Shibuda: Achaneni na ‘Agano la Kale’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda: Achaneni na ‘Agano la Kale’

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crashwise, May 17, 2011.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mbunge wa Maswa Magharibi(CHADEMA) John Shibuda amesema mtindo wanaotumia CCM kujivua gamba, ni sawa na mtu kujimwangia poda kuondoa harufu ya jasho aliyonayo.
  Pia, Shibuda aliwataka watanzania kutafakari kwa makini, mwenendo wa CCM kwa sababu ni gari bovu, kama hawana mizingo ndani yake ni bora kuachana nalo na kupanda jipya ambalo ni CHADEMA.
  Akihutubia mkutano wa hadhara jimbo la Busega juzi shibuda alisema haiwezekani watangaze kujivua gamba wakati watanzania wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha na kwamba, huo ni usanii ambao kiongozi mwenye mamlaka ya kuletea nchi yake maendeleo, hapaswi kufanya.
  Shibuda alisema CCM haitaki ustawi wawanachi wake ni kama katiba ya nchi inavyotamka, bali inataka ustawi wa wawekezaji ambayo ni kinyume na katiba.

  “Upendo wa CCM kwa wananchi ni michango, ambayo wanaihalalisha kwamba kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake, Ilhali zahanati hazina vitanda na wagonjwa wanalala kwenye chaga” alisema shibuda.

  Aliendelea kuwa CCM ni maprofesa wa uongo, huku akiwataka wananchi kuwa makini kupembua mbinchi na mbivu, kwa kujiunga kwenye chama cha wokovu na kuachana na Agano la kale.
  Kuhusu elimu ya uraia Shibuda alisema kuwafundisha wananchi elimu ya uraia ni sawa itawafungua macho na kwamba ndiyo maana CCM haitaki kufanya hivyo ikihofia kuondolewa madarakani.
  “Uchafu wa CCM unanikumbusha maneno ya Baba wa taifa (Hayati Mwalimu Julius Nyerere) aliposema upinza wa kwali utatoka ndani ya CCM, hilindiloninalolifanya mimi ni mbengu inyopandwa na chadema, ni mbegu ambayo itazaa matunda bora,” Shibuda alisema CCM inakumbatia wawekezaji haramu na kusahau wazalendo, huku ikiwakwamisha kwa kuwapandishia kodi..


  Source: Mwananchi

  *********************************************************
  Kwa kasi hii CHADEMA mpaka kufika 2015 viongozi wa CCM wenye vitambi watapungua maana mashambulizi ni kila kona….
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Sasa ni kutwanga kote kote hadi kieleweke.Shibuda fanya kazi ya kung'alisha kiatu hicho kanda ya ziwa, kwani DR.SLAAA tayari alishakiwekea dawa ya KIWI, wabunge fanyeni kazi ya kung'alisha ili kiatu kivaliwe na CDM.CCM miguu yao inanuka, ina-fungus sana watachafua wakikendelea kukivaa.PEOPLESSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  tushukru Babu anatibu magojwa ya moyo maana viongozi wengi wa CCM tunge wapoteza....lol
   
 4. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  I salute you Comrade John Shibuda. Walipoona upo kimya wakaanza zogo kumbe ulikuwa unakusanya nguvu. Sambaratisha kabisa CCM huko usukumani
   
 5. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  safi sana babu!!! ''Upinzani wa kweli utatokea ccm'' (Nyerere). Yeye ni mmoja wao na kwamba mbegu yake imepandwa tayari na CDM, na hivyo ndo maana wana ccm wengi wanamiminika CDM.
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  karudi kundini au
   
 7. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na mimi naongezea:

  Shibuda alisema CCM inakumbatia wawekezaji haramu na kusahau wazalendo, huku ikiagiza askari-mbwa kuuwa raia kwa kuwafyatulia risasi za moto ili kulinda maslahi ya wawekezaji wa kigeni wanaopora madini yetu kama ilivyotokea huko Nyamongo.
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Maneno ya Shibuda ni mazito yamejaa mafundisho na CCM wanajua hayo ayasemayo kwa kuwa si wakweli sasa ni muda wa kuwaanika hawa kila jambo liwe wazi CCM izikwe watanzania wajaribu Chama kingine .
   
 9. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #9
  May 17, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  ulishindwa kutambua kwa nini Kikwete alienda Kugida Kikombe mapeeema?
   
 10. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hongera yako Leo Mzee shibuda umegeuka kuwa dhahabu kwa yale mavuvuzela yetu, Ni juzi tu hata wiki haijapita tangu waendelee kukutukana. Waoneshe mfano wa mpinzani halisi na si wao watu shari.
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Shibuda Msema kweli kaza mwendo,hakikisha wasukuma wetu somo wanalipata waachane na Agano la Kale
   
 12. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #12
  May 17, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  hapa mwananchi wa kawaida ndiye anayechezewa akili. Huyu haleti hali bora na huyu anasaka wanachama, mwisho wa siku wote ni maslahi kwanza. mwananchi wa kawaida hafaidiki ataishia kulalamika.
   
 13. M

  Mbwazoba Member

  #13
  May 17, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!! sio ushabiki, ila nilikuwa nakutamani sana tangu ukiwa chama cha magamba, mzee SHIBUDA umiza sana mzeee, ila nitakutembelea huko shy nijifunze ngano na misemo yako, maana inakufanya uwe na mvuto kwenye hotuba zako mzeee, sasa ccm wana nn cha kuwadanganya watz?????????????
   
Loading...