"shikamoo" nchini kenya

LE GAGNANT

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
1,241
251
Hakuna salamu ya "shikamoo" kwa waswahili wa Nairobi, kiswahili chao kinachukua sana tafsiri ya moja kwa moja ya Kingereza kwa maneno mengi.

Ni Mombasa pekee nimebahatika kupata salamu ya "shikamoo"
 
Na sisi shikamoo tunaing'ang'ania ya nini? Inamaanisha, niko chini ya miguu yako. Salamu ya kitumwa! Lakini wazee usipowaamkia patachimbika!! Tubadilike waswahili!
 
Na sisi shikamoo tunaing'ang'ania ya nini? Inamaanisha, niko chini ya miguu yako. Salamu ya kitumwa! Lakini wazee usipowaamkia patachimbika!! Tubadilike waswahili!

tatizo na shikamoo ni lazima ukadirie umri wa mlengwa. Jinsi tulivochoka nchi hii si ajabu ukaishia kuumpa shikamoo dogo la dot com generation.
 
Huwa nikifanya tafsiri ya neno kwa neno napata kizunguzungu.
Shika maana yake ushike.
Moo huwa nahisi inafanana na kile kiungo.
OTIS
 
Shikamoo ililetwa na mabwana wa utumwa ndio maana inatumiwa maeneo ya pwani zaidi kwa maeneo yote ya afrika mashariki. Hata bongo mikoani hawaitumii sana hiyo shikamoo.
Ulishaenda kyela na kukuta wanyakyusa wanasalimiana shikamoo?
 
Salamu za mtaani Kenya.... Itakuaje mtu wangu/ mzae? unajibu SAFI
Iz hau? unajibu poa
 
Shikamoo ililetwa na mabwana wa utumwa ndio maana inatumiwa maeneo ya pwani zaidi kwa maeneo yote ya afrika mashariki. Hata bongo mikoani hawaitumii sana hiyo shikamoo.
Ulishaenda kyela na kukuta wanyakyusa wanasalimiana shikamoo?

Mwalimu wako au mtu wa makamo hesabu ya mzee wako ulikuwa unamuamkiaje?
Shikamoo haina maaana ya utumwa ni heshima na utamaduni wa kiafrika kwa kijana kumpa mtu alie na umri wa kumzidi. Hukuti mtu mwenye umri mkubwa namuamkia mdogo shikamoo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom