Hongera Sana Mkuu pia nimefurahi Sana kuona wewe ni miongoni mwa-watu walio nielewa hoja yangu pamoja sana Mkuu. Ujue Watu wanalalamika tu kuhusu chama lakini shida sio chama shida ni jamii(Watanzania )hata kama chama kikibadirishwa.
Naam,
Lakini pia hatua moja ya kubadilisha jamii ni kujenga utamaduni wa kubadilisha chama tawala.
Kwa sasa hivi kuna watu wengi wameamini kwamba CCM ikitoka madarakani nchi itakuwa na machafuko. Kama wazee walivyoamini Nyerere akitoka madarakani nchi itakuwa na machafuko.
Hivyo sehemu ya kubadili mentality hii ya watu ni kubadili uongozi.
Tatizo watu wengi wanapenda majibu rahisi kwa maswali magumu.
Wanakuwa kama wale Wamarekani wanaotaka kuwe na kidonge cha kutibu matatizo yote. Kidonge au app ya simu.
Wakati kuna matatizo mengine ya jamii hayana shortcut. Hutakiwi kuchagua uongozi mzuri tu na kuuachia kila kitu. Uongozi unatakiwa kusimamiwa, ama sivyo utayumba.
Sasa kuusimamia uongozi maana yake ni kufanya kazi. Kusoma manifesto za vyama, kusoma bajeti, kuchambua ripoti, kufuatilia kazi za CAG, kudai habari, kudai haki, kulazimisha wabunge wabadili sheria, kufungua kesi mahakamani, kuandamana, kuhakikisha chaguzi zinakuwa za huru na haki, kulinda kura, kuelimisha wananchi.
Hii ni kazi kubwa, watu wengi wanapenda kulalamika lakini ukiwaambia fanyeni kazi hii na hii kupata mabadiliko mnayoyataka, wanakuwa wagumu. Sio tu wale ambao hawana elimu, ambao kwa kiasi fulani unaweza kuwa excuse kwamba mtu kama hana elimu unategemea vipi achambue mikataba na mambo ya uchumi kwa kina, bali pia hata hao wanaoitwa wasomi wengi wao ni wazembe.
Ndiyo maana utawasikia wengi hata upinzani wakiongea ni kupigana madongo personally, ad hominem attack, logical fallacies.
Ukimuuliza mtu naomba unielezee falsafa ya uchumi ya CHADEMA inasemaje, vipaumbele vya sera za CHADEMA kwenye uchumi ni vipi? Vinatofautianaje na vya CCM, watu wengi, hata hao wanaoitwa wasomi, hawawezi kukuelezea vizuri.
Kuna siku tulikuwa tumekaa tunaongea watu mbalimbali. Akaja jamaa mmoja kiongozi ongozi wa CHADEMA. Akawa anaongea sana. Sasa rafiki yetu mmoja akamuuliza swali. CHADEMA ina mrengo gani wa kisiasa? Inasimamia wapi? Right wing,? Far right? Center right, centrist, center left au far left?
Jamaa akawa anajiumauma hajui kaulizwa nini. Badala ya kutoa mrengo, akawa anatoa slogan za "Peoples Power".
Mpaka Godbless Lema akaingilia kumuokoa kujibu swali vizuri.
Watu wengi hawajali sera. Wanataka mtanange wa kuitoa CCM tu.
Hii inatengeneza uwezekano wa kuitoa CCM halafu watu wasijue cha kufanya baada ya kuiondoa CCM.
Kwa sababu focus yao yote ilikuwa kuiondoa CCM.