Shibuda Ampigia Debe JK Ashinde Urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda Ampigia Debe JK Ashinde Urais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malafyale, Jan 22, 2010.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Mbunge wa Maswa, John Shibuda (CCM), amebadili msimamo wake na safari hii ameibuka na kumpigia debe Rais Jakaya Kikwete.

  Akizungumza wakati wa ziara ya Rais Kikwete mkoani Shinyanga juzi, Mbunge huyo machachari alisema Tanzania ina bahati kwa kuwa na kiongozi kama Rais Kikwete, ambaye ametekeleza ahadi zake nyingi kwa wana-Shinyanga na Watanzania kwa jumla.

  Aidha, Shibuda alimtakia mema Rais Kikwete akisema kuwa Mungu atamjalia kwa sababu ya tabia yake ya kujali wananchi kwa kutimiza ahadi ambazo alizotoa mwaka 2005 wakati akijinadi kwa wananchi kuomba kura.

  “Huyu ni rafiki yangu, mtani wangu na swahiba wangu ambaye hatukukutana kwenye Mkutano Mkuu wa CCM. Ninamjua amefanya mengi na namwombea kwa Mwenyezi Mungu amjalie mafanikio zaidi. Aliyepewa na Mwenyezi Mungu, hapokonyeki,” alisema Shibuda juzi wakati akizungumza, kwenye sherehe za Uzinduzi wa Programu ya Kilimo Kwanza kwenye Kiwanda cha pamba cha Aldawi kilichoko Lalago, wilayani Maswa.

  Shibuda aliwaeleza mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe hizo kuwa baadhi ya ahadi ambazo zilitolewa na Rais Kikwete ama moja kwa moja ama kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) tayari zimetekelezwa.
  “Tuna bahati ya kuwa na kiongozi kama wewe. Uliahidi kutengeneza barabara na umefanya hivyo. Wakati tulipokabiliwa na njaa, Serikali yako ilitupa msaada wa chakula. Wakati bei ya pamba yetu iliingia matatizo, uliingilia kati na kuhakikisha kuwa wakulima wetu wanaendelea kulipwa kulingana na jasho lao. Sasa unatoa mbegu za ruzuku za pamba na madawa ya ruzuku ya pamba,” alisema Shibuda na kuongeza:

  “Tunakupongeza kwa kuimarisha demokrasia na utawala bora nchini. Unahangaika dunia nzima kutafuta jinsi gani nchi yetu inavyoweza kusaidiwa. Wewe siyo mtu wa kukaa ofisini kupokea majungu ya watu. Unahangaika kwa ajili ya nchi yetu, kwa ajili ya watu wako. Julai, mwaka jana, naye Mama Salma alikuja hapa kuunga mkono juhudi zetu za maendeleo akatoa vitanda na shuka kwenye hospitali yetu na fedha za kusaidia vikundi vya Saccos.”

  Shibuda alisema Mama Salma wakati wa ziara hiyo ya siku tatu mkoani Shinyanga alizindua programu hiyo.

  Kauli ya Shibuda ya kusifu utendaji wa Rais Kikwete inaonyesha kuwa huenda akasitisha msimamo wake wa siku nyingi kuwa atajitokeza kuchukua fomu za kugombea urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu kupitia CCM.

  Shibuda alichukua fomu za uteuzi wa mgombea urais kupitia chama tawala katika uchaguzi wa mwaka 2005, lakini jina lake lilichujwa na kikao cha kwanza cha Kamati Kuu (CC).

  Hivi karibuni, Shibuda alisema kuwa atachukua fomu tena wakati ukifika kuchuana na Rais Kikwete, ingawa kwa mujibu wa utaratibu wa CCM, Rais Kikwete ndiye anayepaswa kuwa mgombea wa kiti hicho hadi hapo atakapomalizia muhula wake wa pili Oktoba, 2015.

  Nipashe ilipowasiliana na Shibuda jana jioni ili atoe ufafanuzi kama atasitisha nia yake ya kugombea urais, alisema kwa kifupi bila kufafanua kuwa Tanzania hakuna siasa za kuchafuana.

  Alisisitiza kwamba kama mtu amefanya vizuri ni vema kumsifu na si kuendesha visa na chuki. “ Mimi si muumini wa siasa za chuki… simvai mtu wala sing’oi mtu kwa sababu si muhogo,” alisema na kueleza kuwa hawezi kukaa kimya kama yapo mazuri ya kumsifu Rais Kikwete.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Haki ya mamaa maradhi yote ugua lkn umaskini usiombee;pampja na kuonekaa na nia thabiti ya kumpinga JK kwenye sanduku la kura baadae mwaka huu Mbunge wa Maswe John Shibuda"katepeta"tayari maana anajua akifanya hivyo Kamati Kuu itamshughulikia na atakosa tena mshahara wa Ubunge unaomfanya aishi!

  Njaa ni mbaya sana jamani!
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  I dont think amebadili mawazo haya ni yale yale matatizo yetu ya siku zote na ya waandishi wa habari, Shibuda kasema "Huyu ni rafiki yangu, mtani wangu na swahiba wangu ambaye hatukukutana kwenye Mkutano Mkuu wa CCM"

  Kusema huyu ni rafiki yangu si kubadili msimamo hata kama wana mitizamo tofauti sikutegea aseme huyu ni adui yangu, tatizo liko kwetu zaidi kuelewa nini hasa lengo la mleta habari.

