Jana nilivunjika sana moyo. Heri utukanwe na mtoto wa jirani, kuliko wako wa kumzaa. Inauma sana na ndio maana CCM walishangilia sana! Zilikuwa ni dakika kumi za mashambulizi kwa wanaCHADEMA na uongozi mzima! Nadhani hii inahusiana na bifu na Wenje,maana naona chama kilimpuuza na malalamiko yake ya kijinga.
Chadema kimeshakuwa chama kikubwa sasa, inabidi wawe na uwezo wa kuthubutu kuwachukulia hatua wanaovunja sheria na taratibu za Chama. Ilibidi waanze na Zitto! Hofu yangu ni kwamba itajengeka hisia kwa wanachama kwamba ukiwa mkubwa kwenye chama, hata ukikosea hakuna atakayekuchukulia hatua. Hii impunity ndio inayoiua CCM!
Shibuda anatufundisha umuhimu wa kuwa na katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi! Shibuda anajipendekeza kwa rais na CCM kwakuwa anajua watamlinda wakati wa uchaguzi! Watu kama wakina Cheyo na Mrema wasingekuwa ndumilakuwili kama tungekuwa na tume huru ya uchaguzi! CCM wanapenda kuwa na proxyies upinzani kwakuwa wanajua kuwa upinzani wanaweza kuuana wenyewe kisiasa kwa urahisi sana. It worked with NCCR, why not try it now?
Chadema wachukue hatua,shibuda hastahili kuwa na kadi ya chadema. Ameongea mengi hadharani, sirini anaongea mangapi? Chadema inawezaje kumshirikisha shibuda ktk mikakati yao ya maendeleo ya chama?Chadema ina sapoti kubwa sana ya vjana, hyo ndio hazina yao! Sio wazee kama shibuda ambao wanahesabu siku zao kisiasa. Bank on the youths!