Shida ni kwenye king'amuzi cha startimes? TCRA mko wapi?

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
58,677
102,721
Wadau kuna hali isiyo ya kawaida muda wa siku karibia nne sasa katika king'amuzi cha startimes. Katika king'amuzi hicho unaweza kuona chanel 2 tu za nyumbani iwapo hujalipia kifurushi chochote. Chanel hizo ni TBC1 na TV1 pekee yake. Nijuavyo mimi sheria inataka chanel zote za ndani zionekane hata kama hujalipia kifurushi chochote, channel hizo ni kama Channel 10, ITV, startv nk. Sasa ukifungua chanel hizo inakuambia kwamba hiyo ni chanel inayohitaji malipo.

Sasa naomba kujua mamlamka ya mawasiliano TCRA mko wapi watu wanafanya kinyume na sheria na hakuna hatua stahiki zinachukuliwa na wala kituo hicho hakitoi taarifa yoyote kwa umma? Inakuwaje mtu akitukana inakuwa rahisi kumkamata lakini kituo kikubwa kama hicho kinakiuka sheria ya nchi bila taarifa kutolewa wala hatua kuchukuliwa? Ama na wenyewe walikuwa wakwepa kodi kama tetesi za kituo kingine zinazoendelea huku mitandaoni?
 
Mimi nimeacha kuangalia tv muda mrefu habari zote napata millard ayo na muungwana blogg
 
Channels zote siku hizi unalipia no free lunch mkubwa kuanzia mwezi wa saba
 
Hata mimi yamenukita wiki moja iliyopita.Nilibakiwa na channel moja ya TBC 1 tu.Nilipowapigia simu wakaniambia ni tatizo la kiufundi na wakati huo huo wakanitaka nilipie kwa hoja sijalipia muda mrefu.Baada ya kulipia channel zikarudi na tatizo la kiufundi likawa limeisha automatically!!

TCRA kuna tatizo na wanapaswa kuwajibika kama sio kuwajibishwa.
 
Channels zote siku hizi unalipia no free lunch mkubwa kuanzia mwezi wa saba

Hakuna anayetaka bure, ila tunaangalia sheria inasemaje. Kama sheria imebadilika inabidi tutangaziwe, na isitoshe tunajua serekali hii ni yetu wanyonge kama tunavyotangaziwa na rais wetu kila apandapo jukwaani. TCRA tunaitaka itutangazie tujue nini kinaendelea, mbona TV1 tunaona bure na hiyo TBC1?
 
eti kuna tatizo la kiufundi ili kupata tena channel za ndani lipia 5000 tu...yaan tatizo liwe kwao halaf mm ndo nlipie...hio TBC1 wataangalia wenyew...silipii tena
 
Kuna aina mbili za pay Tv. DTH na DTT. DTH ni inayotumia satellite dish na hii sheria haimbani mtoa huduma kuonesha local channels bure kama hujafanya malipo lakini DTT ambazo hutumia antenna ni lazima kuacha local TVs hata kama malipo yamekwisha.

DTH stands for Direct To Home and DTT stands for Digital Terrestrial Television
 
Hakuna anayetaka bure, ila tunaangalia sheria inasemaje. Kama sheria imebadilika inabidi tutangaziwe, na isitoshe tunajua serekali hii ni yetu wanyonge kama tunavyotangaziwa na rais wetu kila apandapo jukwaani. TCRA tunaitaka itutangazie tujue nini kinaendelea, mbona TV1 tunaona bure na hiyo TBC1?
Ndugu yangu hizo free channels tano serikali ilikuwa inazilipia so kuanzia mwezi wa saba serikali imejiondoa kulipia kwa hiyo hata tcra wanajua hilo. Na hata mungi msemaji wa tcra alisha elezea hicho kitu so acha tutafunwe
 
Ndugu yangu unajua usemalo ama na wewe umeamua kusema tu ili uonekane wangalau unakwenda na wakati? Hebu niambie kama unataka uone hizo chanel tano serekali ilizojitoa unatakiwa kulipia shilingi ngapi kwa mwezi? Hapo ndio nitajua unajua unalosema, vinginevyo na wewe utakuwa umeamua tu kupiga siasa hapa jukwaani.
 
