Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 62,255
- 109,195
Wadau kuna hali isiyo ya kawaida muda wa siku karibia nne sasa katika king'amuzi cha startimes. Katika king'amuzi hicho unaweza kuona chanel 2 tu za nyumbani iwapo hujalipia kifurushi chochote. Chanel hizo ni TBC1 na TV1 pekee yake. Nijuavyo mimi sheria inataka chanel zote za ndani zionekane hata kama hujalipia kifurushi chochote, channel hizo ni kama Channel 10, ITV, startv nk. Sasa ukifungua chanel hizo inakuambia kwamba hiyo ni chanel inayohitaji malipo.
Sasa naomba kujua mamlamka ya mawasiliano TCRA mko wapi watu wanafanya kinyume na sheria na hakuna hatua stahiki zinachukuliwa na wala kituo hicho hakitoi taarifa yoyote kwa umma? Inakuwaje mtu akitukana inakuwa rahisi kumkamata lakini kituo kikubwa kama hicho kinakiuka sheria ya nchi bila taarifa kutolewa wala hatua kuchukuliwa? Ama na wenyewe walikuwa wakwepa kodi kama tetesi za kituo kingine zinazoendelea huku mitandaoni?