Shibuda Kurudi CCM Leo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda Kurudi CCM Leo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 9, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG] [​IMG]

  Jangwani kungechangamka kama Shibuda angerudia CCM leo. Kama mkutano huo ulipangwa mapema kabla ya ule wa Chadema, basi Chadema wangefanya papara kuhusu Shibuda mkutano huo lingekuwa tunda lake. Lakini hakuna pa kusimamia maana mti umeteleza. Hawa CCM wanamizengwe mingi ambayo ukituliza kichwa wanabaki kama mpira unaogonga ukuta na kurudi ulikotoka.
   
 2. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kuharisha leo ndio ugonjwa mlio nao cdm, nasikia matumbo wote yanawauma
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  CCM yamwaga mamilioni kuivaa CHADEMA
  CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimedaiwa kutumia mamilioni ya fedha kugharimia mkutano wake wa hadhara unaotarajiwa kufanyika leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, katika kile kinachoonekana kujibu mapigo ya mahasimu wao, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


  Kinyume na madai ya CCM kwamba lengo la mkutano huo ni kuhamasisha uhai wa chama na kutolea ufafanuzi mambo kadhaa yanayojitokeza ndani ya chama hicho, lakini duru za siasa zimedai kuwa, lengo kuu ni kujipima nguvu na CHADEMA ambacho wiki mbili zilizopita kilifanya mkutano wa hadhara katika viwanja hivyo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

  Katika mkutano huo wa CHADEMA ambao ulirushwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha ITV, maelfu ya wanachama waliofurika, walifika katika viwanja hivyo kwa njia zao bila kusombwa na magari, wala kupokea posho. Ili kuhakikisha mkutano wa leo unafunika ule wa CHADEMA kwa kupata watu wengi, CCM imeamua kuwasafirisha wajumbe wake kwa magari makubwa ya kukodi kama vile malori na mabasi kutoka kila tawi na kuwafikisha katika viwanja hivyo.


  Mbali ya kusombwa kwa magari, CCM pia imeamua kugawa bure fulana na kofia, na kuna madai kuwa chama hicho kitatoa posho kwa wanachama wake watakaohudhuria mkutano huo.
  Mkakati wa kuhakikisha mkutano huo unapata watu wengi, umesukwa kuanzia ngazi ya matawi, wilaya hadi mkoa kwa zaidi ya wiki moja sasa.


  Kana kwamba hiyo, haitoshi, CCM imeandaa baadhi ya wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava) watakaotumbuiza mapema kabla ya kuanza mkutano kwa nia ya kuwavuta wanachama.
  Baadhi ya wasanii hao ni Diamond, Marlaw, Frola Mbasha na wengine wengi ambao walipata kutumika wakati wa mikutano ya kampeni ya Rais Jakaya Kikwete.


  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Uenezi na Itikadi CCM, Nape Nnauye alisema baadhi ya mawaziri na makada maarufu ndani ya chama hicho tawala, watahutubia katika mkutano huo.
  Alisema mkutano huo unaotarajiwa kuwa wa aina yake, ulipangwa siku nyingi kwa lengo la kuwakutanisha pamoja viongozi wa chama wa mashina na matawi waliochaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi wa CCM unaoendelea katika ngazi mbalimbali.


  "Kuna vyombo vimesema mkutano huo utahutubiwa na Mzee Mkapa, Mwinyi. Hiyo sio kweli maana hata mwenyekiti wa chama taifa, Rais Jakaya Kikwete hatakuwepo jukwaani," alisema Nape.
  Aliwataja mawaziri watakaohutubia mkutano huo kuwa ni pamoja na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano), Steven Wassira, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC), Abdulrahman Kinana na Nape mwenyewe.


  "Mzee Kinana atazungumzia masuala ya katiba na sheria na atatoa kauli kuhusiana na vurugu zilizotokea visiwani Zanzibar na kueleza msimamo wa chama kuhusu kikundi cha Uamsho cha visiwani humo kinachodaiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo.
  "Wasira atajikita kwenye uchumi, Dk. Mwakyembe atazungumzia jinsi serikali inavyoshughulikia masuala ya uchukuzi, Magufuli atazungumzia utekelezaji wa ilani katika eneo la ujenzi na mkakati wa kuondoa foleni jijini Dar es Salaam," alisema Nape.

  Kama ilivyokuwa kwa CHADEMA, CCM nao wameamua kurusha mkutano huo moja kwa moja kupitia kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) na Televisheni ya ITV na baadhi ya vituo vya redio.
  Aliwataka wananchi, wanachama wa CCM na wakereketwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo ili kuwasikiliza viongozi wa chama na serikali watakaozungumzia kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015.
   
