Sheria za barabarani Mbeya

Ravalomanana

JF-Expert Member
Sep 8, 2018
1,384
1,313
Mkoa wa Mbeya umeweka utaratibu wa magari ya abiria na malori kusubiriana kwenye milima ili yapite kwa zamu. Katika utaratibu huu, magari husubiri kwa muda wa nusu saa ili magari ya aina nyingine yapite.

Utaratibu huu uko barabara ya Mbeya -Tunduma na huchelewesha sana abiria sababu kuna maeneo kama matatu hivi yenye miinuko mikali kama pale Mbalizi.

Rai yangu kwa viongozi wangetafuta njia mbadala ya kupunguza ajali ambazo hazitakua kero kwa abiria.
 
Kama itasaidia kupunguza ajali it's ok.
lkn nadhani kunaweza kuwa na suluhisho zuri zaidi ya hilo....
 
Kama utaratibu huu unasaisia kupunguza ajali hata wakiongeza muda wa kusubiriana na kuwa lisaa lizima ni sawa tu
 
Zamani nilikuwa mwenyeji wa mkoa huo,Sasa hivi imegeuka njia tu ya mi kupita kuelekea kwetu SONGWE.sio Jambo baya kusubiria kwa usalama wa uhai wetu.Nadhani Sugu au tulia mmoja wao atayepita anayo kazi kubwa kuishawishi wizara ya ujenzi kujenga fly over ya 3 Tanzania sio tu dar,kwani hata barabara hiyo Ina umuhimu mkubwa kwa maslahi ya nchi kwani ni barabara inayotuunganisha na nchi zilizo kusini mwa afrika
 
Sema kwasababu huwa kuuliza maswali magumu, inaonekana umetumwa. Ahadi ya barabara mbilimbili ulitolewa, lakini miaka imeisha, hata Moja tu shida.
 
Kwa zile ajali za mlima mbalizi boratu iwe hivyo wakati tukisubiri mbinu mpya. Bora kuchelewa ufike salama, kumbuka Tunduma ndio boda kubwa zaidi Tz hivyo itakuwa na malori mengi zaidi.
Ughonile.
 
Ni bora kusubiriana mkuu maana ule mteremko umeua raia wengi mno na kuwaacha wengine na ulemavu wa kudumu.
 
Bora watumie huo utaratibu ajali zimezidi sana kwenye hiyo bara bara unazungumzia muda wakati huna uhakika wa kufika salama kama mazingira sio salama kwa abiria...
 
Back
Top Bottom