"shikamoo" nchini kenya

Na sisi shikamoo tunaing'ang'ania ya nini? Inamaanisha, niko chini ya miguu yako. Salamu ya kitumwa! Lakini wazee usipowaamkia patachimbika!! Tubadilike waswahili!
mzee tukumbuke kuwa language is arbitrary. kama wao walitumia kwa tafsiri ambayo kwa sasa haipendezi, wazee wetu wameamua kulitumia neno hilo likiwa na heshima ya hali ya juu. na yapo maneno mengi ya aina hii tena mengine ni matusi kwa jamii nyengine ila yanatumika.
 
Huwa nikifanya tafsiri ya neno kwa neno napata kizunguzungu.
Shika maana yake ushike.
Moo huwa nahisi inafanana na kile kiungo.
OTIS

Usiku huu umekula kweli wewe?:yawn:
 
Lugha ya Kiswahili imechukua (sio kukopa) maneno mengi toka Lugha ya Kiarabu na kufanya sehemu ya utamaduni wake. Shikamoo ni moja ya maneno yenye asili ya Kiarabu. Bila kujali sana maana yake, ni sehemu ya utamaduni wa Lugah ya Kiswahili. Hakuna neno lolote jingine la Kiswahili lenye hadhi na maana sawa na 'Shikamoo'
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom