Shibuda ashangiliwa na wabunge wa CCM

elimukwanza

Senior Member
Dec 27, 2010
168
23
Mbunge shibuda akiendeleza kile kinachoitwa Vijembe,mipasho ya bunge la sasa huku akitumia misamiati ya kiswahili cha pwani kumponda kiongozi wa CHADEMA na wanachadema alishangiliwa sana na wabunge wa CCM hadi mwisho bunge kugeuka ushabiki na kuimba CCM CCM CCM.Na alifika mbali zaidi na eti kuwaomba pole wananchi wa zanzibar eti kwa waliyoyapata ya kutengwa kutokana na maamuzi waliyofanya,akuwa wazi zaidi ila alimaanisha CDM kutoishirikisha CUF kutokana na kuunda serikali.
Ilinisikitisha sana huu unafiki na uzandiki mbona kama wanampenda walimchinjia baharini kwenye NEC,Shibuda amesahau au katumwa? maana sikuona kachangia hoja yeyote kuhusu Hotuba ya Rais zaidi ya kumponda(majungu) kiongozi wa CDM.leo pale bungeni kama unataka usifiwe wewe iponde CDM unawezwa ukabebwa
CDM msikate tamaa ila kuweni waangalifu kupokea makada mitumba toka CCM ni bora mkawekeza nguvu zenu kwa vijana wapya ambao hawaijui CCM achaneni na Mitumba ya CCM mlenge wagombea vijana na muutangaze mwaka 2015 kuwa wa vijana 70% ya wagombea wenu wawe vijana wasomi

Nawasilisha
 
Elimu kwanza umeongea neno......mabadiliko huletwa na vijana ona misri sasa....najisikia kumtusi shibuda ok...the One fogive me for what I AM:thinking: on shibuda's speech.
 
Ni utabiri kupata kwa uhakika alikusudia kusema nini, na mimi kwa upeo wangu nilitegemea spika wa bunge angemuuliza katika mipasho ile alikusudia kusema nini. Kwa kuwa bungeni sio mahali pa kuimbia taarabu wala kufumba mambo, binafsi sikuelewa chochote alichokusudia kusema.
 
Nilifikiri ni mimi pekee yangu ambaye sikumuelewa huyu baba maana hakuna chochote alichangia kuhusu hotuba ya raisi.
 
Kokoro la Samaki hukusanya hata samaki waliooza!! Ni wakati wa kuchambua kati ya samaki wafaao au watupwao!! Kuwa tayari kwa mabadiliko zaidi. 2015 is around the corner!! HAkuna kurara !!!
 
Shibuda bado anaugomvi na Weje. Alikusudia kutumia Usukuma wake lakini ikagonga mwamba hivyo ameamua kuendeleza vita Bungeni. Amesahau yaliyomkuta NEC. Shibuda kumbuka ulikotoka, ulipo na ona unakokwenda!!!
 
Jana nilivunjika sana moyo. Heri utukanwe na mtoto wa jirani, kuliko wako wa kumzaa. Inauma sana na ndio maana CCM walishangilia sana! Zilikuwa ni dakika kumi za mashambulizi kwa wanaCHADEMA na uongozi mzima! Nadhani hii inahusiana na bifu na Wenje,maana naona chama kilimpuuza na malalamiko yake ya kijinga.

Chadema kimeshakuwa chama kikubwa sasa, inabidi wawe na uwezo wa kuthubutu kuwachukulia hatua wanaovunja sheria na taratibu za Chama. Ilibidi waanze na Zitto! Hofu yangu ni kwamba itajengeka hisia kwa wanachama kwamba ukiwa mkubwa kwenye chama, hata ukikosea hakuna atakayekuchukulia hatua. Hii impunity ndio inayoiua CCM!

Shibuda anatufundisha umuhimu wa kuwa na katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi! Shibuda anajipendekeza kwa rais na CCM kwakuwa anajua watamlinda wakati wa uchaguzi! Watu kama wakina Cheyo na Mrema wasingekuwa ndumilakuwili kama tungekuwa na tume huru ya uchaguzi! CCM wanapenda kuwa na proxyies upinzani kwakuwa wanajua kuwa upinzani wanaweza kuuana wenyewe kisiasa kwa urahisi sana. It worked with NCCR, why not try it now?

