Shibuda kufukuzwa CHADEMA

zumbemkuu nadhani sasa inatosha hata wale tuliokuwa na uvumilivu kwake sasa tunasema imetosha.
Ni muhimu sana shibuda akarudishwa huko magambani alikotoka, kuliko kumuacha atumie majukwaa ya chadema kukitukana chama chetu.

mwita, busara yashinda papara mkuu, nadhani ni jambo la muda tu. shibuda hiyo mission yake haitafanikiwa. hebu mnakumbuka miaka 2 iliyopita ccm walisema kuwa chadema haitafika 2015, sasa unadhani walikuwa hawana fact?
 
Last edited by a moderator:
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kitaunda kamati maalum ya kushughulikia tuhuma dhidi ya Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda (CHADEMA), ambapo akipatikana na hatia atakabiliwa na adhabu nzito ikiwemo kuvuliwa uanachama.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho na kuthibitishwa na mmoja wa maafisa wake waandamizi, zimesema kuwa kamati hiyo inayotarajiwa kukutana wakati wowote kuanzia sasa inaongozwa na mjumbe wa Kamati Kuu, Prof. Abadallah Safari.
Imedaiwa kuwa kamati hiyo maalumu itamhoji Shibuda kabla ya kutoa mapendekezo yake katika kikao cha baraza kuu ambapo kuna habari kuwa litachukua uamuzi mzito na mgumu dhidi ya mbunge huyo, ingawa imedaiwa kuwa naye atakuwa na haki ya kukata rufaa.
Hii itakuwa mara ya pili kwa kamati hiyo kumjadili Shibuda kutokana na kupingana mara kadhaa na msimamo wa CHADEMA katika masuala ya msingi ya sera na itikadi, likiwemo suala la nidhamu.
Hivi karibuni, akiwa mjini Dodoma, Shibuda alikiuka utaratibu wa chama chake na kukidhalilisha hadharani mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM waliokuwa katika semina, akidai kuwa hajaona chama kinachoweza kuongoza nchi zaidi ya chama tawala.
Akizungumza na Tanzania Daima, mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Baraza Kuu, Samson Mwigamba, alisema kuwa kitendo alichokifanya Shibuda hakikubaliki kwa mujibu wa katiba yao, ingawa anaweza kudai ni haki yake ya Kikatiba.
Mwigamba alisema katiba inamtaka kila mwanachama wao kukipigania, kukitetea na kukieneza chama chao kwa lengo la kushika dola.
Hivyo kitendo cha Shibuda kudai kwamba mpaka sasa hajaona chama kinachoweza kushika dola, ni kukiuka katiba jambo ambalo linaweza kumfukuzisha moja kwa moja uanachama.

Source:Tanzania Daima
CHADEMA bwana yani issue ya shibuda ndio mnaiundia tume ambayo itagharimu fedha za walipa kodi kwa kitu kilicho wazi kabisa,fanyeni tu maamuzi magumu
 
Dawa ya mchumia tumbo kama shibuda ni KUMPOTEZEA as though he doesnt exist.
anachotaka yeye ni kutajwa tajwa magazetini,kwenye vyombo vya habari na kadhalika...so dawa yake ni ku mute tuuuuuuuuuuuuuuu mpaka ajistukie mwenyewe kuwa kumbe si chochote na si lolote...

huyu ni msaliti mkubwa na adui wa mabadiliko..
 
shibuda ana mahaba mabaya sana juu ya ccm. Yani pamoja na umahututi wake bado anataka kurudi huko?
 
