Shibe na njaa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibe na njaa.

Discussion in 'Jamii Photos' started by Speaker, Feb 27, 2012.

 1. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwao hawa njaa wana iota tu na kuona kwenye movie.

  [​IMG]

  Hawa,wana wakilisha wale ambao kwao wakipata angalau kidogo tu cha
  kufanya mdomo ucheze cheze,siku imeisha.
  [​IMG]
  umaskini.jpg

  Na huyu,...hajui hata mara ya mwisho alikula nini na lini.

  mtz.jpg


  Msitupe vyakula jamani,wakumbukeni wenye njaa.
   
 2. libent

  libent JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  inatia sana huruma yaani mtoto mdogo kajishika tama. Tatizo siku hizi upendo umepoa wanasema kila mtu abebe msalaba wake Mungu atusaidie
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nahisi watanzania tunaongoza kwa uchoyo na ubinafsi,......
  So sad......
   
 4. jchofachogenda

  jchofachogenda JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hii picha ya pili inawakilisha tukio ambalo sijawahi kuliona katika maisha yangu. Huu ni zaidi ya ukatili.
   
 5. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Picha ya kwanza namwona mtoto anafanana sana na Laurent Gbagbo....hata hivyo anawakilisha wengi wa viongozi malimbukeni wa Africa...wanakula mpaka wanakalia sahani zenye chakula wanachokula...wamejawa na ushirikina. Ukimtizama mtoto vizuri utaona kila nyonga ina hirizi yake ...kila mganga anaweka ya kwake au anaambiwa hii ni ya kusafisha sura/nyota ili uwe handsome, watu wakupende na hii ni ya safari za nje, utasafiri wee na hata wakilalama laana haikupati utaendelea tu kudunda mpaka utakapoona umejikusanyia posho za kutosha na kijana wako mkubwa ameshaanzisha miradi mingi kwa niaba yako: na hii ni ya ngekewa na hasa wadosi wa marekani...watawapigia kelele viongozi wengine wote wa kiafrika lakini wewe ng'o!
  Picha ya 2 kadhalika inawakilisha watawala wetu na jinsi wanavyojichukulia madaraka mikononi mwao. Ukitaka uandamane unaambiwa huna kibali, ukitaka kula unaambiwa wakubwa hawajashiba, huna pa kulalamikia
  Picha ya tatu ni uwakilishi wa Mtanzania... Anajuta kuzaliwa Tz. Hakuna kiongozi anayejali hata kama unalala chini ya mti. Mafuriko yamekupiga huna ulichobakishiwa wanasema fuata utaratibu upewe haki yako. Ukifuata utaratibu unapangiwa appointment ya miaka 3 ijayo tena kiongozi huyo akiwa amesafiri ...ukilalama unaambiwa subiri arudi halafu unapigwa kalenda mpya. Pia ni uwakilishi wa mwanafunzi wa chuo aliyejitahidi kusoma akafaulu kwa shida hivyohivyo na ameaply mkopo kaambiwa hana vigezo huku mtoto wa kigogo aliyesoma naye hakufaulu kama yeye ana 100 asilimia ya mkopo huku yeye akiumia. Kila kukicha ni afadhali ya jana.
  Tafakuri ysngu
   
 6. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #6
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  speaker hujambo mkuu..
  sasa huyo baba kwenye picha ya pili kawakanyaga mikono watoto?

  inasikikiitisha kwa kweli.. Njaa kitu kibaya sana..
   
 7. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,471
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  So sad, sipendi kuona watoto wanateseka. Maskin
   
 8. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  du huyo mshua kabila gani?
   
 9. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mkuu picha hizi imenikumbusha kauli moja niliwahi kusikia kwamba, kama kila binadamu atakula kiasi kinachomtosha tu (bila kusaza/kumwaga) basi duniani kusingekuwa na mtu atakayekufa kwa njaa.

  Nakubaliana na wewe mkuu, tusimwage chakula-tupike/tupakue kile ambacho tunaweza maliza ili wengine nao wasiathirike
   
 10. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hahaha,sio ukatili bana.
  Sasa baba atatoa wapi nguvu za kutafuta chakula kingine?
   
 11. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ni mtanzania,.........
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Siku hizi nimejifunza sana,...hata kama sina mtu karibu wa kumpa chakula
  sitaki kumwaga kile ninacho pakua kula.

  Maisha ni safari ya ajabu sana,...ashukuriwe Mungu kwa kufanya mwisho wetu
  kuwa siri kubwa.
   
 13. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  hatari lakini salama.
   
 14. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Lakini mimi hizo picha zote tatu naziangalia kwa jicho la ziada...Picha ya kwanza ni wazi mzazi/mlezi wa huyon mtoto baada ya kushiba huo mpilau akaona ili kujifurahisha amtumbukize kwenye hilo sinia walilolia wali na kumchukua picha. Sitashangaa hiyo picha ikahifadhiwa na huyo bwana akaja kuonyeshwa siku zijazo akiwa amekuwa na hatimaye kubaki kumtania. Picha ya Pili hiyo njemba iliyowabana mikono hao madogo na mibuti yake wakati yeye akifakamia maharage ni kitu cha kutengeneza pia. Watoto wa leo wenye umri unaolingana na wa hao madogo wasingekubali kukaa kimya tena eti mtu amewakanyaga mikono yao yeye anakula na wao wana njaa ya ukweli. Ukitaka kuthibitisha hilo angalia sura zao hazionyeshi hofu, woga wala kutahamaki yaani wame-relax kabisa. So ni picha ya kutaka kutufurahisha tu. Picha ya tatu huyo dogo aliyekaa chini ya mti na kujishika tama naye pia haonyeshi kuwa ni mtoto mwenye njaa. Taswira ya mwili wake tu anaonekana na siha njema. tatizo linaloonekana hapo ni hali ya vumbi alilotapakaa huyo dogo, mavazi machafu na chakafu laiti angekuwa mtoto wa mjini anayepata kuogeshwa kila siku asubuhi na jioni na mavazi mazuri mbona ni bonge a sharobaro!!!. Tuache ku-exaggerate mambo!!
   
 15. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hahaaa dogo anawaza matokeo ya uchaguzi yalivochakachuliwa kudadadeki...yaani haamini kama baba mwaaansha karudi tena ikulu
   
 16. n

  nketi JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  kwani umeambiwa hii picha inawahusu watz?::::::::::::::no research< no right to speak
   
 17. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #17
  Feb 28, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Asante kwa tafakuri iliyoenda shule!
   
 18. n

  nketi JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  kwani umeambiwa hii picha inawahusu watz?::::::::::::::no research< no right to speak
   
 19. n

  nketi JF-Expert Member

  #19
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  "heri njaa ya kujitakia kuliko shibe ya kulazimish"
   
 20. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nani kaziweka hapa?
  au umejifunza hilo neno la kidhungu ukawa una tafuta pa kuliweka ?
   
Loading...