Luca Paguro
JF-Expert Member
- Mar 26, 2023
- 476
- 1,060
Ruangwa tuna shida kubwa ya maji. Mimi nimezaliwa hapa nimekulia hapa hadi leo hii nakaribia umri wa miaka 20 miaka yote hapa tuna shida ya maji tu, tangu niko mdogo tunateseka na shida ya maji hadi leo hii bado tunaendelea kuteseka. Nothing is getting better
Huku maji yanatoka mara moja kwa wiki, yakijitahidi sana mara mbili. Na kutoka kwake yanatoka kwa saa 1 tu halafu yanakata. Kwa wiki nzuri tukibahatika maji yanatoka kwa masaa mawili.
Maana yake hata tank halijai, maji ya tank yanaisha mnabaki hamna maji. Siku nyingine yanatoka maji machafu bombani yanakuwa na rangi nyekundu kana kwamba yamechanganyika na udongo, siku nyingine pia yanatoka kwa spidi ndogo mno hata kwenye tank hayapandi
Maji yenyewe ya chumvi halafu wanabania, yanatoka saa 1 kwa wiki. Bila kisima hutoboi
Nyinyi watu mnaohusika na usambazaji wa maji Ruangwa, leteni maji hata mara tatu kwa wiki, kila siku yatoke masaa mawili mawili basi tupate walau masaa 6 kwa wiki. Maana tunateseka sana wakazi wa haka kamji