Shibuda Shibuda Shibuda, we shibuda,
Ni nani? Ni mtu wa aina gani? Kwa nini sasa ndiyo aone ni wakati wa kuvuruga CDM?
Kujibu maswali haya, inahitaji kugundua ujanja wa kisiasa, Shibuda ninayemjua mimi ni yule aliyeomba kugombwa urais mwaka fulani huko nyuma, shibuda huyo huyo ni yule aliyepingana na sera za wenzake CCM (MAGAMBA) na akatoq ada ya shs 1,000,000 za fomu?!!!!!!!
Shibuda huyu ni yule, uliyelazimisha kutaka kugombea urais mwaka 2010 hata kama chama chake kilitaka agombee Kikwete bila kupingwa?!!!!,
Shibuda huyu ni yule aliyejibu kwa kejeli alipoambiwa protocal za MAGAMBA hazirusu kugombea na Rais aliye madarakani?
Kilichofuata Huyu jamaa akatoswa kwenye hizo vurugu zake akabaki analalamika.
Akakimbilia kwenye ubunge, kura za maoni zikambwaga kule Maswa.
Kwa hisani za CDM kumuona labda huyu jamaa ni potential CDM wakamumkubalia agombee ubunge kule maswa kweli akashinda ubunge kupitia CDM, Shibuda ni buda kweli, akadhani kuwa ameshinda ubunge kwa sababu ya umaarufu wake, kumbe moto wa CHADEMA kanda ya ziwa ulikuwa juu mno, kwamba yoyote angeweza kushinda hata kama si Shibuda.
Kwa ufupi huyo ndiyo Shibuda, ni msumbufu sana kisiasa, hilo si jambo baya lakini kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa njia hiyo kwa kweli si sahihi kabisa.
Mimi kama Mwana CDM nasema kwamba haikubaliki na ni usaliti wa msafiri aliye ndani ya boat ya kasi anayejaribu kuitoboa boat hiyo ili izame akijidanganya kwamba yeye yupo salama kwa vile anawasiliana na muongoza meli aliye nchi kavu. (Nincompoops) INATIA HASIRA NA KUKERA. Ni bora atoswe yeye haraka ili hayo waliomtuma waone kama huo utakuwa mgogoro ndani ya CHADEMA.
Shibuda ni mtu mdogo sana ndani ya CHADEMA, ningejisikia vibaya kama hata angekuwa mtu mwenye mchango mkubwa kwa nchi ama CDM, lakini huyo ni mchumia tumbo tuu,
Inaelekea alidandia boat asiyoijua inakoelekea, si vibaya kumwambia yuko wrong direction hivyo ashuke atafute uelekeo sahihi kwake.
Shibuda ameingia chama ambacho si saizi yake, ni kama maji na mafuta kamwe hayachanganyiki kabisa hata kama ukiyafukia udongoni yatajitenga.
Shibuda si mwana CDM, ila ni mwanaCCM anayetafutia maisha CDM, sasa naona ameshiba kwa hiyo ameamua kunyea kambi. LAANA ya wanamageuzi itamtafuna yeye na vizazi vyake leo, kesho, na hata milele.
Shibuda anatumiwa na CCM, angalia ameanza uppuzi huu baada ya kikao chao cha NEC.NEC ya CCM imeweka strategy zao za mwisho baada ya kuiona hatari inayowakabili, hivyo, wanadhani makuwadi wao waliomio ndani ya CDM watawasaidia.
Wimbi la wanaCCM kuhama is a real threat to CCM, kwa kuwa wananchi wanaikubali sana CDM.
CDM kwa taarifa yako Shibuda si chama laini kinachoweza kudhoofishwa na wewe, ni chama kinachoweka misingi bora sana ya upinzani wa sera na ubora wa utawala.
CDM inao uongozi bora, wananchi tunaelewa hivyo, CDM ina strategy makini na nzuri sana ambazo haziharibiwi hata kidogo na uppuzi wa SHibuda ama kuwadi mwingine yoyote. CDM inao wanachama wanaoelewa kwa nini wao ni wanaCDM ni si kwa kufuata mkumbo ama kulazimishwa kama ilivyo kwa CCM.
Viongozi wangu wa CDM muinangalie kwa mtazamo huo, kwamba hiyo ni dhana ambayo CCM wameipima na kuona labda itapunguza kasi ya uhamaji wa wanachama wao.
Iaminike wazi kwamba wimbi hili la mageuzi ni kama kimbunga ambacho kinakumba miti, viti, mbao, nyumba nakadhalika hakizuwi na shuka la kitandani.
Kwa heri Shibuda kwenye ulingo wa siasa, huwezi kukubalika CDM na hakika hata CCM hutakubalika unatumika kama punda ili mzigo ufike. CHADEMA tulikupenda lakini CCM wamekupenda zaidi, kalale pema JAHANAMU.