Malafyale
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 13,813
- 11,127
Mbunge wa Maswa, John Shibuda (CCM), amebadili msimamo wake na safari hii ameibuka na kumpigia debe Rais Jakaya Kikwete.
Akizungumza wakati wa ziara ya Rais Kikwete mkoani Shinyanga juzi, Mbunge huyo machachari alisema Tanzania ina bahati kwa kuwa na kiongozi kama Rais Kikwete, ambaye ametekeleza ahadi zake nyingi kwa wana-Shinyanga na Watanzania kwa jumla.
Aidha, Shibuda alimtakia mema Rais Kikwete akisema kuwa Mungu atamjalia kwa sababu ya tabia yake ya kujali wananchi kwa kutimiza ahadi ambazo alizotoa mwaka 2005 wakati akijinadi kwa wananchi kuomba kura.
Huyu ni rafiki yangu, mtani wangu na swahiba wangu ambaye hatukukutana kwenye Mkutano Mkuu wa CCM. Ninamjua amefanya mengi na namwombea kwa Mwenyezi Mungu amjalie mafanikio zaidi. Aliyepewa na Mwenyezi Mungu, hapokonyeki, alisema Shibuda juzi wakati akizungumza, kwenye sherehe za Uzinduzi wa Programu ya Kilimo Kwanza kwenye Kiwanda cha pamba cha Aldawi kilichoko Lalago, wilayani Maswa.
Shibuda aliwaeleza mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe hizo kuwa baadhi ya ahadi ambazo zilitolewa na Rais Kikwete ama moja kwa moja ama kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) tayari zimetekelezwa.
Tuna bahati ya kuwa na kiongozi kama wewe. Uliahidi kutengeneza barabara na umefanya hivyo. Wakati tulipokabiliwa na njaa, Serikali yako ilitupa msaada wa chakula. Wakati bei ya pamba yetu iliingia matatizo, uliingilia kati na kuhakikisha kuwa wakulima wetu wanaendelea kulipwa kulingana na jasho lao. Sasa unatoa mbegu za ruzuku za pamba na madawa ya ruzuku ya pamba, alisema Shibuda na kuongeza:
Tunakupongeza kwa kuimarisha demokrasia na utawala bora nchini. Unahangaika dunia nzima kutafuta jinsi gani nchi yetu inavyoweza kusaidiwa. Wewe siyo mtu wa kukaa ofisini kupokea majungu ya watu. Unahangaika kwa ajili ya nchi yetu, kwa ajili ya watu wako. Julai, mwaka jana, naye Mama Salma alikuja hapa kuunga mkono juhudi zetu za maendeleo akatoa vitanda na shuka kwenye hospitali yetu na fedha za kusaidia vikundi vya Saccos.
Shibuda alisema Mama Salma wakati wa ziara hiyo ya siku tatu mkoani Shinyanga alizindua programu hiyo.
Kauli ya Shibuda ya kusifu utendaji wa Rais Kikwete inaonyesha kuwa huenda akasitisha msimamo wake wa siku nyingi kuwa atajitokeza kuchukua fomu za kugombea urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu kupitia CCM.
Shibuda alichukua fomu za uteuzi wa mgombea urais kupitia chama tawala katika uchaguzi wa mwaka 2005, lakini jina lake lilichujwa na kikao cha kwanza cha Kamati Kuu (CC).
Hivi karibuni, Shibuda alisema kuwa atachukua fomu tena wakati ukifika kuchuana na Rais Kikwete, ingawa kwa mujibu wa utaratibu wa CCM, Rais Kikwete ndiye anayepaswa kuwa mgombea wa kiti hicho hadi hapo atakapomalizia muhula wake wa pili Oktoba, 2015.
Nipashe ilipowasiliana na Shibuda jana jioni ili atoe ufafanuzi kama atasitisha nia yake ya kugombea urais, alisema kwa kifupi bila kufafanua kuwa Tanzania hakuna siasa za kuchafuana.
Alisisitiza kwamba kama mtu amefanya vizuri ni vema kumsifu na si kuendesha visa na chuki. Mimi si muumini wa siasa za chuki simvai mtu wala singoi mtu kwa sababu si muhogo, alisema na kueleza kuwa hawezi kukaa kimya kama yapo mazuri ya kumsifu Rais Kikwete.
CHANZO: NIPASHE