Mimi wameikatia toka julay 1 wakanibakishia TBC !!

.kwanini wanichagulie tv ya kuangalia mpaka hapo ntakapolipia ?

Nimelipia 12000 tatizo likaisha SAA hiyo hiyo!

Turuhusiwe kuchagua Chanel itwatakayonibakishia mpaka nitakapopolipia !
 
Nina
Ndugu yangu unajua usemalo ama na wewe umeamua kusema tu ili uonekane wangalau unakwenda na wakati? Hebu niambie kama unataka uone hizo chanel tano serekali ilizojitoa unatakiwa kulipia shilingi ngapi kwa mwezi? Hapo ndio nitajua unajua unalosema, vinginevyo na wewe utakuwa umeamua tu kupiga siasa hapa jukwaani.
Jina uhakika ninacho kisema serikali ilikuwa ina lipia hizo channels ili watu waone bure but from July wamiliki walipewa barua ya kuchagua channel moja itakayokuwa free azamtv tbc 1, dstv channel ten, star time tbc. Hata continental decoder lazima ulipie ndiyo utaona channel japo kuwa na wao hawatumii satellite wanatumia minara ya ardhini. Na mungi msemaji wa tcra alisha elezea hiki kitu akasema wana maongezi na serikali ili kuona kuona kama inaendelea kulipia hizo five local channels.
 
Nashukuru kwa maelezo yako marefu, kimsingi siyapingi lakini nayaweka kwenye kundi la maneno ya kijiweni. Ninachotaka unimbie ili uweze kuona wangalau hizo local channels tano unatakiwa uweke sh ngapi kwa mwezi? Mfano hao startimes, kinyume na hapo ni kwamba unataka kusema maneno ya kusadikika kwani sheria bado iko wazi na haijabadilishwa, labda kama kuna ukiukwaji wa sheria za nchi, na hili TCRA wanapaswa kulitolea ufafanuzi.
 
Wadau kuna hali isiyo ya kawaida muda wa siku karibia nne sasa katika king'amuzi cha startimes. Katika king'amuzi hicho unaweza kuona chanel 2 tu za nyumbani iwapo hujalipia kifurushi chochote. Chanel hizo ni TBC1 na TV1 pekee yake. Nijuavyo mimi sheria inataka chanel zote za ndani zionekane hata kama hujalipia kifurushi chochote, channel hizo ni kama Channel 10, ITV, startv nk. Sasa ukifungua chanel hizo inakuambia kwamba hiyo ni chanel inayohitaji malipo.

Sasa naomba kujua mamlamka ya mawasiliano TCRA mko wapi watu wanafanya kinyume na sheria na hakuna hatua stahiki zinachukuliwa na wala kituo hicho hakitoi taarifa yoyote kwa umma? Inakuwaje mtu akitukana inakuwa rahisi kumkamata lakini kituo kikubwa kama hicho kinakiuka sheria ya nchi bila taarifa kutolewa wala hatua kuchukuliwa? Ama na wenyewe walikuwa wakwepa kodi kama tetesi za kituo kingine zinazoendelea huku mitandaoni?
Rais kasema mkiangalia tv hamtafanya kazi kwaio itafika kipindi tv na radio stations zote zitakuwa zinawashwa usiku tu bas
 
Poa mkubwa basi ma
Nashukuru kwa maelezo yako marefu, kimsingi siyapingi lakini nayaweka kwenye kundi la maneno ya kijiweni. Ninachotaka unimbie ili uweze kuona wangalau hizo local channels tano unatakiwa uweke sh ngapi kwa mwezi? Mfano hao startimes, kinyume na hapo ni kwamba unataka kusema maneno ya kusadikika kwani sheria bado iko wazi na haijabadilishwa, labda kama kuna ukiukwaji wa sheria za nchi, na hili TCRA wanapaswa kulitolea ufafanuzi.
Poa mkubwa maneno yangu ni ya kijiweni endelea kulipia tu. Najua ninacho kisema kama huniamini tuishie hapo lakini hutasikia tamko la serikali wala tcra hii biashara iliisha Isha ni mwendo wa kulipia from star times, continental, azam tv, ting, dstv.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom