Shida sio CCM shida ni Watanzania

Shida sio CCM shida ni Watanzania

CCM ndicho architect mkuu wa hali tunayoishuhudia leo, iwe ni watu kupigana vijembe, unafiki miongoni mwa viongozi, wasomi wazembe, au raia waliokosa uelewa wa kufuatilia mambo kwa kina. Hii ni kwa sababu chama hiki ndicho kilichoweka misingi ya mfumo wetu wa taifa tangu uhuru. Kama misingi hiyo ingekuwa imara na yenye maadili, leo tungekuwa tunavuna matunda ya maendeleo ya kweli. Huwezi kutenganisha msingi wa nyumba na uimara wa nyumba yenyewe. Vivyo hivyo, huwezi kutenganisha hali ya taifa hili na nafasi ya CCM. Hiki si chama tu kama vyama vingine, ni taasisi iliyoasisi mfumo mzima wa uongozi na maendeleo ya Tanzania. Hakujawahi kuwa na chama kingine kilichoshikilia hatamu kwa kipindi hicho chote, na kwa mantiki hiyo, hakuna namna ya kuitenganisha hali ya taifa letu na athari za CCM.
Mkuu shida ni Watanzania sio chama. Maelezo hayo tumeshajadiri Hapo juu. 👇👇

Lakini pia hatua moja ya kubadilisha jamii ni kujenga utamaduni wa kubadilisha chama tawala.

Kwa sasa hivi kuna watu wengi wameamini kwamba CCM ikitoka madarakani nchi itakuwa na machafuko. Kama wazee walivyoamini Nyerere akitoka madarakani nchi itakuwa na machafuko.

Hivyo sehemu ya kubadili mentality hii ya watu ni kubadili uongozi.

Tatizo watu wengi wanapenda majibu rahisi kwa maswali magumu.

Wanakuwa kama wale Wamarekani wanaotaka kuwe na kidonge cha kutibu matatizo yote. Kidonge au app ya simu.

Wakati kuna matatizo mengine ya jamii hayana shortcut. Hutakiwi kuchagua uongozi mzuri tu na kuuachia kila kitu. Uongozi unatakiwa kusimamiwa, ama sivyo utayumba.

Sasa kuusimamia uongozi maana yake ni kufanya kazi. Kusoma manifesto za vyama, kusoma bajeti, kuchambua ripoti, kufuatikia kazi za CAG, kudai habari, kudai haki, kulazimisha wabunge wabadili sheria, kufungua kesi mahakamani, kuandamana, kuhakikisha chaguzi zinakuwa za huru na haki, kulinda kura, kuelimisha wananchi.

Hii ni kazi kubwa, watu wengi wanapenda kulalamika lakini ukiwaambia fanyeni kazi hii na hii kupata mabadiliko mnayoyataka, wanakuwa wagumu. Sio tu wale ambao hawana elimu, ambao kwa kiasi fulani unaweza kuwa excuse kwamba mtu kama hana elimu unategemea vipi achambue mikataba na mambo ya uchumi kwa kina, bali pia hata hao wanaoitwa wasomi wengi wao ni wazembe.

Ndiyo maana utawasikia wengi hata upinzani wakiongea ni kupigana madongo personally, ad hominem attack, logical fallacies.

Ukimuuliza mtu naomba unielezee falsafa ya uchumi ya CHADEMA inasemaje, vipaumbele vya sera za CHADEMA kwenye uchumi ni vipi? Vinatofautianaje na vya CCM, watu wengi, hata hao wanaoitwa wasomi, hawawezi kukuelezea vizuri.

Kuna siku tulikuwa tumekaa tunaongea watu mbalimbali. Akaja jamaa mmoja kiongozi ongozi wa CHADEMA. Akawa anaongea sana. Sasa rafiki yetu mmoja akamuuliza swali. CHADEMA ina mrengo gani wa kisiasa? Inasimamia wapi? Right wing,? Far right? Center right, centrist, center left au far left?

Jamaa akawa anajiumauma hajui kaulizwa nini. Badala ya kutoa mrengo, akawa anatoa slogan za "Peoples Power".

Mpaka Godbless Lema akaingilia kumuokoa kujibu swali vizuri.

Watu wengi hawajali sera. Wanataka mtanange wa kuitoa CCM tu.

Hii inatengeneza uwezekano wa kuitoa CCM halafu watu wasijue cha kufanya baada ya kuiondoa CCM.

Kwa sababu focus yao yote ilikuwa kuiondoa CCM.
 
