Shida sio CCM shida ni Watanzania

Shida sio CCM shida ni Watanzania

Naam,

Lakini pia hatua moja ya kubadilisha jamii ni kujenga utamaduni wa kubadilisha chama tawala.

Kwa sasa hivi kuna watu wengi wameamini kwamba CCM ikitoka madarakani nchi itakuwa na machafuko. Kama wazee walivyoamini Nyerere akitoka madarakani nchi itakuwa na machafuko.

Hivyo sehemu ya kubadili mentality hii ya watu ni kubadili uongozi.

Tatizo watu wengi wanapenda majibu rahisi kwa maswali magumu.

Wanakuwa kama wale Wamarekani wanaotaka kuwe na kidonge cha kutibu matatizo yote. Kidonge au app ya simu.

Wakati kuna matatizo mengine ya jamii hayana shortcut. Hutakiwi kuchagua uongozi mzuri tu na kuuachia kila kitu. Uongozi unatakiwa kusimamiwa, ama sivyo utayumba.

Sasa kuusimamia uongozi maana yake ni kufanya kazi. Kusoma manifesto za vyama, kusoma bajeti, kuchambua ripoti, kufuatikia kazi za CAG, kudai habari, kudai haki, kulazimisha wabunge wabadili sheria, kufungua kesi mahakamani, kuandamana, kuhakikisha chaguzi zinakuwa za huru na haki, kulinda kura, kuelimisha wananchi.

Hii ni kazi kubwa, watu wengi wanapenda kulalamika lakini ukiwaambia fanyeni kazi hii na hii kupata mabadiliko mnayoyataka, wanakuwa wagumu. Sio tu wale ambao hawana elimu, ambao kwa kiasi fulani unaweza kuwa excuse kwamba mtu kama hana elimu unategemea vipi achambue mikataba na mambo ya uchumi kwa kina, bali pia hata hao wanaoitwa wasomi wengi wao ni wazembe.

Ndiyo maana utawasikia wengi hata upinzani wakiongea ni kupigana madongo personally, ad hominem attack, logical fallacies.

Ukimuuliza mtu naomba unielezee falsafa ya uchumi ya CHADEMA inasemaje, vipaumbele vya sera za CHADEMA kwenye uchumi ni vipi? Vinatofautianaje na vya CCM, watu wengi, hata hao wanaoitwa wasomi, hawawezi kukuelezea vizuri.

Kuna siku tulikuwa tumekaa tunaongea watu mbalimbali. Akaja jamaa mmoja kiongozi ongozi wa CHADEMA. Akawa anaongea sana. Sasa rafiki yetu mmoja akamuuliza swali. CHADEMA ina mrengo gani wa kisiasa? Inasimamia wapi? Right wing,? Far right? Center right, centrist, center left au far left?

Jamaa akawa anajiumauma hajui kaulizwa nini. Badala ya kutoa mrengo, akawa anatoa slogan za "Peoples Power".

Mpaka Godbless Lema akaingilia kumuokoa kujibu swali vizuri.

Watu wengi hawajali sera. Wanataka mtanange wa kuitoa CCM tu.

Hii inatengeneza uwezekano wa kuitoa CCM halafu watu wasijue cha kufanya baada ya kuiondoa CCM.

Kwa sababu focus yao yote ilikuwa kuiondoa CCM.

umeandika vziru Kijana
 
🤣🤣
Mimi naona kama CCM hawatupi mateso ilitakiwa tupewe mateso makodi ya ajabu,hali iwe ngumu kweli kweli dadeki mpaka mtu akiwa njiani awe anaongea peke yake na kutoa ulimi nje kama Mbwa😁😁
 
Safi Sana Mkuu umeelezea vyema sana Sana. Watu wanaongea umbea umbea tu kwenye mambo mapana haelewi nini kinahitajika kwenye Taifa lao.
 
Habari Wakuu.

Ukiwa makini utaelewa kwamba hapa Tanzania shida sio CCM shida ni Watanzania wenyewe (ambao wanaunda CCM).

Hivyo basi hata kama chama kingine kikiingia Madarakani shida na vilio vitakuwa ni vilevile tena inawezekana ikawa zaidi. WHY? kwasababu shida sio chama shida ni watanzania wenyewe.
Hata kama tungeamua kuandaa orodha ya Watanzania waliolifikisha taifa hili katika kiwango cha sasa cha umasikini, wale wanaounda CCM wangekuwa miongoni mwa wa kwanza kwenye orodha hiyo, wakifuatiwa na wengine. Hakuna namna unaweza kutenganisha umasikini wa kifikra na wa kimwili unaolikumba taifa hili na nafasi ya CCM katika hilo. Tuseme ukweli bila kupepesa macho.
 
Shida sio Watanzania shida ni Ccm
 
Kama shida ni CCM kwa nini wana Nchi tusichukue maamuzi magumu au tupo kwa ule usemi NANI ATAMFUNGA PANYA KENGELE?
Paka mwenyewe simba kichaa anatafuna kila mmoja mwenye kuhoji juu ya huyu paka simba.
 
