Sheria ya Upekee wa Uelewa na Uhalisia wa Maisha (Kanuni Ya Nne ya Akili na Ulimwengu)

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,920
3,221
Kanuni za Akili na Ulimwengu

Kanuni ya nne - Sheria ya Upekee wa Uelewa na Uhalisia wa Maisha

Wewe ni Kama Sumaku Inayoishi.

Maisha unayoishi hivi sasa hayajaachana na ulimwengu unaoendelea akilini. Ukiwa umefuatilia sheria ya kwanza utakuwa umejifunza kuwa kila tokeo lina chanzo chake, sheria ya pili ikasema mwanadamu ana uhuru wa kufikiria na ni yeye mwenyewe ndiye mwenye uwezo wa kutumia akili yake kufikiria na sio mwingine, kila mmoja ana uhuru wa kufikiria na kanuni ya tatu ikasema kuwa unapoelekeza umakini wako napo panakua.

Sheria au kanuni hii ya nne inafuata baada ya kuelewa kanuni zile tatu zilizotangulia. Kanuni zote zimeonyesha umuhimu wa akili na ufahamu wetu katika kutengeneza maisha yetu. Sheria hii ni kama imedhibitisha kabisa kwa kusema kuwa uhalisia wa kila mwanadamu unatokana na kinachoendelea kwenye akili yake.

Ulimwengu wa ndani unahusisha mengi sana, unahusisha imani yako juu ya maisha, uelewa wako juu ya maisha, jinsi unavyoona na kuweka mtazamo wako katika mawazo, fikra na hali mbalimbali, wasiwasi, hisia (mbaya na nzuri), mawazo ya ndani ya kujisemea mwenyewe, matendo yako utendayo ndani na nje ya ufahamu wako n.k

Kila mwanadamu, kila mtu, anaishi katika uelewa wake juu ya ulimwengu huu. Hii ndio maana, kila mmoja ana Nature of Reality yake (Uhalisia wake). Kila mtu anaishi katika dunia yake pekee na maalum kwa upande wake. Kwa mara ya kwanza unaweza ukashangaa kuona ufahamu huu lakini ukizidi kuuweka akilini na kuutafakari kwa kutazama maisha na watu mbalimbali utaona kuna ukweli mkubwa sana ambao ni wachache wameweza kuugundua na kuona jinsi kanuni hii inavyofanya kazi katika maisha yetu.

Kutokana na sheria hii inamaanisha kuwa wanadamu wanatofautiana sana juu ya uhalisia walio nao wa ulimwengu, kila mtu ana uhalisia wake na tafsiri yake ya ndani. Lakini utofauti huo ukiuchunguza utagundua umetokana na utofauti wa akili na matumizi ya ufahamu kwa kila mtu.

MIFANO.
Bugs: Huu ni mtazamo walio nao watu wanaoitazama dunia kifizikia. Maisha yao yanatokana na uelewa wao unaopatikana katika milango ya ufahamu, aina hii ya watu inategemea milango ya ufahamu kuelewa ulimwengu huu. Wengi wao huamini kuwa maisha yanatokea tu, hamna chanzo cha hali walizonazo wala hamna chanzo cha matokeo wanayoyaona wao huona matokeo ni matokeo tu na hawawazii kama kunaweza kukawa na chanzo, hawawazi kuwa kuna ulimwengu wa ndani bali wao huishi kwa kutazama ulimwengu wa nje na kuona upo tu kama ulivyo. Watu hawa huweka mitazamo yao katika kuamini bila kufuatilia chanzo kwani aina hii ya watu hutegemea dunia ya nje.

Watesekaji - Hawa pia nao wanaishi katika uelewa wao wa uhalisia wa maisha. Hawa hutumia ufahamu wao kuweka umakini kwenye pande mbili mbili za maisha. Kila wanachoona wanaona kuna sides mbili, wanaona kuna pande mbili mbili. Aina hii ya watu wameweza kuendeleza ufahamu wao kwa kuona kuna mema na mabaya, mazuri na mabaya, mwanga na giza, shetani na Mungu, chuki na upendo, afya na magonjwa, umasikini na utajiri. Yaani kila wanachokiona lazima waona kinyume chake. Aina hii ya watu hujikita sana katika imani na kuona kila jambo lina pande yake na wanahukumu kuwa upande fulani ndio mbaya na huu ndio mzuri. Hupoteza wakati wao kuona hiki ni kema na kingine ni kibaya badala ya kufuatilia ni kwanini. Aina hii ya watu huweka judgements na ni wepesi kuhukumu.
Wengi wao huamini kuwa Mungu ndiye mpaji, na wanaamini kuwa wakikaa katika mazuri watapata mazuri na wakikaa katika mabaya Mungu atawahukumu na kuwateketeza.

Waabuduji- Hawa huamini kuwa baraka na mikosi inatoka nje yao. Hawa hawaamini kuwa maisha yao yanahamasika na wao bali wao huamini kuwa maisha yao yameundwa na hali au na chanzo ambacho wao hawawezi kukiongoza. Wao huweka imani zao nje yao. Wengi huamini mambo ya kuridhi, utabiri wa nyota, jinsia, miaka, rangi za mwili, na elimu zao ndio peke yake vinatengeneza maisha ya watu. Wengine huamini kabisa race/aina fulani ya watu ina akili zaidi yao. Pia huamini kuwa mambo yanayotokea katika maisha yao huadhiriwa na rangi walizovaa, au mafuta wanayojipaka, harufu na manukato wanayotumia, anachoambiwa na walimu wake au na jamii, waganga wa jadi, vyakula wanavyokula, mpangilio wa nyumba na jinsi wanavyolala, nyota, majina, miaka ya kuzaliwa n.k Kwa kifupi aina hii ya watu huamini dunia ya nje yao ndio inapangilia maisha yao.

Wapanda Milima - Aina hii ya fikra ni aina ambayo wanadamu wengi wa aina hii wameonekana kama watu waliofanikiwa katika maisha. Hawa huamini kuwa wana nguvu ya asili ndani yao katika kutengeneza maisha yao. Wanaamini uwezo wao, akili zao na juhudi zao katika maisha. NI aina ya watu ambao waliwahi kutamani kutimiza jambo fulani, wakajitahidi katika maisha yao kulitimiza, japokuwa waliona changamoto lakini hawakuweka akili zao kwenye kushindwa bali walizidi kuamini nguvu ya ndani na hatimaye wakafanikiwa malengo yao na kuona umuhimu wa kuwa na imani na kuwaza mawazo chanya. Na baada ya kufanikiwa malengo yao hawa wanajitahidi kuhamasisha wengine kujituma na kuwashauri wajaribu kuanda milima au vikwazo walivyo navyo kwa imani ya kujiamini. Hawa huishia kuwa wabunifu wakuu wa vitu mbali mbali, n.k
Wapanda Milima

Waamini - Hawa ni wale wanaoamini kuwa kuna Supreme Master lakini hawashikiliwi na kulazimika kuamini katika dini. Hawa huamini huisoma dunia ya kiimani na dunia ya kifizikia kwa pamoja kuelewa ulimwengu. Hawa huona maisha ni mageuzi na kila siku jamii zinazidi kuwa na akili na wanaamini hapo baadaye mwanadamu atazidi kubadilika na kuzidisha akili na huona kuwa maisha ni maajabu na wao hutumia maisha yao kujifunza siri za maisha. Hawa hawana sifa ya kuamini tu kila jambo bali wanapenda kulichunguza na kupenda kujua mengi. Wengi hufikia hatua ya kufunuliwa na kuamka baada ya kufahamu sana Nature of Reality (Uhalisia).

Mgawanyiko huo haujalenga kuwagawanya watu mbali mbali katika mitazamo yao bali ni kama mfano kuonyesha kuwa wanadamu wanaishi katika tafsiri yake tofauti tofauti juu ya ulimwengu. Na tafsiri hizo zinaadhari maisha yetu.

