Shigongo amvaa Tundu Lissu

Shigongo amvaa Tundu Lissu

Kama mpaka sasa hujajua walichosahihisha, basi hukustahili hata kuuliza swali hili.
kuna madini ambayo yamezuiliwa mpaka sasa? kuna mkataba ambao umeshabadilishwa mpaka sasa? kama upo nambie, mwanzo tuliambiwa kwamba wale Acacia ni wezi, wamekuja Ikulu mkulu kawapongeza kawaita wanaume, tangia lini wezi wanapongezwa eti kwa sababu wamekuja kunegociate? tangia lini unanegociate na mwizi? sheria zinasemaje kuhusu wakwepa kodi na wahujumu uchumi? kwamba tunegociate nao na kuwasifia kwamba wao ni wanaume???
 
Njaa nuksi sana naona anatafuta stimulating package huyo Shingongo naona anapiga debe kwa Jacaranda..wakati Jacaranda nae anatembeza kibakuli kwa weupe huko kila anopokweda kuomba pesa ananyimwa tu.. Kumbe bado haja Qualified vigezo vya Democracy kabisa..yuko Hoi hapo
 
Mfanyabiashara na kada wa Chama Cha Mapinduzi, Erick Shingongo amemnyoooshea kidole Tundu Lissu na kusema anashindwa kuelewa kwanini Mwanasheria huyo amekuwa ni mpingaji wa mambo mazuri na kusema jambo hili linamshushia heshima.

Erick Shigongo amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema yeye kwanza anapongeza hatua alizochukua Rais Magufuli juu ya sakata la madini na kudai kuwa limekuwa na matokeo chanya kwani kiongozi wa Barrick amelazimika kuja Tanzania na kubembeleza yaishe.

"Namheshimu sana Lissu, sana tu. Ni msomi wa sheria, tena mzuri tu! Lakini namshangaa, nashindwa kumwelewa kwa kitu kimoja kwamba kwa nini hawezi kukubali pale jambo jema linapofanyika? Mimi nadhani ni kujijengea heshima kubwa sana kuonyesha uzalendo pale nchi inapopambana na wizi wa maliasili ambazo hata hao Acacia wenyewe wameukubali, sasa kwa nini Lissu anaendelea kubeza kile kinachofanyika? Hakika hili linamshushia heshima" alisema Shingongo

View attachment 525174
Hivi zile hela zake amelipwa au ndio anasubiri kwanza mauzo ya Makinikia ?
 
Yupo sawa
Lisu kaishiwa, kiki zinamharibu huyu mtu
Kashindwa kuwatetea Wananchi wake
Anawatetea Wazungu
Huyu niwakupimwa sio bure
Siyo Lisu tu na wale waliyosema wanaomuunga mkono papa lowasa nao wakapimwe akili a.k.a Mchungaji Msigwa
000601fe405446b8c7f600b86aae2be7.jpg
 
Yaani mtu kama Shigongo kumuelewa Lissu anachokisema ni shida.Sijui ni nani amewaaminisha kwamba Lissu anampinga Magufuli ukweli umepindishwa waziwazi.Lissu hajapinga chochote ila anaonyesha namna nzuri ya kushughulikia hilo suala watu wameamua kujifanya hamnazo na kumgeuzia kibao.Kama alivyosema Profesa Mhongo ukweli utabaki kuwa ukweli
 
Mfanyabiashara na kada wa Chama Cha Mapinduzi, Erick Shingongo amemnyoooshea kidole Tundu Lissu na kusema anashindwa kuelewa kwanini Mwanasheria huyo amekuwa ni mpingaji wa mambo mazuri na kusema jambo hili linamshushia heshima.

Erick Shigongo amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema yeye kwanza anapongeza hatua alizochukua Rais Magufuli juu ya sakata la madini na kudai kuwa limekuwa na matokeo chanya kwani kiongozi wa Barrick amelazimika kuja Tanzania na kubembeleza yaishe.

"Namheshimu sana Lissu, sana tu. Ni msomi wa sheria, tena mzuri tu! Lakini namshangaa, nashindwa kumwelewa kwa kitu kimoja kwamba kwa nini hawezi kukubali pale jambo jema linapofanyika? Mimi nadhani ni kujijengea heshima kubwa sana kuonyesha uzalendo pale nchi inapopambana na wizi wa maliasili ambazo hata hao Acacia wenyewe wameukubali, sasa kwa nini Lissu anaendelea kubeza kile kinachofanyika? Hakika hili linamshushia heshima" alisema Shingongo

View attachment 525174
duuh kumbe na wewe ni mmojawapo wa watu wasioelewa kweli kilevi cha safari hii kimewachanganya watanzania
 
Anajpendekeza kwa baba jesca yawezekana anadaiwa TRA
 
Shigongo amuache Lissu,nilihudhuria jana mahafali ya CHASO Dodoma,Lissu aliongea mambo mengi sana,na alikua zaidi ya shule,na akifika mahali akasema yuko tayari kubaki peke yake sehemu anayoamini ni salama kuliko kuungana na wale wanaoahangilia bila yakujua mambo yalivyo.
 
huyu kaishiwa sera kitambo, na hajui Lisu anatetea nini, Lisu awezi kutetea wezi, ila anatoasomo jinsi ya kuwaana twende kwenye ukweli.
Anatetea tu maslahi yake binafsi. Kama kweli angekuwa ni mtetezi wa wanyonge wananchi wake kule kwao wasingekuwa maskini kiasi kile.
NI MTETEZI WA TUMBO LAKE TU.
Afadhali hata wenzie kwenye majimbo yao kuna maendeleo angalau. Yeye ni kubwata bwata tu pasipo faida yoyote.
 
Kwanza kabisa...SIAMINI KAMA SHIGONGO ANAO HUO UZALENDO KIASI CHA ROBO TUU YA UZALENDO ALIO NAO TUNDU LISSU.

kunywa maji mwanangu.....

hivi zile bilioni zilizokutoa chozi zilikuwa na uzalendo wa aina yoyote?

Erick Erick Erick....tuache tusiongee sana kumi la mwisho hili tunaivizia nyota ya bahati ya lailtulkadri....tuache bwana shigongo...msikilize mama alivyosema...

KUNYWA MAJI MWANANGU.
 
Lissu niwakuogopwa kama Ukoma
huyu Ni msaliti
Msaliti ni hiyo ambayo aligonga meza kushabikia Sera na sheria mbovu pamoja na mikataba ya kihuni, wakati huo Lissu anaongoza harakati za kuzinusuru rasilimali zetu,, Leo anjifanya kushangaa eti nchi inaibiwa,,
 
Back
Top Bottom