Shibuda ni mpinzani?

Shibuda ni mpinzani?

Tuhuma za Masalia kulipwa na Shibuda zina ukweli wowote?
 
Kifo cha mfa maji ndicho kinachomkumba shibuda
 
Hebu tuchepuke kutoka kumwangalia Shibuda binafsi.

Je nyuma yake wapo akina nani? Kwa maslahi gani?
 
Kinachomsibu shibuda ni kuwa mkwelii sana .angefaa sana kwenye siasa za kimarekani lakini kwa hapa tz atapata shida sana.lakini asikate tamaa kwani anaonyesha njia.ipo siku atakua shujaa wa kweli.
 
Naona tumuweke kwenye fungu linalomstahiki yaani "mwanasiasa" kwasababu chache hapo chini;
1. Ni bingwa wa kufanya mambo yasiyo "hasa" yaani hiyo ni sifa ya hao wote! Wanasiasa ni waongo wote.
2. Anajuwa kutumia ujinga na shida za watu kujitafutia umaarufu. Hao wote ndio sifa yao kubwa.
3. Anafuata upepo unakoelekea. Ni sifa kubwa ya watu hao na ukishindwa kuangalia upepo unaenda na maji. Kwake yeye ameshaangalia kuwa maslaha yake aliko ni ya muda kwani alitumiwa na muda mfupi atatupwa hivyo amekaa mguu nje mguu ndani.
4. Anajuwa kuwa siasa ni ajira yenye ushindani mkubwa hivyo hutakiwi kuapia kutotenda jambo na kama ilivyoajira nyengine awe tayari kutumika popote patakapompa maslahi. Ni nani kati ya wanasiasa wetu ambae hajafika hapo alipo kwa kutumika vyama tofauti? Kwa mfano nani alidhani Hamad Rashid atakuwa alipo sasa?

Halafu mwanasiasa anakuwa "mpinzani" pale tu anapokosa nafasi katika utawala hivyo neno uhalisia wa upinzani ni kufanya siasa nje ya utawala. Ingekuwa jambo zuri kama wangeitwa jina jengine badala ya wapinzani kwani iwapo siasa lengo lake ni kuleta utawala Bora na hali bora za maisha ya wananchi yule anaeitwa mpinzani wa hilo anakuwa na nafasi gani kwa wananchi?

Pengine Shibuda kalifahamu hili na ndio maana anashirikiana na wa pande zote yaani wale walio nje ya utawala na walio ndani ya utawala kwa faida ya wananchi na huo ndio utakuwa mtaji wake atakapoenda popote!
 
Siyo mnafiki na mlamba viatu.

Siyo ajabu umeshindwa kumuelewa kwa sababu siasa za Tanzania zimejaa wanasiasa wanafiki na waongo ambao kwa uwingi wao, wanakufanya kuamini kama kile wanachokifanya ndiyo sahihi.

Wanasiasa kama Mh. shibuda ni nadra kuwapata Tanzania.
 
shibuda alipotoswa na chama chake alishawishiwa kuhamia CHADEMA ili akatetee jimbo lake, mara tu baada ya kushinda na CCM baada ya kutolewa jasho kwenye kura za urais 2010 ikabidi watumie sarakasi zao kuanza kucheki profile za kila mbunge aloshinda kupitia CHADEMA ndipo kitengo cha kijasusi cha CCM kikabaini wabunge kadhaa wa CHADEMA wanaoweza kuwatumia katika harakati zao za kupunguza speed ya CHADEMA kuelekea 2015, kumbuka kwa CCM mara tu uchaguzi ukiisha ni mwanzo wa maandalizi mengine ya uchaguzi unaofuata...
bilashaka nimeeleweka.
 
sidhani kama haxo maneno uliyomsifia nayo kama yana hekima kwa nchi kama Tz inayosifika kuwa na democrasia ya midomoni mwa watu pasipokua na vitendo vya democrasia

hebu leta yako yenye hekima tuone kama tutayasifia........
 