Hivi kuna haja ya kumjadili Shibuda kweli.Nadhani ni case ya kufukuza moja kwa moja.Au CCM na CDM ni Waarabu wa Pemba?
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kitaunda kamati maalum ya kushughulikia tuhuma dhidi ya Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda (CHADEMA), ambapo akipatikana na hatia atakabiliwa na adhabu nzito ikiwemo kuvuliwa uanachama.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho na kuthibitishwa na mmoja wa maafisa wake waandamizi, zimesema kuwa kamati hiyo inayotarajiwa kukutana wakati wowote kuanzia sasa inaongozwa na mjumbe wa Kamati Kuu, Prof. Abadallah Safari.
Imedaiwa kuwa kamati hiyo maalumu itamhoji Shibuda kabla ya kutoa mapendekezo yake katika kikao cha baraza kuu ambapo kuna habari kuwa litachukua uamuzi mzito na mgumu dhidi ya mbunge huyo, ingawa imedaiwa kuwa naye atakuwa na haki ya kukata rufaa.
Hii itakuwa mara ya pili kwa kamati hiyo kumjadili Shibuda kutokana na kupingana mara kadhaa na msimamo wa CHADEMA katika masuala ya msingi ya sera na itikadi, likiwemo suala la nidhamu.
Hivi karibuni, akiwa mjini Dodoma, Shibuda alikiuka utaratibu wa chama chake na kukidhalilisha hadharani mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM waliokuwa katika semina, akidai kuwa hajaona chama kinachoweza kuongoza nchi zaidi ya chama tawala.
Akizungumza na Tanzania Daima, mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Baraza Kuu, Samson Mwigamba, alisema kuwa kitendo alichokifanya Shibuda hakikubaliki kwa mujibu wa katiba yao, ingawa anaweza kudai ni haki yake ya Kikatiba.
Mwigamba alisema katiba inamtaka kila mwanachama wao kukipigania, kukitetea na kukieneza chama chao kwa lengo la kushika dola.
Hivyo kitendo cha Shibuda kudai kwamba mpaka sasa hajaona chama kinachoweza kushika dola, ni kukiuka katiba jambo ambalo linaweza kumfukuzisha moja kwa moja uanachama.

Source:Tanzania Daima
 
mfukuzeni tu, but litazameni kwanza kisheria.

Kumvua uanachama haihitaji huko. tunaangalia katiba ya chama inasema nini kuhusu wajinga wajinga kama hao!
Watakao takiwa kuangalia sheria ni bunge baada ya kuvuliwa uanachama na kubaki uchi.
 
Wadau,
Hili andiko la bwana joseph limeenda skuli sana hebu tulipitie bila jazba.

MBUNGE wa Maswa Mashariki na mwanachama asiye wa siku nyingi wa Chadema, John Shibuda, amejikuta katika mtafaruku na ‘wenye chama chao’, kwa linaloitwa kosa la kutangaza kuwania urais wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2015.

Kinachowauma Chadema kupitia Baraza lake la Vijana (Bavicha) chini ya Mwenyekiti John Heche, ni kwanza kujitangaza kwa Shibuda mapema, pili kujinasibu kwamba atamwomba
Rais Jakaya Kikwete awe Meneja wake wa kampeni, lakini tatu mahali alikotangazia.

Bavicha wanalalamika Shibuda kutangaza azma yake hiyo katika semina ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Dodoma, lakini wanaloliona baya zaidi ni aliposema kwamba hakuna chama cha upinzani chenye uwezo wa kuongoza Dola kama CCM.

Hapo ndipo wanapotamka wazi, kuwa kama anaona hakuna chama cha upinzani chenye uwezo wa kuongoza Dola huku kila chama kikiwania kushika Dola, basi na aende katika chama anachoona kina uwezo huo, ambacho kwa mujibu wa Shibuda ni CCM.

Chadema wana haki ya kujibu pigo hilo la Shibuda, hasa pale ilipoona kama inabezwa kuwa si
miongoni mwa vyama vyenye uwezo wa kushika Dola, huku kikijinasibu kuwa ndicho kinachoelewa matatizo ya wananchi na kimbilio lao, lakini pia mpaka kikaonya dhidi ya
wanaotaka kukizuia kushika Dola mwaka 2015.

Pande hizi mbili za mgogoro huu zina haki ya kimsingi, kwamba Shibuda ana haki zote za kutangaza azma yake kama Mtanzania huru lakini mwanachama wa chama kinachojinasibu kujenga demokrasia na maendeleo kwa mujibu wa jina lake.

Lakini Chadema nayo ina haki ya msingi ya kujitetea, ili isidharauliwe wala kutibuliwa mipango yake ya kutwaa madaraka na kumsimamisha mgombea inayemtaka, ingawa hata
alichokifanya Shibuda kinaweza kuirahisishia kupata mgombea wake.

