Sheria ya Uchaguzi Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya Uchaguzi Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rodgers, Jul 1, 2011.

 1. R

  Rodgers Senior Member

  #1
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 108
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Nimekuwa nikifuatilia chaguzi mbalimbali zilizofanyika hapa Tanzania kwa muda mrefu, kwa kweli nimekuwa nikitatizika na suala moja ambalo nimeona ni bora niombe msaada kwa wadau mbalimbali wakiwemo wanasheria.

  Katika chaguzi zetu mbalimbali za kisiasa inapotokea mgombea kukosa mpinzani kwa sababu zozote zile , Tume ya uchaguzi huwa inamtangaza mgombea aliyekosa mpinzani kuwa mshindi bila ya kupigiwa kura. Kwa maoni yangu nadhani dhana hii siyo sahihi hasa kwenye mfumo wa vyama vingi ambapo pia tumezuia wagombea huru/binafsi. Mara nyingi kwenye chaguzi zetu hasa za ngazi ya udiiwani na ubunge tumesikia baadhi ya wagombea wakijitoa kwenye dakika za mwisho huku ikidaiwa kuwa wamerubuniwa kwa fedha na hivyo kumuachia mgombea mmoja ambapo mojakwa moja hutangazwa kuwa mshindi.

  Ikumbukwe kuwa sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985 pamoja na Katiba ya Tanzania vinaruhusu mtu yeyote mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 kupiga kura ili kuchagua kiongozi na haijalishi kama mpiga kura huyo ni mwanachama wa chama chochote cha kisiasa ama laa. Wakati huo huo sheria hiyo pamoja na Katiba vinamzuia mtu huyohuyo kugombea nafasi ya kisiasa iwapo siyo mwanachama wa chama cha kisiasa chenye usajili rasmi.

  Hofu yangu inajitokeza kwenye hatua hii katika mchakato mzima wa uchaguzi, je itakuwaje mathalani wagombea wa kiti cha uraisi kupitia vyama mbalimbali wakajitoa dakika za mwisho baada ya muda kupita aidha kwa kurubuniwa kwa fedha ama sababu nyingine yeyote na kumuachia mgombea mmoja tuu wa uraisi. je tume ya uchaguzi itampitisha mgombea aliyebaki kama Raisi mteule bila ya kupigiwa kura?

  Mathalani kama itakumbukwa kwenye uchaguzi wa mwaka jana kwenye jimbo la nyamagana huko jiji la mwanza, msimamizi wa uchaguzi alimtangaza bwana L. Masha kama mshindi kutokana na pingamizi alilokuwa amemuwekea mgombea wa Chadema.Hata hivyo mgombea aliyewekewa zuio alirudishwa kwenye kinyang'anyiro baada ya kukata rufaa kwenye Tume ya uchaguzi ya Taifa. Matokeo ya kura yanajulikana kwani Bwana aliyetangazwa mshindi hapo awali alishindwa vibaya sana kwani hakuwa chaguo la wana- nyamagana
   
 2. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2015
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,491
  Likes Received: 4,764
  Trophy Points: 280
  hapa ni kiongo bongo tu mkuu hakuna sheria wala chombo
   
Loading...