Chadema wachukue hatua,shibuda hastahili kuwa na kadi ya chadema. Ameongea mengi hadharani, sirini anaongea mangapi? Chadema inawezaje kumshirikisha shibuda ktk mikakati yao ya maendeleo ya chama?Chadema ina sapoti kubwa sana ya vjana, hyo ndio hazina yao! Sio wazee kama shibuda ambao wanahesabu siku zao kisiasa. Bank on the youths!
 
Huyu ni pandikizi la CCM kule CHADEMA, CHADEMA kama hawakuwa makini anaweza kabisa kukivuruga chama halafu akatangaza kurudi kwenye chama cha mafisadi.
 
Jana nilivunjika sana moyo. Heri utukanwe na mtoto wa jirani, kuliko wako wa kumzaa. Inauma sana na ndio maana CCM walishangilia sana! Zilikuwa ni dakika kumi za mashambulizi kwa wanaCHADEMA na uongozi mzima! Nadhani hii inahusiana na bifu na Wenje,maana naona chama kilimpuuza na malalamiko yake ya kijinga.

Chadema kimeshakuwa chama kikubwa sasa, inabidi wawe na uwezo wa kuthubutu kuwachukulia hatua wanaovunja sheria na taratibu za Chama. Ilibidi waanze na Zitto! Hofu yangu ni kwamba itajengeka hisia kwa wanachama kwamba ukiwa mkubwa kwenye chama, hata ukikosea hakuna atakayekuchukulia hatua. Hii impunity ndio inayoiua CCM!

Shibuda anatufundisha umuhimu wa kuwa na katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi! Shibuda anajipendekeza kwa rais na CCM kwakuwa anajua watamlinda wakati wa uchaguzi! Watu kama wakina Cheyo na Mrema wasingekuwa ndumilakuwili kama tungekuwa na tume huru ya uchaguzi! CCM wanapenda kuwa na proxyies upinzani kwakuwa wanajua kuwa upinzani wanaweza kuuana wenyewe kisiasa kwa urahisi sana. It worked with NCCR, why not try it now?

Chadema wachukue hatua,shibuda hastahili kuwa na kadi ya chadema. Ameongea mengi hadharani, sirini anaongea mangapi? Chadema inawezaje kumshirikisha shibuda ktk mikakati yao ya maendeleo ya chama?Chadema ina sapoti kubwa sana ya vjana, hyo ndio hazina yao! Sio wazee kama shibuda ambao wanahesabu siku zao kisiasa. Bank on the youths![/QUOTE]

Huyu anastahili kabisa kufukuzwa kwenye chama kabla ya kusababisha athari zaidi na akifukuzwa anapoteza na ubunge.

Kweli ni bunge la mipasho, nilitegemea vitu vya maana sasa naona upupu mtupu, mfano mbunge anatumia dakika tano kuwashukuru hadi kuku....pumbavu kabisa, tumekupeleka bungeni ukatushukuru kwa maneno au vitendo??? Naenda Tahrir Square
 
jana hata mm nlumia sn na taarab alyo2imbia hyu mzee acye na hta chembe ya busara. Yan ckmwelewa mwnzo mwsho. Cdm vjana 2ko nyma yenu. Msvunjwe moyo na mpuuz km shibuda. Hana jipya keshazoea majungu. Kama vp fukuywha mbali.
 
Nadhani alikuwa amepata mbili ,tatu maana ndio zake akinywa huyoo.Jamani pombe ni mbaya?????
 
Nilishasema tena na tena - SHIBUDA HAFAI HATA KWA BURE. Swali langu kwa uongozi wa CDM ni
mtaendeshaje chama mkiwa na mtu kama huyu?
 
