Sheria ya uuzaji mashamba. Swali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya uuzaji mashamba. Swali

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Namtih58, Feb 11, 2009.

 1. N

  Namtih58 JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 236
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  When it comes to harmonisation of laws in the region, mojawapo wa swala linalo jadiliwa sana ni la ardhi.

  Leo mimi nina swali

  Je itakuwa kosa kutakiwa mtu kumuomba ruksa mke/mume na watoto{tukizingatia umri}, kabla ya kukubaliwa kuuza/kugawa shamba.
   
 2. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Suala la ardhi/shamba lina matatizo yake tena kama ni la kurithi au ulinunua pamoja na ndugu/mke wako. Pia inategemea eneo mnalomiliki,yani ni eneo moja kubwa au mbalimbali yani mashamba yapo mahali tofauti.
  Kama shamba linamilikiwa na zaidi ya mtu mmoja yaani wewe na ndugu/mke/watoto, ni vizuri kuwashirikisha wakati una nia ya kuuza hata kama unataka kuuza kipande chako kidogo hata kama mlikuwa mlimegeana.
  Pia hata kama shamba ulirithi au ulinunua peke yako bila kumshirikisha mtu ni vyema kwa familia(mke na watoto) kushirikishwa kwa nia ya kuwataarifu dhumuni lako wakati unataka kuliuza hilo shamba/ardhi, maisha hayatabiriki na siku hazifanani na familia yako ni muhimu!
   
 3. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  aroo, inategemeana hiyo mali/shamba ni mali ya nani kisheria. kama ni yako binafsi, hauhitaji ruhusa ya mtu mwingine. kama ni mali yako wewe na mkeo, lazima upate consent ya mkeo. usipofanya hivyo hiyo disposition itakuwa void. ni sawa na mnunuzi kaingizwa mjini na ndio hapo mtakaposhikana naye mashati, kama mchaga atakuja na panga. kwa kawaida, mali nyingi kama umeoa mkuu lazima itakuwa yako wewe pamoja na mkeo, hivyo ruhusa ya mkeo inahitajika. watoto si lazima, hiyo siyo mali yao. haujafa bado mzee unataka waanze kutumia urithi hata kabla haujaenda kaburini...hahaha, hata kama umeshawaandikia wills, itakuwa applicable pale utakapokuwa umekufa. na, will yenyewe uzuri wake warithi huwa hawatakiwi kuiona hadi pale utakapokufa ndo siku yao ya kwanza kuiona ulivyowaandikia. nimeongea kwa lugha rahisi, siyo ya kisheria ili uelewe. una swali?

  however, watoto wanaweza wakapinga kama watakuwa na akili, wakagundua kuwa, kwa kufanya hivyo utaathiri maslahi yao, ya mama yao au ya kitu chochote kile. inategemea sababu yoyote ile watakayotoa. na hawatakiwi kukukataza home kule, wanatakiwa waende wakaweke pingamizi mahakamani na maelezo ya mahakama kuhusu uhalali na athari za kuuza. wakiwa na sababu inayokubalika, wanaweza wakawini, wakishindwa ndi hivyo tena. ila kwa kifupi, kama ni kwa nia nzuri, na hakuna madhara, we uza tu kama title/hati ya ardhi hiyo ni jina lako peke yako. kama hati ina mkeo, kaka yako au mtu yoyote yule, lazima consent yake mzee.
   
 4. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Sheria ya Ardhi ya Vijijini imeweka bayana; Mwenzi wako lazima akubali tena kwa maandishi. Anaweza kuweka pingamizi mahakamani. Kwa hiyo mzee angalia sana. Soma Kifungu cha 161-164 cha sheria ya Ardhi(No. 4, 1999) kimebainisha vizuri zaidi. Sheria inamlinda zaidi mwenzi wako. Kuhusu suala la watoto, kama ardhi ni ya kijiji then Baraza la ardhi la kijiji linaweza kukataa kubariki mauzo. Kuna vifungi vingine vinavyoongelea rushwa na ubatili wa mauzo yanayonendana na rushwa kwa hiyo mzee angalia watu wa Haki Ardhi wasije kukushukia kama mwewe.

  Shadow
   
Loading...