KERO Shida ya maji Ruangwa imezidi sasa

KERO Shida ya maji Ruangwa imezidi sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Tujiandae tukatiki Oktoba 29 shida ya maji itakuwa historia🥳
 
Pole sana,hamia pale kijiji cha Nandagala kuna ukuta mkubwa juu ya kilima mule maji 24/7 kwa nini uteseke.
 
Hapo bora wangeprint bango moja kubwa.
Mabango makubwa yapo tayari. Huku kuna kila size ya bango, nyumba za watu masikini wamebandika kazi na utu kwenye milango na kuta za nyumba zao za udongo. Taa za barabarani, majengo ya watu kila kona kuna mabango ya kutosha ya size tofauti tofauti

Kama ni kura huku wameshapata. Mi sijali walete tu maji
 
Duh... Kama wameshaanza mradi basi waumalizie tu, maji yatufikie. Viongozi wasije wakala pesa za mradi halafu sisi tukaendelea kuteseka tu, hali si shwari kabisa.
Maana mimi Ruangwa mjini sioni changamoto nyingine tofauti na maji. Walete maji jamani, hizi pesa za huu mradi mafisadi waziache tu, chonde chonde 😥
Kwa ruangwa mjini kilichobaki maji na flyover bc😂😂😂😂😂
 
Ruangwa tuna shida kubwa ya maji. Mimi nimezaliwa hapa nimekulia hapa hadi leo hii nakaribia umri wa miaka 20 miaka yote hapa tuna shida ya maji tu, tangu niko mdogo tunateseka na shida ya maji hadi leo hii bado tunaendelea kuteseka. Nothing is getting better

Huku maji yanatoka mara moja kwa wiki, yakijitahidi sana mara mbili. Na kutoka kwake yanatoka kwa saa 1 tu halafu yanakata. Kwa wiki nzuri tukibahatika maji yanatoka kwa masaa mawili.

Maana yake hata tank halijai, maji ya tank yanaisha mnabaki hamna maji. Siku nyingine yanatoka maji machafu bombani yanakuwa na rangi nyekundu kana kwamba yamechanganyika na udongo, siku nyingine pia yanatoka kwa spidi ndogo mno hata kwenye tank hayapandi

Maji yenyewe ya chumvi halafu wanabania, yanatoka saa 1 kwa wiki. Bila kisima hutoboi

Nyinyi watu mnaohusika na usambazaji wa maji Ruangwa, leteni maji hata mara tatu kwa wiki, kila siku yatoke masaa mawili mawili basi tupate walau masaa 6 kwa wiki. Maana tunateseka sana wakazi wa haka kamji
Aweso na CCM yote wamefeli kwenye issue ya maji japo wanajisifu eti wamemtua mwanamke ndoo kichwani. Labda wanamaanisha wamemtwika. Hilo ni tatizo kwenye miji yote ya hii nchi ya Samia. Kwenye kila mji, huwa kunakuwepo ka kikundi kadogo ka wakazi (wakiwemo viongozi wa serikali na vigogo wengine) ambao wanapata maji muda wote. Halafu wanatumia takwimu za hao wachache kutudanganya kuwa hakuna shida ya maji.
 
Kwa ruangwa mjini kilichobaki maji na flyover bc😂😂😂😂😂
😂😂 Ni kweli sisi maji ndo yanatuharibia, maana haka ni kamji kadogo ila hakana changamoto nyingi
Umeme haukatiki sana, shule hazikuwepo sasahivi zimejaa tele, barabara kila mtaa wameweka lami na taa za barabarani, na bado wanaendelea kujenga barabara. Kuna uwanja wa mpira, wamejenga hospitali nzuri, Internet mitandao yote inashika 4G vizuri sana, watu wanaongezeka na sasahivi nimeanza kuona kidogo watu wameanza kujenga nyumba nzuri