Ila kilichofanywa na Bavicha kumshambulia Shibuda, kinaonesha wazi kuwa demokrasia ndani ya Chadema ni ya hatihati, na huenda kuna wateule wachache ndani ya chama hicho wanaojua nani atagombea muda ukifika – ni kinyume cha Demokrasia.

Tumeshuhudia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ambaye ni mwanachama wa siku nyingi, Kabwe
Zitto, akisakamwa ndani ya Chadema pale alipotangaza kwamba urais anautaka na muda mwafaka ukifika atagombea.

Tulipata kushuhudia alivyosakamwa Zitto alipotaka kugombea uenyekiti wa Chadema dhidi
ya Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe; lakini ilikuwa vivyo hivyo kwa marehemu Chacha Wangwe, alipoonesha nia ya kugombea pia nafasi hiyo huko nyuma.

Chadema inataka kutwambia nini sisi ambao tulidhani kweli inajenga demokrasia sawa na jina lake? Inataka kutueleza kuwa ni ya wateule wachache na ndiyo wenye haki ya kugombea uongozi wa juu wa Taifa hili? Kwa nini iwe nongwa kwa wengine kujitangaza?

Mimi nadhani Shibuda hajakosea kiasi hicho kama ambavyo Bavicha inataka kuufahamisha umma, yeye alionesha nia na kuitangaza, ambalo si kosa katika Katiba ya chama chochote
achilia mbali ya nchi.

Kutangazia mbele ya wajumbe wa NEC ya CCM nalo si tatizo, kwa sababu Shibuda hakwenda pale kama mwanachama wa CCM, bali mjumbe wa Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora Afrika (APRM) ambao ndio ulikuwa umeandaa semina ile kwa wajumbe wa NEC.

Shibuda kumwomba Rais Kikwete awe Meneja wake wa Uchaguzi nayo ni hiari yake kwa sababu kwanza ni mtani wake, lakini pia wakati huo Kikwete atakuwa amemaliza muda wake wa uongozi na kubaki kuwa Rais mstaafu, ambaye yawezekana kabisa hatakuwa na kikwazo.

Badala ya Chadema kumlalamikia Shibuda kwa uamuzi wake huo alioutangaza uwe mzaha, utani au uliodhamiriwa kwa dhati ya moyo wake, ungemtumia kujitangaza na kujenga uhusiano chanya na vyama vingine vya siasa vinavyoamini katika ujenzi wa demokrasia nchini.

Lakini pia kinapaswa kuwapa uhuru wanachama wao kutangaza azma zao mapema na hivyo kupata fursa ya kuona ni nani pumba na nani mchele, badala ya kubana fikra za wanachama katika kutoa hisia zao.

Chadema mlimpokea Shibuda kwa nderemo, vifijo na vigelegele alipohama CCM mkamsaidia mpaka akapata ubunge, iweje anapotaka urais mnaanza kumletea mikingamo na mizengwe na kuamini kuwa si afaaye?

SOSI: HabariLeo | Lipi kosa la Shibuda katika medani hii?

Msaidieni badala ya kumkatisha tamaa.
 
Hakika kwa uchambuzi wa makini kama huu nakupa pongezi sana bwana Joseph,

Post imetulia sana na inakidhi vigezo!
 
Nilivyosoma source tu ya habari nimesikia kutapika na nikapuuza kila kilichoandikwa.
 
Shibuda hana tatizo ila yeye binafsi kama Shibuda ndio tatizo na kibaya zaidi hajijui kama mleta tread alivyo.
.
 
Wadau,

Lakini pia kinapaswa kuwapa uhuru wanachama wao kutangaza azma zao mapema na hivyo kupata fursa ya kuona ni nani pumba na nani mchele, badala ya kubana fikra za wanachama katika kutoa hisia zao.

Msaidieni badala ya kumkatisha tamaa.