Mfumo ccm kwa kufafanulia zaidi kwa kuwa sifa ya jamii yako ni kujua tu kusoma na kuandika pekee
Tuna wasomi wengi sana Mkuu. Lakini Kwa Bahati mbaya zamani tulikuwa tunapata tabu Sana kuwaelimisha wajinga sasaizi tunapata tabu sana kuwaelimisha wasomi.
 
Tuna wasomi wengi sana Mkuu. Lakini Kwa Bahati mbaya zamani tulikuwa tunapata tabu Sana kuwaelimisha wajinga sasaizi tunapata tabu sana kuwaelimisha wasomi.
Kama chawa kijani sio?
 
Habari Wakuu.

Ukiwa makini utaelewa kwamba hapa Tanzania shida sio CCM shida ni Watanzania wenyewe (ambao wanaunda CCM).

Hivyo basi hata kama chama kingine kikiingia Madarakani shida na vilio vitakuwa ni vilevile tena inawezekana ikawa zaidi. WHY? kwasababu shida sio chama shida ni watanzania wenyewe.
Shida ni
Wasafi
Efm
Ufm
Wnatangaza Simba vs yanga tu
 
Shida sio CCM wala Wananchi shida hapo ni Vyama vya siasa..vimeshindwa kuendesha siasa za hoja badala yake vimejikita kwenye udini,chuki,mauaji na umimi huku vikibakia kuwacha njia panda wapiga kura ambao hawarambi asali..wapiga kura hawaitaji hayo wao wanahijaji hoja mbadala na matokeo halisi ya hoja hzo zitakozoweza kulifikisha taifa mbele nasio mipasho kama waimba taarabu..hvo basi TANZANIA BILA VYAMA VYA SIASA INAWEZAKANA.
 
Mkuu Safi sana maelezo yako mazuri, wewe ni moja ya Watanzania wanaojielewa pia naongezea Hapo kwenye vyama vya siasa ndiyo Watanzania wenyewe hao ninao wasema.
 
Mkuu Safi sana maelezo yako mazuri, wewe ni moja ya Watanzania wanaojielewa pia naongezea Hapo kwenye vyama vya siasa ndiyo Watanzania wenyewe hao ninao wasema.
ukisema watanzania wenyewe ukumbuke ndani ya hao watanzania kuna wengine hawana sare wala kadi sasa hawa ambao hawana sare wala kadi ndo mnawachezesha kama ngoma..mfano sahv CHADEMA wanasema no reforms no election hapo hapo waliounda hyo no reforms no election baadhi wametimkia CHAUMMA kwahyo hapo tuna aminishwa mtu na sio chama ??Haya basi wapinzani wengine wabariki hakuna na wao wanahoja zao zinamashiko wanasema sisi tutashiriki uchaguzi mfano, ACT WAZALENDO haya yule aliepewa pendekezo ya reforms bado anachakata na hajatoa majibu yoyote hapo na tunaelekea uchaguzi ???? wapinzani wengine bado hawajulikani wapo upande upi..kwahyo unagundua kuwa mambo ni vuluvulu bila mpangilio, sasa kwasisi tusiokuwa na sare wala kadi tunasema hvi:TANZANIA BILA VYAMA VYA SIASA INAWEZEKANA.
 
CCM ndicho architect mkuu wa hali tunayoishuhudia leo, iwe ni watu kupigana vijembe, unafiki miongoni mwa viongozi, wasomi wazembe, au raia waliokosa uelewa wa kufuatilia mambo kwa kina. Hii ni kwa sababu chama hiki ndicho kilichoweka misingi ya mfumo wetu wa taifa tangu uhuru. Kama misingi hiyo ingekuwa imara na yenye maadili, leo tungekuwa tunavuna matunda ya maendeleo ya kweli. Huwezi kutenganisha msingi wa nyumba na uimara wa nyumba yenyewe. Vivyo hivyo, huwezi kutenganisha hali ya taifa hili na nafasi ya CCM. Hiki si chama tu kama vyama vingine, ni taasisi iliyoasisi mfumo mzima wa uongozi na maendeleo ya Tanzania. Hakujawahi kuwa na chama kingine kilichoshikilia hatamu kwa kipindi hicho chote, na kwa mantiki hiyo, hakuna namna ya kuitenganisha hali ya taifa letu na athari za CCM.
Kabla ccm haijawepo 1977 ilikuwepo TANU na ASP!!

Majasusi wa nchi walipaswa kuzifinyanga siasa zetu ziwe na afya na ustawi wa taifa na sio magenge Fulani kama sasa!!

Baraza la uslama la taifa Lili lala usingizi!!?
 
Back
Top Bottom