Kanuni hii ni mwanga kwani inakusaidia kuzidi kujichunguza na kuchagua mtazamo ambao umejifunza na kuuchunguza badala ya kuamini tu kila jambo. Ufahamu kuwa unachoamini na kufahamu juu ya maisha hakina umbali na maisha yako. Ni kama gurudumu.

@blessing-baraka @UNDENIABLE @KikulachoChako @aretaskimario @Patrickn @Noah.. @Ms.Lincoln @IGWE @aretaskimario @crunkstaa @Matola @it is me
 
mkuu Apollo you deserve my like

shukrani sana kwa chakula cha ubongo na ubarikiwe sana kwa moyo wako mkunjufu
ni watu wachache sana wenye moyo kama wako wa kujitolea muda wao na kutoa elimu yakinifu kwa wa-tanzania wenzao bila ada yoyote

Cc: mshana jr
Cc: Monstgala
Cc: Kiranga
Cc: Dreson4
Cc: Ishmael

. made in mby city.
 
Last edited by a moderator:
mkuu Apollo nakuelewa sana mana ushawahi kunitumia hadi vitabu vya hii elimu ila sijaona sehemu ya 2 na ya 3 km vp fanya kunitag ya 2 na 3
 
mkuu Mwamba028 habari yako ?
huyu ndugu yetu siyo mchoyo wa maharifa kama wajuzi wa mambo mengine

mkuu kama hautajali fanya kunitumia hivyo vitabu na mimi nipanue uelewa
ikiwezekana vi-upload hapahapa jukwaani

. made in mby city.
 
Last edited by a moderator:
Mimi nadhani utaniweka kwenye kundi la mwisho, maana I always think humans bado tuna evolve, na the next stage ya evolution has to be something more intelligent than humans, na i think its either machines(computers) zenyewe ndo iwe next stage, au basi sisi wenyewe tuwe kama cyborgs kwa kujijaza na gadgets mbalimbali mwilini...

Mfano data sasa hivi tunatunza kwenye vitu kama hard disks na if u need more data most times u have to go bigger in terms of size, lakini we can still keep data kwenye DNA, encoding GTAC into something that can be decoded by a computer is very possible, na kwa sababu hii basi binadamu anaweza kutumika kama data storage, binadamu moja anaweza tunza data zaidi ya data yote iliyopo kwenye internet nzima kwa sasa, Facebook nzima na data zao zote inaweza ingia kwenye kidole kimoja tu, if only we can fasten the reading and writing process maana sasa hivi inawezekana lakini ni slow, we could start keeping data into our own bodies ikiwezekana hata kuzipass to generations to come.

Thats one example ila still more to come where we not only store the data lakini kuweza kuretrieve into our heads kama unavofikiria sasa hivi data zinakuja, basi same thing ukitaka kujua history basi unadownload data into your brain zinakua converted na unaweza ukarecall data kwa neural activity tu..

Hiyo ndo the next stage in human evolution, a point where we don't need to sit down in classes and learn, you want to be a pilot u just download the entire manual into your brain, there u go. Wanna be a doctor you download an entire book to your brain.
 
mkuu Apollo you deserve my like

shukrani sana kwa chakula cha ubongo na ubarikiwe sana kwa moyo wako mkunjufu
ni watu wachache sana wenye moyo kama wako wa kujitolea muda wao na kutoa elimu yakinifu kwa wa-tanzania wenzao bila ada yoyote

Cc: mshana jr
Cc: Monstgala
Cc: Kiranga
Cc: Dreson4
Cc: Ishmael

. made in mby city.

Asante kwa kuni-tag katika topic hii Etcetera. Ni kama perfect place to share and discuss some deep related issues, lakini pia kuleta challenges katika mitazamo hii kwa ujumla wake au kwa vipengele vyake.
 