Mbunge shibuda akiendeleza kile kinachoitwa Vijembe,mipasho ya bunge la sasa huku akitumia misamiati ya kiswahili cha pwani kumponda kiongozi wa CHADEMA na wanachadema alishangiliwa sana na wabunge wa CCM hadi mwisho bunge kugeuka ushabiki na kuimba CCM CCM CCM.Na alifika mbali zaidi na eti kuwaomba pole wananchi wa zanzibar eti kwa waliyoyapata ya kutengwa kutokana na maamuzi waliyofanya,akuwa wazi zaidi ila alimaanisha CDM kutoishirikisha CUF kutokana na kuunda serikali.
Ilinisikitisha sana huu unafiki na uzandiki mbona kama wanampenda walimchinjia baharini kwenye NEC,Shibuda amesahau au katumwa? maana sikuona kachangia hoja yeyote kuhusu Hotuba ya Rais zaidi ya kumponda(majungu) kiongozi wa CDM.leo pale bungeni kama unataka usifiwe wewe iponde CDM unawezwa ukabebwa
CDM msikate tamaa ila kuweni waangalifu kupokea makada mitumba toka CCM ni bora mkawekeza nguvu zenu kwa vijana wapya ambao hawaijui CCM achaneni na Mitumba ya CCM mlenge wagombea vijana na muutangaze mwaka 2015 kuwa wa vijana 70% ya wagombea wenu wawe vijana wasomi

Nawasilisha

Hata leohapa JF kama unataka usifiwe wewe iponde CCM na JK unawezwa ukabebwa!!! sioni kwanini Shibuda mumshambulie mbona Mbowe mwenye kamwaga misifa mingi sana kwa Rais? Au kwakuwa Shibuda ni mtoto wa kambo? Nadhani aliyoyasema yote ni ya ukweli hasa ya Zanzibar mie binafsi nampongeza sana kwa ujasiri wake aendelee kuwa mwana demokrasia kwani yupo kwenye chama cha Demokrasia na Maendeleo aitumie vema Demokrasia yake.

YouTube - Mh. Freeman Mbowe ajadili hotuba ya Rais (Michuzi Blog)
 
Huyu anastahili kabisa kufukuzwa kwenye chama kabla ya kusababisha athari zaidi na akifukuzwa anapoteza na ubunge.

CUF walimfukuza Naila Jidawi uanachama Msekwa akasema ni mbunge halali nadhani hata Chiku Abwao aliwahi kufukuzwa NCCR kama sikosei lakini akaendelea kula kuku pale Dodoma. Mzee mipango hii huwa inasukwa ikasukika.
 
Akifukuzwa chamani si mbunge tena, soma hapo chini.

"Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Na Salim Said

OFISI ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi, inamtambua aliyekuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fred Mpendazoe kuwa bado ni mbunge wa jimbo la Kishapu kupitia Chama hicho hadi hapo itakapopata taarifa rasmi kutoka CCM.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ge-mpendazoe-bado-ni-mbunge-wa-kishapu-3.html
 
Aahh, osie uzakosea, sio vyedi...usiwatukane, waache wajitukane wenyewe, maana kwa mtu mwenye akili timamu huwezi kutukana au kuropoka siri za nyumbani mwako na mkeo/mumeo anaekupa kula...Shibuda hana maadili yupo kimaslahi ziaidi

haya mghoshi, hongea kwa ushauri, seniughiize vituhu, hasira zimekua nyingi mpaka akili zinaniruka sometimes hasa nikifikiria hizi siasa za bongo.
 
Even me I was baffled by what he was saying, he need to be taken care off, we youth can move this country up we dont need another hypocrite. He should explain what he meant, its either you are with us or against us there is no middle ground. He want to use us! If he is not agreeing with our party leaders we have procedures to make your concern if we are doing wrong, not making us naked in front of our enemies. We need him to punished
 
Demkrasia hiyo..mbona huko ccm wwabunge wanaikosoa serikali yao na bila tatizo

Chadema wakubali demokrasia waache ubabe wa kijinga

Shibuda was right
 
Back
Top Bottom