 5. k

  kitero JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 563
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa hawa wazee wanapigania khanga za kazi gani? ingekuwa kofia angalau mpaka khanga wanapigania hii noma.Hii kazi ya kugawa khanga ilitakiwa ifanywe na UWT
   
 6. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Shibuda akitoka cdm nitalia kwa furaha
   
 7. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  mkuu hauko mbali sana na ukweli... I have seen him yesterday sehemu fulani, don't trust the Guy !
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hii picha ha ha ha ha ha ha.

  [​IMG]
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nape kasema mkutano huo uliandaliwa muda mrefu kabla ya ule wa Chadema.
  Kauli hiyo ni dalili tosha kwamba mizengwe ya Shibuda nyuma ya pazia kulikuwa na msukumo fulani, na kama mtakumbuka Shibuda alisema akifukuzwa uanachama atazunguka nchi nzima kuishtaki Chadema kwa wapiga kura.

  Shibuda hana hoja nzito ya kutangaza kujivua Uchadema leo kwa vile kitendawili kimeteguliwa.

  Zengwe hilo lililosukwa kwa ustadi mkubwa kwa malengo kwamba viongozi wa Chadema wangekurupuka tu kuchukua haraka hatua bila kutuliza kichwa, leo pale
  Chadema Square (Jangwani) wangekuwa na pakusimamia kuisema Chadema kwa kumtumia Shibuda. Busara ya viongozi wa Chadema imewababaisha CCM na kubaki wameduwaa. Hiki ndicho nilichokuwa nasema mara kadhaa subira ni muhimu, mambo ya papo kwa papo si uamuzi wa busara na hekima.
   
 10. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Duuh! SUBIRA HUVUTA HERI
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Yes it is. Wanasaikolojia husema usipende kutoa matamko wakati umeudhika kwani ukituliza kichwa baada ya kutulia unaweza kufikiri vizuri zaidi na kutoa jibu ambalo lina-make sense. Kawia ufike.
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Hii ndiyo hali halisi ya Jangwani leo
   
 13. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Kinacho onekana hapa ni kwamba CCM wanatumia UMASKINI na UJINGA wa Wadanganyika kuwarubuni kwa Khanga,Kofia, T-shirts na Pilao. Kwa Watanzania makini hawawezi kudanganyika na upuuzi huu wa CCM.

  Chama cha CHADEMA na wanachama wake kimethibitisha kuwa hakiwezi kudanganyika tena. Nawashauri Watanzania wote kwa ujumla wao waikatae CCM na rushwa zake za kinafiki!

   
 14. Mbavu mbili

  Mbavu mbili JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 803
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 60
  hahahahahahaaha
  T.A.N.Z.A.N.I.AAAAAAA
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Hii hapa ni moja ya msafara wa wanaoenda mkutanoni Jangwani leo. Bila usafirishaji wahudhuriaji Chadema Square pangebaki na ukame usio kifani.
   
 16. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,754
  Trophy Points: 280
  Njaa mbaya hili lijamaa linawadangaya w
   
 17. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,754
  Trophy Points: 280
  Huyo chibuda hana faida yoyote kwa cdm arudi tuu ccm
  chadema haitapungukiwa na lolote
  zaidi itakaa sawa huyu chiibuu daa anaropokaga na kuleta
  mkanganyiko ndani ya chama
   
 18. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  ha ha haaaaa, hata kwalite ya hizo tisheti kwa muonekano tu mmmh!
   
 19. m

  mamajack JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  hahahahah,kweli mwenda wazimu hajitambu,kanga na tshirt zipo leo?
   
 20. a

  andrews JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [h=2][​IMG] ccm kuanzisha al shabab mikoa ya pwani[/h]
  KATIKA HALI YA KUWAGAWA WATANZANIA CCM IMEANZA KUWATUMIA BAKWATA KUWAGAWA WANANCHI.WAZIRI WA ELIMU NI MUISLAM MAKAMU WA RAIS MISLAM KATIBU ITIKADI CCM NI MUISLAM,RAIS WA NCHI MUISLAM MKUU USALAMA WA TAIFA NI MISLAM SASA VP LEOBAKWATA WASEME WANA FELISHWA HIZI NI MBINU CHAFU ZA CCM KUWATOA WANANCHI KWENYE WIMBI LA MAGEUZI YA KISIASA NA KUIINGIZA UDINI KWENYE JAMII NI HATARI NA NI LAANA KWA HAWA WANAMTANDAO HUU TUNASEMA ILI TANZANIA IWE NA AMANI 2015 CCM LAZIMA IONDOKE ISITULETEE MAAFA.WAMEANZA UAMSHO NA HAKUNA KARIPIO KALI LILILOTOLEWA KUONESHA CCM INAVYOHUSIKA VILIVYO KABLA YA UCHAGUZI 2015 WASHINDWE WALEGEE NA WASAMBARATIKE.MUNGU IBARIKI TANZANIA:confused2:​
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...