Last edited by a moderator:
Binafsi napenda kuchunguza mambo zaidi kwa kina sana kuliko wengi wanapoishia hivyo ingawa nasoma mitazamo tofauti nadhani ni budi kwa jukwaa kuchambua mitazamo kuliko kuiandika tu kama ilivyoandikwa pengine. Utaniwia radhi kwa kutaka ufafanuzi zaidi wa kina ambao utaweka wazi hizi zinazoitwa sheria au kanuni za mind and universe.

Kwa kuwa uko topic ya nne basi nami nitajikita hapa hapa katika vipengele hivi katika changamoto ili labda kuelewa zaidi au kuonesha udhaifu wa mitazamo hii.

Mfano umesema: "Maisha unayoishi hivi sasa hayajaachana na ulimwengu unaoendelea akilini. Ukiwa umefuatilia sheria ya kwanza utakuwa umejifunza kuwa kila tokeo lina chanzo chake, sheria ya pili ikasema mwanadamu ana uhuru wa kufikiria na ni yeye mwenyewe ndiye mwenye uwezo wa kutumia akili yake kufikiria na sio mwingine, kila mmoja ana uhuru wa kufikiria na kanuni ya tatu ikasema kuwa unapoelekeza umakini wako napo panakua.Sheria au kanuni hii ya nne inafuata baada ya kuelewa kanuni zile tatu zilizotangulia.

Kanuni zote zimeonyesha umuhimu wa akili na ufahamu wetu katika kutengeneza maisha yetu. Sheria hii ni kama imedhibitisha kabisa kwa kusema kuwa uhalisia wa kila mwanadamu unatokana na kinachoendelea kwenye akili yake
."Labda kwa kuanzia, kwa kanuni hii ya nne una maana Mawazo yako ndiyo yajengayo uhalisia wako!?
In what extent?

Hii nadharia ina loop-holes nyingi na haipaswi kuitwa kanuni kwa maana halisi ya kanuni ambazo kamwe haziyumbi kwa namna yeyote mfano angalia fundamental laws of physics, zinapimika na kujaribika kwa kila namna na zimesimama kama zilivyo. Hizi tunaziita kanuni au sheria kwa kuwa hazina matundu wala waziyumbi na hivyo kama binadamu tumeweza kuunda vitu madhubuti ( machines, tools, buildings etc) na kwa mwendelezo kwa kutumia kanuni hizi.

Kwamba mawazo ya kiumbe jamii ya homo sapiens yanatengeneza na kuhalisi physical universe anayoitazama au kuifikiria! Hii kwa mtazamo wa kina concept hii kwanza inapendekeza kwamba ili ulimwengu uwepo lazima maisha haya tuyajuayo yawepo ili kuutazama. Na kutoka katika mada, observer wa ulimwengu amelengwa kuwa kiumbe mwenye conscious na bila huyu kuutazama ulimwengu basi uhalisia ulimwengu huu unakuwa haupo, so to say.

Kwa namna nyingine ambayo ni soft lakini iliyotolewa katika mzizi wa mtazamo huu ni kwamba mwanadamu yuko responsible kwa uhalisia wake mwenyewe kama ulivyoanisha na hivyo basi kwa kuwa walio nje yake wanaweza kuwa si halisi kama hawatokea katika akili yake. Nachelea kusema kwamba ingawa kuna mchango mdogo wa matokeo (performance) katika uhalisia wa mwanadamu kutokana na anachotaka kiwe sehemu kubwa haibebwi na "kinachoendelea katika akili yake" hivyo si sawa kusema hii ni kanuni.

Wanaokubaliana na mtazamo huu wa mada watapaswa kuamini kuwa mawazo yana uwezo wa kuumba, kuendesha na kuwa na nguvu juu ya uhalisia wa nje/unaotokea. Kwamba matendo, matukio, vitu na muda na space vinaweza kuendeshwa kwa mawazo ya mtu mwenyewe akili mwake na hivyo kuwa reality. Je ni kweli mawazo ya mtu yana uwezo huu as inevitable consequence of situation that cannot be altered of changed mpaka hali hii iitwe kanuni? Hapana hii ni wrong. Mawazo/fikra za kiumbe wa kibailojia mwenye asili ya carbon hayana nguvu ya kuumba uhalisia wa ulimwengu wake na kuwa na full control ya ulimwengu huo.

