Shetani hakumdanganya Hawa na Adam kama baadhi ya viongozi wa dini na baadhi ya wapendwa katika dini wanavyosema na kumlaumu katika ibada zao isipokuwa shetani alimwambia Hawa ukweli.
Shetani alimwambia Hawa ukweli ambao Mungu hakutaka Adam na Hawa waujue. Katika bustani ya Eden Shetani/Ibilisi(nyoka) alimwambia Hawa mambo makuu mawili;
1. Wakila matunda waliyokatazwa watakuwa kama Mungu.
2. Wakila matunda waliyokatazwa hawatakufa.
Nikianza na jambo la kwanza, Shetani alimwambia Hawa kuwa wakila matunda ya mti waliokatazwa basi watakuwa kama Mungu kwa kujua mema na mabaya.
Kweli baada ya Adam na Hawa kula matunda waliyokatazwa walipata maarifa ya kutambua mema na mabaya na kufikia hatua ya kujitambua kuwa wako uchi na kuanza kujifichaficha. Mpaka hapa hakuna uongo uliosemwa na shetani. Rejea (mwa 3:1-12).
Katika jambo la pili, Mungu baada ya kugundua Adam na Hawa wamekula matunda aliyowazuia, wamepata maarifa na wamekuwa kama yeye kwa kujua mema na mabaya aliamua kuwafukuza kutoka katika bustani ya Eden ili wasije kujiongeza tena wakatwaa matunda ya mti wa uzima wakala wakaishi milele. Hii ina maana Shetani hakudanganya kwa maana Adam na Hawa wangefanikiwa kula tunda la mti wa uzima wasingekufa na wangeishi milele na hii inaonyesha shetani hakuwa muongo. Mungu mwenyewe anathibitisha hili jambo katika (mwa 3: 22-24)
Kwa kuzingatia hayo mambo wawili inaonyesha si kila kitokacho kwa shetani ni uongo au ni jambo baya kwa binadamu mana bila nyoka kutimba bustanini huenda binadamu bado angekuwa zezeta asiye na maarifa yoyote lakini pia bila Mungu kuingilia kati huenda binadamu tusingekuwa tunawaza kuhusu kifo na kupata majonzi ya kufiwa na wapendwa wetu mana tungeishi milele. Tafakari