na kuifikisha mkoani.

Tuanze na viwanda vya kutengeneza usalama
 
Sasa mkuu Wabunge ndio akina MLINGA. Tutarajie nn?

RIP DEMOKRASIA
 
Napendekeza spidi iongezwe toka 80kph mpaka 110kph na penye 50kph iwe 70kph.
Kwa barabara zetu zilivyo nyembamba na mbovu, hakika hilo pendekezo lako litatumaliza. Barabara zetu ni nyembamba mno; na mahala pengi unatembea kwenye lami, lakini utafikiri unapita juu ya barabara ya vumbi. Kwani gari haitulii ni kuchezacheza tu kutokana na barabara kutokuwa smooth.

Tukiwa na barabara pana na zilizo smooth, hakika hata no speed limit (kwenye highway tu) nitakubaliana nayo.

Highway kama ya Dar-Moro ilipaswa iwe na lanes angalau tatu kila upande. Moro-Dodoma, lanes mbili; Dodoma-Singida lanes mbili n.k.
 
Bado ni lazima madereva wajali uhai wa abiria bila kushurutishwa hapo ndio tutapunguza ajali
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…