Human beings kama living observers wa physical universe na fundamental physical constants zake hatuwezi wala hatubebi uwezo wa kuwa creators wa ulimwengu na uhalisia tunaouona individually. We are simply observing. Impact inayotokana na interference yetu katika ulimwengu ni sehemu ndogo ambayo nayo ni chini ya physical fundamental laws of the universe lakini si kanuni ya akili. Nadhani ingekuwa vema kwa wewe kufafanua kwa extent gani thoughts zina-create someone's reality? Kama ni katika performance tu hii ni rahisi sana kuegemea katika kivuli hicho ambacho mifano yake haipaswi kuifanya concept hii iwe universal law.

Ukiamini kwamba utakuwa rais wa nchi siku moja hii itakusaidia katika kuelekeza nguvu zako kwenye matokeo hayo lakini si sheria kwamba kwa kuwa umeweka thoughts hizo kwa asilimia mia basi thoughts hizi zina nguvu ya kufanya hii iwe reality, na ni kanuni nope! Tunaweza kusema umejaribu kuinfluence matokeo kwa kuwa kuwaza hili basi unaweza jenga mazingira fulani ya kufanikisha matokeo lakini huna mamlaka ya mwisho ya matokeo haya. Hapo ndipo hii inakuwa si kanuni bali concept tu! Na hii ni katika performance tu kwingineko ni pagumu zaidi. Hakuna any fine tuned phenomena katika universe ambayo inamhitaji kiumbe kutoka duniani awepo ndio nayo iwepo katika uhalisia wake.

Rahisi zaidi ni kwamba kama mawazo yetu yana nguvu hii ya ku-influence reality katika phyisical world, nataka kujua kwa uhakika kama mtu aliyefuzu vizuri katika kuielewa concept hii amewahi kuwaza kupaa angani na akaweza kupaa huku watazamaji wakishuhudia nguvu ya mawazo katika fikra za mwanadamu?.

Naomba mwanga katika haya kwa kuanzia ili tuanze kujadili zaidi vipengele vingine.
 
mkuu Mwamba028 habari yako ?
huyu ndugu yetu siyo mchoyo wa maharifa kama wajuzi wa mambo mengine

mkuu kama hautajali fanya kunitumia hivyo vitabu na mimi nipanue uelewa
ikiwezekana vi-upload hapahapa jukwaani

. made in mby city.

mkuu salama sana,,km vp ntumie email yako pm nikufowadie mana ku atach hapa vinakataaga
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Apollo nakusoma vizuri. but katika hayo makundi uliyoorodhesha hapo kuna hali fulani ya uwezekano wa mtu mmoja kuwa na sifa ya makundi zaidi ya mawili. Unalielezea vipi suala hilo mkuu?
 
Last edited by a moderator:
mkuu Apollo you deserve my like

shukrani sana kwa chakula cha ubongo na ubarikiwe sana kwa moyo wako mkunjufu
ni watu wachache sana wenye moyo kama wako wa kujitolea muda wao na kutoa elimu yakinifu kwa wa-tanzania wenzao bila ada yoyote

Cc: mshana jr
Cc: Monstgala
Cc: Kiranga
Cc: Dreson4
Cc: Ishmael

. made in mby city.

Nimerejea ngoja kupambuzuke nije hapa
 
Last edited by a moderator:
Kanuni za Akili na Ulimwengu

Kanuni ya nne - Sheria ya Upekee wa Uelewa na Uhalisia wa Maisha

Wewe ni Kama Sumaku Inayoishi.