Hongera Sana Mkuu pia nimefurahi Sana kuona wewe ni miongoni mwa-watu walio nielewa hoja yangu pamoja sana Mkuu. Ujue Watu wanalalamika tu kuhusu chama lakini shida sio chama shida ni jamii(Watanzania )hata kama chama kikibadirishwa.
Chama ndicho kilichoanzisha na kuunda misingi ya hali hii tuliyonayo leo. CCM haijaingia madarakani juzi tu kimekuwepo tangu nchi hii ilipopata uhuru kupitia TANU, na baadaye kuungana na ASP kuunda CCM. Ndicho kilichoweka msingi wa mifumo yote hii mibovu tunayoiona leo. Haiwezekani kukiondoa kwenye lawama kama chanzo cha mmomonyoko wa maadili na mifumo duni ya kiuongozi na kijamii.Ni muhimu kukumbuka kwamba kilikuwa chama pekee hadi mwaka 1995, na falsafa yake ndiyo iliyotumika kama dira ya uongozi, maadili na maendeleo ya taifa. Falsafa zake hizi za kisiasa na kiitikadi ni mojawapo ya zilizoharibu kizazi, na sasa mnatafuta njia za kujisafisha dhidi ya madhara ambayo taifa hili litaendelea kuyabeba kwa miaka mingi ijayo.
 
CCM ndicho architect mkuu wa hali tunayoishuhudia leo, iwe ni watu kupigana vijembe, unafiki miongoni mwa viongozi, wasomi wazembe, au raia waliokosa uelewa wa kufuatilia mambo kwa kina. Hii ni kwa sababu chama hiki ndicho kilichoweka misingi ya mfumo wetu wa taifa tangu uhuru. Kama misingi hiyo ingekuwa imara na yenye maadili, leo tungekuwa tunavuna matunda ya maendeleo ya kweli. Huwezi kutenganisha msingi wa nyumba na uimara wa nyumba yenyewe. Vivyo hivyo, huwezi kutenganisha hali ya taifa hili na nafasi ya CCM. Hiki si chama tu kama vyama vingine, ni taasisi iliyoasisi mfumo mzima wa uongozi na maendeleo ya Tanzania. Hakujawahi kuwa na chama kingine kilichoshikilia hatamu kwa kipindi hicho chote, na kwa mantiki hiyo, hakuna namna ya kuitenganisha hali ya taifa letu na athari za CCM.
 
Hata kama tungeamua kuandaa orodha ya Watanzania waliolifikisha taifa hili katika kiwango cha sasa cha umasikini, wale wanaounda CCM wangekuwa miongoni mwa wa kwanza kwenye orodha hiyo, wakifuatiwa na wengine. Hakuna namna unaweza kutenganisha umasikini wa kifikra na wa kimwili unaolikumba taifa hili na nafasi ya CCM katika hilo. Tuseme ukweli bila kupepesa macho.
Ndiyo hao Watanzania ninazo wazungumzia Mkuu. Hutuwezi tukawa kila siku tunawalaum waliopita sisi pia tutalaumiwa mbeleni hivyo basi tutaendelea kutengeneza vizazi na vizazi vya kulaum. Kiufupi Kila kizazi kitakuwa kinasema fulani ndiyo mwenye makosa na kuendelea kubaki hapohapo kila Karne. So shida ni Watanzania sio vyama au chama .
 
Chama ndicho kilichoanzisha na kuunda misingi ya hali hii tuliyonayo leo. CCM haijaingia madarakani juzi tu kimekuwepo tangu nchi hii ilipopata uhuru kupitia TANU, na baadaye kuungana na ASP kuunda CCM. Ndicho kilichoweka msingi wa mifumo yote hii mibovu tunayoiona leo. Haiwezekani kukiondoa kwenye lawama kama chanzo cha mmomonyoko wa maadili na mifumo duni ya kiuongozi na kijamii.Ni muhimu kukumbuka kwamba kilikuwa chama pekee hadi mwaka 1995, na falsafa yake ndiyo iliyotumika kama dira ya uongozi, maadili na maendeleo ya taifa. Falsafa zake hizi za kisiasa na kiitikadi ni mojawapo ya zilizoharibu kizazi, na sasa mnatafuta njia za kujisafisha dhidi ya madhara ambayo taifa hili litaendelea kuyabeba kwa miaka mingi ijayo.
Mkuu Kwahiyo unaamini CCM ikitoka Madarakani kutakuwa na utofauti katika jamii yenye mindset kama hizi za kulaum watu waliopita.

Hutuwezi tukawa kila siku tunawalaum waliopita sisi pia tutalaumiwa mbeleni hivyo basi tutaendelea kutengeneza vizazi na vizazi vya kulaum. Kiufupi Kila kizazi kitakuwa kinasema fulani ndiyo mwenye makosa na kuendelea kubaki hapohapo kila Karne. So shida ni Watanzania sio vyama au chama .
 
Back
Top Bottom