MKUU
Ngekewa,
Nadhani mwelekeo wako ni wa mtu aliyekata tamaa, watu waoga na wanaokata tamaa ni watu wasiofanikiwa maishani, japo nakuombea wewe ufanikiwe.
Naamini hakuna siasa za namna ya siasa za shibuda, ila kuna watu wa aina ya shibuda..anachokifanya yeye ni ubinafsi tu, yaani anatafuta namna ya siasa zinazoweza kumtambulisha yeye binafsi, ni selfcentred kind of person..siasa ni muunganiko wa watu wenye malengo fulani kwa kutumia serikali, lakini Shibuda ana aina yake na mfumo wake wa siasa..siasa za popo, si ndege wala si mnyama na kwa vyovyote aina ya siasa zake haitamvusha 2015! Ni vigumu kuaminika na hatoaminika tena kwa wapiga kura wake, awe amegombea cdm, ccm au binafsi..
Mark my word!
Wapo watu safi kwenye siasa, lakini siasa ni upinzani, kwa hiyo si wakati wote wanaonekana hivyo, ndo maana leo weka jina lolote la Mwanasiasa utapata wanaomsifu na watakaomponda lakini hiyo haiufanyi mchezo wote wa siasa uwe ni wa wezi watupu au wabinafsi watupu japo wezi wapo, hata kwenye dini wapo pia, hapa ni suala la mtu binafsi, lakini shibuda anataka asiwe na upande, anataka Ccm wampende na Chadema wasimchukie, huu ni unafiki, hakuna kitu kama hicho na hasa siasa zetu, atapotea kabisa maana kote hatoaminika!..ndo anakoelekea, kushindwa vibaya sana na kupotea