Maisha unayoishi hivi sasa hayajaachana na ulimwengu unaoendelea akilini. Ukiwa umefuatilia sheria ya kwanza utakuwa umejifunza kuwa kila tokeo lina chanzo chake, sheria ya pili ikasema mwanadamu ana uhuru wa kufikiria na ni yeye mwenyewe ndiye mwenye uwezo wa kutumia akili yake kufikiria na sio mwingine, kila mmoja ana uhuru wa kufikiria na kanuni ya tatu ikasema kuwa unapoelekeza umakini wako napo panakua.

Sheria au kanuni hii ya nne inafuata baada ya kuelewa kanuni zile tatu zilizotangulia. Kanuni zote zimeonyesha umuhimu wa akili na ufahamu wetu katika kutengeneza maisha yetu. Sheria hii ni kama imedhibitisha kabisa kwa kusema kuwa uhalisia wa kila mwanadamu unatokana na kinachoendelea kwenye akili yake.

Ulimwengu wa ndani unahusisha mengi sana, unahusisha imani yako juu ya maisha, uelewa wako juu ya maisha, jinsi unavyoona na kuweka mtazamo wako katika mawazo, fikra na hali mbalimbali, wasiwasi, hisia (mbaya na nzuri), mawazo ya ndani ya kujisemea mwenyewe, matendo yako utendayo ndani na nje ya ufahamu wako n.k

Kila mwanadamu, kila mtu, anaishi katika uelewa wake juu ya ulimwengu huu. Hii ndio maana, kila mmoja ana Nature of Reality yake (Uhalisia wake). Kila mtu anaishi katika dunia yake pekee na maalum kwa upande wake. Kwa mara ya kwanza unaweza ukashangaa kuona ufahamu huu lakini ukizidi kuuweka akilini na kuutafakari kwa kutazama maisha na watu mbalimbali utaona kuna ukweli mkubwa sana ambao ni wachache wameweza kuugundua na kuona jinsi kanuni hii inavyofanya kazi katika maisha yetu.

Kutokana na sheria hii inamaanisha kuwa wanadamu wanatofautiana sana juu ya uhalisia walio nao wa ulimwengu, kila mtu ana uhalisia wake na tafsiri yake ya ndani. Lakini utofauti huo ukiuchunguza utagundua umetokana na utofauti wa akili na matumizi ya ufahamu kwa kila mtu.

MIFANO.
Bugs: Huu ni mtazamo walio nao watu wanaoitazama dunia kifizikia. Maisha yao yanatokana na uelewa wao unaopatikana katika milango ya ufahamu, aina hii ya watu inategemea milango ya ufahamu kuelewa ulimwengu huu. Wengi wao huamini kuwa maisha yanatokea tu, hamna chanzo cha hali walizonazo wala hamna chanzo cha matokeo wanayoyaona wao huona matokeo ni matokeo tu na hawawazii kama kunaweza kukawa na chanzo, hawawazi kuwa kuna ulimwengu wa ndani bali wao huishi kwa kutazama ulimwengu wa nje na kuona upo tu kama ulivyo. Watu hawa huweka mitazamo yao katika kuamini bila kufuatilia chanzo kwani aina hii ya watu hutegemea dunia ya nje.

Watesekaji - Hawa pia nao wanaishi katika uelewa wao wa uhalisia wa maisha. Hawa hutumia ufahamu wao kuweka umakini kwenye pande mbili mbili za maisha. Kila wanachoona wanaona kuna sides mbili, wanaona kuna pande mbili mbili. Aina hii ya watu wameweza kuendeleza ufahamu wao kwa kuona kuna mema na mabaya, mazuri na mabaya, mwanga na giza, shetani na Mungu, chuki na upendo, afya na magonjwa, umasikini na utajiri. Yaani kila wanachokiona lazima waona kinyume chake. Aina hii ya watu hujikita sana katika imani na kuona kila jambo lina pande yake na wanahukumu kuwa upande fulani ndio mbaya na huu ndio mzuri. Hupoteza wakati wao kuona hiki ni kema na kingine ni kibaya badala ya kufuatilia ni kwanini. Aina hii ya watu huweka judgements na ni wepesi kuhukumu.
Wengi wao huamini kuwa Mungu ndiye mpaji, na wanaamini kuwa wakikaa katika mazuri watapata mazuri na wakikaa katika mabaya Mungu atawahukumu na kuwateketeza.