Wanajenga lami kwenda moja kwa moja hadi Nachingwe sasahivi. Inatoka Nachingwea hadi hapa Ruangwa na inaendelea hadi kwenda njia ya Mbekenyera. Hii barabara inaendelea na ujenzi niliipiga picha juzi
IMG_20251010_081318.jpg
Screenshot_2025-10-15-22-53-04-620_com.google.android.apps.photos-edit.jpg
 
Aweso na CCM yote wamefeli kwenye issue ya maji japo wanajisifu eti wamemtua mwanamke ndoo kichwani. Labda wanamaanisha wamemtwika. Hilo ni tatizo kwenye miji yote ya hii nchi ya Samia. Kwenye kila mji, huwa kunakuwepo ka kikundi kadogo ka wakazi (wakiwemo viongozi wa serikali na vigogo wengine) ambao wanapata maji muda wote. Halafu wanatumia takwimu za hao wachache kutudanganya kuwa hakuna shida ya maji.
Advance nimesoma Mbeya, kule hakukuwa na shida ya maji
Ila maeneo mengi ya Tanzania maji ni shida. Sasa kwa nini wanatudanganya kuwa hakuna shida ya maji. Unajua huwezi kusolve tatizo kama ukijidanganya eti hilo tatizo halipo
 
Katikati ya michenga na chimbila a pana tank kubwa mno je halijaanza kazi?
 
Pole sana Luca Paguro, Ila wewe ni snitch ulimkataa mwanao baada ya kubadilika kwenye maji kisa demu, 😅😅
 
Kijana kuwa na subira, Kuna miradi mkubwa wa maji ya kutoka chanzo Cha Nyangao, mradi huu ukikàmilika utahudumia kata za njiani za Malolo, Nandagala,Mnacho, Chienjele, Nkowe , Likunja na kata zote za mjini(kata za Ruangwa na Nachingwea), na vijiji baadhi vya wilaya ya Nachingwea mfano baadhi ya vijiji vya kata ya Chiola(Mtimbo, Chiola A na B, Namauni na Chingunduli).
Kwa Sasa mradi upo katika hatua ya kuunganisha mabomba ya line kuu, Kwa upande wa ujenzi wa matanki tayari umekamilika. Kata ya Malolo Tanki limejengwa kati ya Kijiji Cha Michenga na Chimbila A, pia Kuna Tanki lingine limejengwa juu milimani katika Kijiji Cha Chimbila A, Tanki lingine katika Kijiji Cha Nandagala
 
Pole sana Luca Paguro, Ila wewe ni snitch ulimkataa mwanao baada ya kubadilika kwenye maji kisa demu, 😅😅
Alberto alizingua mwenyewe alikuwa na wivu wa kijinga, pale bila kumsnitch maana yake Giulia angejua na mimi ni sea monster 😅
 
😂😂 Ni kweli sisi maji ndo yanatuharibia, maana haka ni kamji kadogo ila hakana changamoto nyingi
Umeme haukatiki sana, shule hazikuwepo sasahivi zimejaa tele, barabara kila mtaa wameweka lami na taa za barabarani, na bado wanaendelea kujenga barabara. Kuna uwanja wa mpira, wamejenga hospitali nzuri, Internet mitandao yote inashika 4G vizuri sana, watu wanaongezeka na sasahivi nimeanza kuona kidogo watu wameanza kujenga nyumba nzuri

Wanajenga lami kwenda moja kwa moja hadi Nachingwe sasahivi. Inatoka Nachingwea hadi hapa Ruangwa na inaendelea hadi kwenda njia ya Mbekenyera. Hii barabara inaendelea na ujenzi niliipiga picha juziView attachment 3489224View attachment 3489227
Barabara hii ni nachingwea to kilanjelanje mkeka tupu hiyo ukifika nanjilinji pale mto mbwemkulu wachina wanakesha wanajenga daraja kubwa sana
 
Back
Top Bottom