  “ Mimi si muumini wa siasa za chuki… simvai mtu wala sing’oi mtu kwa sababu si muhogo,” alisema na kueleza kuwa hawezi kukaa kimya kama yapo mazuri ya kumsifu Rais Kikwete.

  Kwangu mimi maneno kama haya hayaoneshi kuwa amebadili mawazo labda wenzagu.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Shibuda sijakuelewa kabisaaaaa
   
 5. O

  Omumura JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakuu, mlitegemea kipya chochote kutoka kwa Shibuda?hana lolote na bado ataendelea kumpigia debe siku zote muungwana, ama kweli, ukistaajabu ya mrema na Sheikh Yahya utayaona ya Shibuda!!!Habari ndo hiyo, period!
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Watoto wa mjini huwa wanasema ndio imetoka hiyo! Kaput!

  Respect.


  FMEs!
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,818
  Trophy Points: 280
  Mtandao ni kitu kingine kabisa hawa watu hawashikiki. Huyu juzi tu alikuwa anatwambia anaanza mkakati wa kumrushia madongo Kikwete, leo kabadilisha mawazo naye ameshakuwa mshangiliaji wa Kikwete. Yale madongo yote aliyotaka kuyarusha sijui kimetokea nini mpaka kimembadilisha mawazo yake! Usifanye mchezo kushikishwa bulungutu ambalo hujawahi kuliona tangu uzaliwe unaweza kabisa kuweweseka na hata kupata uchizi wa aina fulani. Huyu jamaa kaweweseka na sasa Kikwete kishasafishiwa njia ya 2010 nyeupeeee! Cheyo anampigia debe Kikwete, Mrema anampigia debe Kikwete, CHADEMA hawaelewani wanaadhiriana na kufukuzana kila kukicha.

  Kwa hiyo Rais wa Tanzania 2010 kishajulikana na hana mpinzani, sasa kizungumkuti bado kiko Zenj labda Karume naye atapigiwa magoti ili asikubaliane na wazo la CUF na CCM Zenj ili aingie tena kwenye awamu ya tatu ili kuunda Serikali ya mseto. Nakupenda sana Tanzania!
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Jan 23, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  I dont get it, sijaona katika maneno yake aliposema hatagombea, kwani si unaweza kumsifu mtu na bado mkachuana!!!

  Kama Shibuda ataamua kubadilika basi ataamua kivyake , lakini haya maneno siyo universal ushahidi wa madai haya! jamani hatuna diplomasia??
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Jan 23, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  well, well well well, Let me see.

  Je shibuda ana cheo serikalini kama vile uwaziri au ukuu wa mkoa? kama hana, then I don't know why. Kama anacho, then I don't know why; the future is here.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  That is why I dont rally behind any politician in Tanzania. They keep changing their thoughts more than chameleon changes its color
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,818
  Trophy Points: 280
  Huyu Shibuda alikuwa analia njaa tu kapiga kelele mpaka kundi la mtandao likamsikia na kuamua kutibu njaa yake sasa anapiga makofi na vigelegele.
   
 12. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tatizo tumezoea sana siasa za uadui,mkipingana na mtu kisiasa ni marufuku kuzungumza mazuri yake, This is damn wrong.
   
 13. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  Shibuda amejisemea ukweli mtupu. Uswahiba huendana na tabia kushabihiana. Bila shaka walikutana kwenye miziki na starehe zingine enzi zile.
   
 14. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Msimshangae Shibuda, labda tishio la Sheikh Yahaya limemwingia kaona kuliko kuondoka duniani nijitoe kwenye haya mambo!
   
 15. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mmmh kweli siasa ni mchezo mchafu, huyu bwana keshaogopa mkwara wa Sheikh Yahya na akachanganywa zaidi na juhudi za kina Mrema na Cheyo kumpigia debe JK..,time will tell...
   
 16. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  anajihakikishia CHAKULA 2010........!ninyi mtaendelea na blah blah weeeeee!mwenzenu yupo ki-maslahi zaidi
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Yaani nyinyi mlipanda chelewa mkadhani itachipua minazi ???
   
 18. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,749
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  sidhani kama ni mbaya mgeni ajapo nyumbani ukamkirimia na kumpamba hata kama unaelewa udhaifu wake,ni wageni wangapi ambao wamekluja nchini na kutumwagia sifa lukuki lakini baada ya hapo wanatugeuka? Juzi amekuja Drogba akaulizwa unakiona vp kiwango cha Tanzania katupamba kuliko jinsi tunavyojielewa.Shibuda ni mtu mzima na Shinyanga ni nyumbani.KARIBU MGENI NA MWENYEJI ASIFU!!!!!!!!!!!!!
   
 19. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ....kaogopa kufa huyo......!
   
 20. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Shibuda akijitoa na kumfagilia JK basi (let me borrow a word from Makamba) MWEHU!
   
Loading...