Waabuduji- Hawa huamini kuwa baraka na mikosi inatoka nje yao. Hawa hawaamini kuwa maisha yao yanahamasika na wao bali wao huamini kuwa maisha yao yameundwa na hali au na chanzo ambacho wao hawawezi kukiongoza. Wao huweka imani zao nje yao. Wengi huamini mambo ya kuridhi, utabiri wa nyota, jinsia, miaka, rangi za mwili, na elimu zao ndio peke yake vinatengeneza maisha ya watu. Wengine huamini kabisa race/aina fulani ya watu ina akili zaidi yao. Pia huamini kuwa mambo yanayotokea katika maisha yao huadhiriwa na rangi walizovaa, au mafuta wanayojipaka, harufu na manukato wanayotumia, anachoambiwa na walimu wake au na jamii, waganga wa jadi, vyakula wanavyokula, mpangilio wa nyumba na jinsi wanavyolala, nyota, majina, miaka ya kuzaliwa n.k Kwa kifupi aina hii ya watu huamini dunia ya nje yao ndio inapangilia maisha yao.

Wapanda Milima - Aina hii ya fikra ni aina ambayo wanadamu wengi wa aina hii wameonekana kama watu waliofanikiwa katika maisha. Hawa huamini kuwa wana nguvu ya asili ndani yao katika kutengeneza maisha yao. Wanaamini uwezo wao, akili zao na juhudi zao katika maisha. NI aina ya watu ambao waliwahi kutamani kutimiza jambo fulani, wakajitahidi katika maisha yao kulitimiza, japokuwa waliona changamoto lakini hawakuweka akili zao kwenye kushindwa bali walizidi kuamini nguvu ya ndani na hatimaye wakafanikiwa malengo yao na kuona umuhimu wa kuwa na imani na kuwaza mawazo chanya. Na baada ya kufanikiwa malengo yao hawa wanajitahidi kuhamasisha wengine kujituma na kuwashauri wajaribu kuanda milima au vikwazo walivyo navyo kwa imani ya kujiamini. Hawa huishia kuwa wabunifu wakuu wa vitu mbali mbali, n.k
Wapanda Milima

Waamini - Hawa ni wale wanaoamini kuwa kuna Supreme Master lakini hawashikiliwi na kulazimika kuamini katika dini. Hawa huamini huisoma dunia ya kiimani na dunia ya kifizikia kwa pamoja kuelewa ulimwengu. Hawa huona maisha ni mageuzi na kila siku jamii zinazidi kuwa na akili na wanaamini hapo baadaye mwanadamu atazidi kubadilika na kuzidisha akili na huona kuwa maisha ni maajabu na wao hutumia maisha yao kujifunza siri za maisha. Hawa hawana sifa ya kuamini tu kila jambo bali wanapenda kulichunguza na kupenda kujua mengi. Wengi hufikia hatua ya kufunuliwa na kuamka baada ya kufahamu sana Nature of Reality (Uhalisia).

Mgawanyiko huo haujalenga kuwagawanya watu mbali mbali katika mitazamo yao bali ni kama mfano kuonyesha kuwa wanadamu wanaishi katika tafsiri yake tofauti tofauti juu ya ulimwengu. Na tafsiri hizo zinaadhari maisha yetu.

Kanuni hii ni mwanga kwani inakusaidia kuzidi kujichunguza na kuchagua mtazamo ambao umejifunza na kuuchunguza badala ya kuamini tu kila jambo. Ufahamu kuwa unachoamini na kufahamu juu ya maisha hakina umbali na maisha yako. Ni kama gurudumu.

@blessing-baraka @UNDENIABLE @KikulachoChako @aretaskimario @Patrickn @Noah.. @Ms.Lincoln @IGWE @aretaskimario @crunkstaa @Matola @it is me

Sina la kuongeza kwakweli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom