Shibuda ajichimbia kaburi lake

Kitu ambacho CHADEMA hawawezi kuthubutu ni kumuondoa Shibuda, wanajuwa wakifanya hivyo ndio kifo chao, kama wanabisha wamuondoe halafu waone nini kitafata.

CHADEMA ilikuwepo, Shibuda kaikuta na ataiacha ikipepea juu kwa juu. Kufukuzwa kwa Shibuda ndiyo itaiongezea credibility CHADEMA.
 
Ukiwa na ndugu chizi lazima ukubali matokeo akinya zoa nenda katupe akivua nguo mvalishe. Halafu sukari hata ikiwa tani elf 90 aiwezi kukoza kwenye maji ya bahari. Shibuda ni kama anapiga mluzi huku ana karanga mdomoni haeleweki anaimba nyimbo gani huyu ana bahati mbaya hiki anachokifanya tayari kimefanywa na wengi tumemstukia.

Mi nawataka viongoz wa CHADEMA wamuone kama mtoto chizi ndani ya nyumba kama tulifanya makosa kumpokea basi lakin tujifunze kutokana na makosa... 2015 apigwe chni aende milembe huyu ni kichaa wa siasa hatufai.
 
Kitu ambacho CHADEMA hawawezi kuthubutu ni kumuondoa Shibuda, wanajuwa wakifanya hivyo ndio kifo chao, kama wanabisha wamuondoe halafu waone nini kitafata.
<br />
<br />
mliwachuuza masikini madiwani wa A town wametimuliwa imekuwa sio isue tena, mmehamia maaswaaaaa, mkichukiwa si bure mnachukiza!!!
 

Mkuu nimekusoma. Labda tuelewane kwa jambo moja; nakumbuka Wangwe alisimamishwa umakamo mwenyekiti kwa sababu ya kuhoji juu ya Ruzuku na si posho. Niliposema alijichimbia kaburi sikuwa na maana ya kuuawa kama ulivyodhani. Kama ningekuwa na maana hiyo basi ina maana kujichimbia kaburi kwa Shibuda ni kuuawa? Angalia kichwa cha habari kinavyosema na mimi nimeenda kwa kufuata kichwa cha habari na sijasema kuuawa!!
 
Hili pia nu funzo kwa CDM, hakipaswi kuokoa kila mtu aliyezama kwenye maji na kumfanya kuwa mmoja wa manahoza wa meli ya ushindi! Ndiyo maana JK alimtosa, maana alibishana naye na kusema hafai kuwa rais na akachukua fomu kupingana naye ilhali wenzake walimuona mwenye upungufu wa maadili, CDM wakamuokota.
 
huyu mbaba ni kigeu geu kweli.....cjui anawazaga kwa kutumia nini???nahisi bado damu ya kijani inamtafuna
 
Chadema andaeni mgombea Jimbo la Shibuda na katika mikutano na maandamano yanayofuata muanze kumtambulisha ili huyo mjinga ajue hana chake.Kisha mpigeni chini halafu tuone kama CCM watamrudisha sana sana atakwenda kwa wake wenza CUF au Kwa mufilisi mwenzake Mrema wa ti elo Piii(TLP)
 

Unajua labda kaona kuwa huku CHADEMA hawana mda wa kuiba sasa kaona anakosa madili ili arudi kule kwenye madili..
 


kauli yako ilikuwa tata,
anyway tugonge kote kote usikonde
 
Kwa kweli hata mimi simwelewi kasimama wapi? maana hoja zake hazieleweki. Hajui kwamba yuko bungeni kwa mgongo wa CHADEMA? na tz hatuna mgombea binafsi, sijui akitimuliwa na huku ataenda wapi, hasomi nyakati.
 
Wanabodi..
John Shibuda ni miongoni wa wabunge wa Chadema ambao anatengwa na wenzake.

Inasikitisha sana kuona Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu, Slaa, kumtenga kwa kutomshirikisha katika shughuli zozote za chama zikiwemo za kampeni.

Miongoni mwa shughuli kadhaa za kisiasa viongozi wakuu wamefanya bila kumshirikisha tangu awe mbunge ni pamoja kutomshirisha katika kampeni Igunga.

Walimtenga kwenye msafara waliokwenda kumuona Rais Kikwete Ikulu, na kutomshirikisha katika msiba wa mbunge mwenzake Regia Mtema.

Mwaka 2010 Shibuda alichangia kwa kiasi kikubwa Chadema kuzoa karibu majimbo 10 kanda ziwa, kusema ukweli huyu hapaswi kuwa mwanasiasa wa kupuuzwa kiasi hiki.

Chadema wana majimbo Maswa Mashariki na Magharibi, wana Bukombe, Meatu, Ilemela, Nyamagana, na Ukwerewe hata jimbo la Musoma mjini linatokana na nguvu yake na ushawishi mkubwa aliyekuwa nao kanda ya ziwa.

Mkoa wa Shinyanga ambao Shibunda anatoka una wabunge wanne wa Chadema, ambao kimsingi walipatikana kutokana ushawishi wake.
 
anashiriki shughuli za chama chenu, CDM ni njia tu iliyompatia ubunge,
 
shibuda bwana umakini ndo unamponza !!!
(tatizo wanaharakati wamevamia siasa)
 
Shibuda akipewa nafasi ya kuongea ni hatari mno. Anapanga maneno kwa kutumia kiswahili cha pwani ambacho kimenyoooka vyema na ana uwezo wa kushawishi. Nadhani ni mbunge pekee kwa CDM aliyetumia muda mfupi sana kupiga kampeni na kushinda.

Tatizo lake kwa CDM ni kwamba ni mkweli. Wakati wenzake wantaka jamii iamini kuwa hawataki posho za vikao huku mioyo yao ikipambwa na maua wakati wa kuchukua posho, yeye akasema hadharani kwamba anazitaka na anataka ziongezwe. Basi kwa kusema ukweli wake wa moyoni Mzee wa Ujira akaonekana adui.
 
anashiriki shughuli za chama chenu, CDM ni njia tu iliyompatia ubunge,

Kosa kubwa la Shibuda ndani ya Chadema ni msimamo wake kukataa kumsusia Rais Kikwete wakati alilizindua bunge la sasa mjini Dodoma. Na sakata la posho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…