Ngekewa kwa hivyo unatuaminisha kwamba wanasiasa ndivyo walivyo?
Je tunapaswa sasa kuwaamini?

Iweje tunafuata legacy zao huku tukitambua moyoni kwamba hawana uhalisia wa kiimani?

Shibuda yupo peke?
 
Last edited by a moderator:
Tuhuma za Masalia kulipwa na Shibuda zina ukweli wowote?
mkuu Msanii hizo tuhuma si za kweli, atawalipa kwa maslahi yapi?
kama shibuda anawalipa masalia kuiharibu chadema ambayo na yeye yumo, manake pesa anazotumia zinatoka CCM ila zinapitia kwake kama mhasibu tu wa kuwalipa wasaliti,
ntapinga hadi kesho, shibuda hawezi kutoa pesa zake kuwalipa watu wanaoivuruga chadema, ila pesa hizo zinatoka CCM kupitia kwake, hilo siwezi kuthibisha.
 
Last edited by a moderator:
Ana taabia za kipopo au kinyonga!hubadili rangi na msimamo wake pindi anapokuwa na kikundi cha watu flani!Watu kama hawa ni wabaya sana.
 
....ntapinga hadi kesho, shibuda hawezi kutoa pesa zake kuwalipa watu wanaoivuruga chadema, ila pesa hizo zinatoka CCM kupitia kwake, hilo siwezi kuthibisha.
Hapo mkuu umenipa jibu kwamba Shibuda ana walio nyuma yake (ingawa ngumu kuthibitisha).

Kwa faida gani hasa?
 
Hapo mkuu umenipa jibu kwamba Shibuda ana walio nyuma yake (ingawa ngumu kuthibitisha).

Kwa faida gani hasa?
acha utani mkuu! hujui faida za usaliti?
nyerere aliwahi kutoa mfano wa zuzu alopewa kipande cha chupa akiambiwa kuwa ni almasi halafu yeye akatoa kipande cha almasi, hahahahahahahahaha....
pesa, vyeo ndo faida ya usaliti thou mara nyingi wasaliti wanatumika kwa mda tu halafu wanatoswa bila vyeo wala pesa... (mfano Tambwe Hizza), walioambulia vyeo kama Ubunge mfano Mbatia NCCR
 
Shibuda ni hiyo namba 2, mpinzani wa wapinzani i.e. CHADEMA.

Uwepo wa huyu jamaa CHADEMA ni funzo kubwa kwetu kwa miaka ijayo kutopokea watu wa calibre yake ambao ni wengi mno kwenye siasa zetu ktk ngazi za mtaa mpaka urais.
 
Shibuda ni hiyo namba 2, mpinzani wa wapinzani i.e. CHADEMA.

Uwepo wa huyu jamaa CHADEMA ni funzo kubwa kwetu kwa miaka ijayo kutopokea watu wa calibre yake ambao ni wengi mno kwenye siasa zetu ktk ngazi za mtaa mpaka urais.
Unaniaminisha kwamba CHADEMA hawakufanya vetting kabla ya kumpa jukumu la kugombea ubunge?

Ni kosa ambalo serikali ya sasa inalifanya kwa ukamilifu na kuishia kupata viongozi mfano wa Mulugo n.k.
 
hata siku moja hutowasikia ccm au magamba wanamsema shibuda kwamba ataifuruga chadema,ila wale viongozi wetu shupavu ndio wanaowasema,yaani wao mbaya wetu ndio mzuri wao na mzuri wetu kwao ndi mbaya
 
hebu tudadavulie unafiki wake mkuu.

Inawezekana ni kipofu hajui afanyalo labda, au waonaje wewe?

anajua sana afanyalo ila ni tabia yake na tabia haina dawa, huyo angekuwa mdada/mmama saa hizi angekuwa na chuo cha 10
 
Njaa tu inamsumbua, yeye ni ndumila kuwili, kama bendera vile anafuata upepo, lakini pia inasemekana aliungana na Kabwe kuunda pm7 na CHAUMMA
 
Back
Top Bottom