Kwenye blue: Huyu Kulangwa na Habari Leo anaweza kuwa na kumbukumbu ndogo sana kwa sababu ameamua iwe hivyo. Kama kweli anaona ni sahihi kwa Shibuda kutangaza nia ya kugombea urais mapema tena kwenye hafla ya NEC- CCM, basi Kulangwa atuambie kwa nini CCM wanang'aka kila mara mmojawapo anaposema fulani ana nia ya kugombea urais? Kwa nini CCM wasiwaambie wanachama wake watu watangaze mapema ili kila mtu ajue moja? Kulangwa angepeleka huo ushauri wa kutangaza mapema kwa CCM.

Pili na muhimu sana. Kulangwa anatakiwa kutofautisha kati ya Demokrasia ndani ya chama na Nidhamu/mila na tamaduni ndani ya chama. Kinachoisumbua CCM ni kutofanya maamuzi kwa wakati hata kwa makosa makubwa na ya kihistoria. Matokeo yake chama kinazama. CHADEMA wameweza kuonesha kuwa mwanachama wake akienda kinyume na maadili, mila ya tamaduni za chama basi maamuzi yatachukuliwa on the spot. Hii tabia ya kuzunguka mbuyu ndiyo sababu tumejikuta tuna watu kama Ekelege. CCM kama kweli wanataka kufufua chama chao wangekaa chini ni kujifunza toka CHADEMA. Lakini cha ajabu watu kama NAPE wanaonekana kupata mbinu toka Shibuda!
 
Hakuna freedom of speech CDM,

Tatizo shibuda kagusa eneo ambalo wapenda madaraka wa CDM nao wanalimezea mate.

Mwacheni shujaa SHIBUDA atoe mawazo yake!
 
Kumvua uanachama haihitaji huko. tunaangalia katiba ya chama inasema nini kuhusu wajinga wajinga kama hao!
Watakao takiwa kuangalia sheria ni bunge baada ya kuvuliwa uanachama na kubaki uchi.

Mungi uwe na nidhamu kwa watu wakubwa waliokuzidi umri! Huna haki ya kumuita shibuda mjinga mjinga!
 
Wanao mlea shibuda ni chadema wasio taka kumfukuza kwa ***** anaofanya! Kasha jionyesha tangu awali kuwa kiroho yuko ccm na kimwili yuko chadema, kwa nini viongozi waendelee kumng'ang'ania wasi muache arudi kwenye roho yake (ccm)?

Wanaoleta kansa ndani ya chadema ni chadema wenyewe na hili ni funzo chama kuacha kuwa kokoro la kubeba kila taka iliyotupwa.
 
Shibuda umevaa viatu that do nt fit ur feet,kindly we request u to get out and go to find ur own green pasture. Mchumia Tumbo MkubWA wewe
 
Pole sana Shibuda kwani umegusa maslahi ya wenzio bila ya kufahamu ama umefanya maksudi!! CDM wana uhakika sana na 2015, lakini msuguano wa Mbowe, Slaa na Kabwe katika kuwania Urais kupitia Chama hicho unaweza ukaleta balaa na umaarufu wote ukaisha, hakuna aliyekamilika tukifikia kwenye suala la madaraka kila mmoja iwe ni ndani ya CCM, CDM ama CUF wote na Baba mmoja Mama mmoja wana uchu wa kuingia Ikulu ambao sijawahi kuuona maishani mwangu. Mungu aingilie kati tu na Kutupatia mwenye hofu ya kumuogopa Yeye kwa dhati.
 
sikubaliani na shibuda ila napinga kufukuzwa//////mpuuzen////wekeni watu wa chini wamshughulikie kisiasa///viongozi wa kitaifa wa cdm wasijibishane naye////jimboni mwaketafuten watu compitent...waandaen//kuchukua jimbo///tambo za shibuda ni mizizi yake jimbon////mkienda naye papara kwa siasa za mihemko.///atawaacha majeruhi,,,,atavuruga chama//mnampa umaarufu////katumwa huyo//mtaona atatangaza hata bungen kugombea urais kupitia chadema/////kuwachanganya watu na kubadili upepo//////:spy:

Wazo kuu....
Najiuliza tu ni kwa kiasi gani ushauri tunaotoa hapa unafika makao makuu
 
Back
Top Bottom