Shigongo acha Udhalilishaji

Shigongo acha Udhalilishaji

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,932
Reaction score
11,849
Shigongo na magazeti yake wameazisha Oparesheni Fichua uovu(OFM) oparesheni hii imejaa udhalilisha na ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo ya haki ya faragha.

Je, wanafanya hivi kwa ruhusa ya mamlaka ipi?

Nani amewapa kibali cha kuendesha oparesheni hii?
 
Mi hayo magazeti ya udaku huwa siyaamini na sioni tija ya kuwepo kwake.Hua najiuliza maswali mengi bila majibu nnapoona mtu mzima na heshima zake ananunua na kulisoma hadharani.
 
Mbona umeandika AACHA? Nilizani umesahau kuanza na H, sababu wengi hawajui kuitumiia. Hivyo unasomeka kuwa hafanyi tena...
 
Shida sio Shigongo bali ni ninyi wasomaji...

Magazeti hayo yamepata usajili kwa ajili ya kuandika habari hizo za kidaku, hivyo hata msomaji unaponunua maana yake una kiherehere cha kusoma udaku...

La hasha ungelitafuta magazeti mengine yenye habari zenye tija na kuachana na hayo yenye taarifa za kidaku...
 
Hakika hili jambo kama usingelileta basi nilikuwa njiani kulileta siku si nyingi. Sawa unafichua uovu ila je ni lazima kumpiga picha huyo mtu akiwa nusu utupu na kuiweka hiyo picha front page? Kwangu mimi hapo ni kama umemuhukumu pasipo kumpa nafasi ya kujieleza. Na unatumia kigezo kipi kumhukumu huyo mtu? Mamlaka yenye haki hiyo ni mahakama sio Shigongo na wala sio magazeti yake.
 
Shida sio Shigongo bali ni ninyi wasomaji...

Magazeti hayo yamepata usajili kwa ajili ya kuandika habari hizo za kidaku, hivyo hata msomaji unaponunua maana yake una kiherehere cha kusoma udaku...

La hasha ungelitafuta magazeti mengine yenye habari zenye tija na kuachana na hayo yenye taarifa za kidaku...

Mkuu sio msomaji wa magazeti hayo ila jana katika peruzi yangu kwenye mtandao nikakuta mzungu yupo na binti amesuka rasta eti wanadai yuko form 3 wakati ni mtu mzima kabisa.
 
Yuko kibiashara zaidi anajua hayo ndio mambo ambayo watz wanayapenda muda si mrefu atakua billionea no tz
 
Kukos culture kama taifa imekua ni kitu hatari sana, maovu wanayofichua ni ya kupanga na cjui mission and vission yao ni ipi ? Ktk kazi yao hyo na inasaiduaje development career ya taifa letu
 
Af Mafumanizi yote ya kupanga,wanawatumia vijana na wadada wa mjini wasio na ajira kutengeneza mafumanizi ili wapate habari.

Se
nt from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
kwahili nakubaliana na wewe mwenyewe huwa najiuliza inakuwaje mtu kaingia guest na mtu wake halafu wao wakamfumanie hizo tarifa wamezipata wapi na huo mlango wa guest nani anaufungua kama siyo jambo la kupanga huu ni ujinga tu.
 
Mkuu uko sahihi watanzania wengi huacha kufuatilia hbr za msingi za maendeleo hata mwenendo wa serikali na kusoma hbr za chupi na boksa anazoandaa ndugu yetu huyu na OFM yake kwa ushirikiano na polisi na sidhani kama serikali wanakusanya kodi ipasavo hapo maana nackia nao hao OFM wanakula rushwa kwa udaku wao huo

Yuko kibiashara zaidi anajua hayo ndio mambo ambayo watz wanayapenda muda si mrefu atakua billionea no tz
 
Shida sio Shigongo bali ni ninyi wasomaji...

Magazeti hayo yamepata usajili kwa ajili ya kuandika habari hizo za kidaku, hivyo hata msomaji unaponunua maana yake una kiherehere cha kusoma udaku...

La hasha ungelitafuta magazeti mengine yenye habari zenye tija na kuachana na hayo yenye taarifa za kidaku...

Shida haiko kwa msomaji, si vibaya msomaji akisoma habari kwenye gazeti lolote na kusema mapungufu ya waandishi hao.
 
Shida sio Shigongo bali ni ninyi wasomaji...

Magazeti hayo yamepata usajili kwa ajili ya kuandika habari hizo za kidaku, hivyo hata msomaji unaponunua maana yake una kiherehere cha kusoma udaku...

La hasha ungelitafuta magazeti mengine yenye habari zenye tija na kuachana na hayo yenye taarifa za kidaku...

Is this from you? Kumlaumu mteja au mtengenezaji, the same to drugs wanaoonekana waovu ni walaji. Tukubali tu hatuna firm gvt, nchi zingine huyo shigongo asingekohoa!

Ni kweli kuna magazeti ya udaku kama hili ImageUploadedByJamiiForums1395470975.005049.jpg
Lakini huwezi kuta mtu kaandikwa kipuuzi na haya magazeti hayanunuliwi na kila mtu, ni mpk mtu awe +18 (ofcoz wenzetu wana proof of age Id).

Serikali yetu ipo km haipo kwa baadhi ya mambo

Sent from Nokla using Jf app
 
niliona nachelewa kuchangia hii post yani huyu jamaa ni juha sana pamoja na hao policcm maana sielewi lengo lao hasa ni nn kutokomeza au kudhalilisha watu.
 
Back
Top Bottom