Shetani hakumdanganya Eva/Hawa

Shetani hakumdanganya Eva/Hawa

Mi nadhani shetani aliwaingiza kingi ili wadedi, maana alishasema siku mtakapokula hilo tunda hakika mtakufa; and is what happened after eating
 
Ukisoma siku zote soma Kwa tafakuri na ufahamu.
Walikatazwa kutokula matunda ya mti mmoja tuu ambao ni mti wa ujuzi wa Mema na mabaya.

Embu soma Hii Aya vizuri
Mwanzo 2:
17lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usile, maana siku utakapokula matunda ya mti huo, hakika utakufa.”

Hakusema matunda ya miti iliyokuwepo katikati ya Bustani, kisha aitaje, nop! Bali Kasema matunda ya MTI.

Huo mti WA uzima hawajakatazwa kuula, sema walikuwa haujui.
Kwahyo unataka kusema kuwa kama wangekuwa wajanja wangekula kwanza mti wa uzima halafu ndo wakala wa ujuzi?
Sasaivi binadamu wote tungekuwa miungu hatufi?
 
Au wangekula Ile mti WA ujuzi wa Mema na mabaya waliokatazwa kisha Wakala matunda ya mti uzima.
Wasingekufa.
Ndivyo maandiko yasemavyo
 
Shetani hakumdanganya Hawa na Adam kama baadhi ya viongozi wa dini na baadhi ya wapendwa katika dini wanavyosema na kumlaumu katika ibada zao isipokuwa shetani alimwambia Hawa ukweli.

Shetani alimwambia Hawa ukweli ambao Mungu hakutaka Adam na Hawa waujue. Katika bustani ya Eden Shetani/Ibilisi(nyoka) alimwambia Hawa mambo makuu mawili;

1. Wakila matunda waliyokatazwa watakuwa kama Mungu.

2. Wakila matunda waliyokatazwa hawatakufa.

Nikianza na jambo la kwanza, Shetani alimwambia Hawa kuwa wakila matunda ya mti waliokatazwa basi watakuwa kama Mungu kwa kujua mema na mabaya.

Kweli baada ya Adam na Hawa kula matunda waliyokatazwa walipata maarifa ya kutambua mema na mabaya na kufikia hatua ya kujitambua kuwa wako uchi na kuanza kujifichaficha. Mpaka hapa hakuna uongo uliosemwa na shetani. Rejea (mwa 3:1-12).

Katika jambo la pili, Mungu baada ya kugundua Adam na Hawa wamekula matunda aliyowazuia, wamepata maarifa na wamekuwa kama yeye kwa kujua mema na mabaya aliamua kuwafukuza kutoka katika bustani ya Eden ili wasije kujiongeza tena wakatwaa matunda ya mti wa uzima wakala wakaishi milele. Hii ina maana Shetani hakudanganya kwa maana Adam na Hawa wangefanikiwa kula tunda la mti wa uzima wasingekufa na wangeishi milele na hii inaonyesha shetani hakuwa muongo. Mungu mwenyewe anathibitisha hili jambo katika (mwa 3: 22-24)

Kwa kuzingatia hayo mambo wawili inaonyesha si kila kitokacho kwa shetani ni uongo au ni jambo baya kwa binadamu mana bila nyoka kutimba bustanini huenda binadamu bado angekuwa zezeta asiye na maarifa yoyote lakini pia bila Mungu kuingilia kati huenda binadamu tusingekuwa tunawaza kuhusu kifo na kupata majonzi ya kufiwa na wapendwa wetu mana tungeishi milele. Tafakari
Kama walidanganywa kuwa hawatakufa, wapo wapi mpaka sasa? Hujui biblia hebu nyamaza.
 
Una hoja nzuri. Lakini hapo uliposema kuwa sio kila neno la shetani lina nia mbaya kwa Mwanadamu ndo ulipoboronga.

Lengo la shetani lilikua kuharibu uhusiano wa Mwanadamu na Mungu kama ambavyo alivuruga uhusiano wake na Mungu alipokua mbinguni. Shetani hutumia maagizo ya Mungu kutuvuruga hapohapo. Kumbuka alipomjaribu Yesu Jangwani, alitumia maandiko matakatifu.

Ni kweli hakudanganya, bali alitumia maagizo yaleyale kuwashawishi watoke katika utii. Ndo maana alitumia maneno yaleyale aliyosema Mungu “Ati hivi ndivyo alivyosema Mungu…” Mwanzo 3:1

Lengo la miti ile ilikua ni kipimo cha Utii. Na shetani alifanikiwa kuwatoa katika utii.
 
Ndio maana nasema ni hadithi za sungura!! Mungu mweza ya yote na mwema, hakujua yote hayo? Huenda Mungu na shetani ni kitu kimoja.
 
Back
Top Bottom