Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,949
- 38,700
Inawezekana kweli ni mpinzani makini.
Nimeangalia mwenendo wake nimepata maswali mawili.
Ametuhumiwa kuihujumu CHADEMA kwa kuwaunga mkono Masalia na makundi ya wanachama wanaokivuruga, kwa nini hachukuliwi hatua? Ana turufu gani kwa chama? Au yanayosemwa dhidi yake ni propaganda za uchonganishi?
Nimeangalia mwenendo wake nimepata maswali mawili.
- Ni mpinzani dhidi ya mfumo mbovu wa CCM?
Aliondoka kwa mbwembwe CCM hasa baada ya kutoshwa kugombea jimboni kwake kwa tiketi ya CCM, Ikumbukwe kwamba dhambi aliyoifanya ni kutangaza kutaka kupambana na JK kwenye mchakato wa uteuzi wa mgombea wa urais. - Ni mpinzani wa upinzani?
Kwa kauli na tambo zake amekuwa akibeza chama chake cha sasa na kuwakosoa kwa wazi viongozi wake na kuukosoa mfumo ama utaratibu wa chama hata kufikia kuchombeza kuwa CHADEMA kimejaa undugunaizesheni.