Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?

WAzo zuri; lakini unafanyaje kuhusu kumpata mtu mwingine kuchukua nafasi ya yule aliyejiuzulu? au unapendekeza watu wasiwe na wawakilishi kwa vile mtu kajiuzulu.
Naaminii kunaa katibuuu. Na kama wabunge yupoo mgombeaa mwenzaa bar kwa namnaa fulan alikarbiaa kuraa za kipindii hkoo angepewaa kushikaa hatamu mkuu. Hizi pesaa in nyingii zinapoteaa bilaa hayaa na uwogaa na wakatii tz INA matatzo mengii hataa elaa ya kuajirii vijanaa inakosekanaa znapelekwaa hukoo kugharamiaaa huu ujinga Wa wanaojiuzuluu
 
Kwelii wakuu inaniumaa snaa naposkiaa hayaa mabilion ya MARUDIO. Wakatii huo huoo hakuna majii kataa au jumbo husikaa sehem zotee. Mradii Wa kuletaa majii ni kama milioni kadhaaa hivii huu ni mtindoo ganii jmn.
 
Wakikubali ushauri wako huu unitag.

Nchi inaendeshwa kama gari... (In Mzee Mwinyi's voice)

Naenda zangu Wellington kula dinner.
 
Nimetafakari sana tukio la mwanafunzi wa elimu ya juu kupigwa risasi na kuuwawa kwa bahati mbaya wakati wa kuzuia maandamano ya wafuasi wa chadema jana kinondoni naona kuna haja sasa ya wabunge wetu tuliowachagua kwenye uchaguzi mkuu uliopita kupeleka mswada bungeni wa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi ,diwani au mbunge endapo ikitokea akijiuzulu ubunge au udiwani basi ateuliwe mwingine kutoka chama hicho hicho kilichokuwa kinatawala katika jimbo au kata husika aapishwe awe mbunge au diwani au ateuliwe aliyekuwa mshindi wa pili katika uchaguzi mkuu uliopita aapishwe awe mbunge au diwani hii itasaidia na itaepusha gharama za mabilioni ya fedha zinazotumika sasa nchini kwenye chaguzi hizi za marudio ambazo tangu 2016 tunaziona na fedha hizi zilitakiwa ziwasaidie watanzania kwenye masuala ya afya , elimu,barabara na masuala mengine ya kijamii ambayo ni ya muhimu sana kwa watamzania na pia kuepusha vurugu zinazoweza kutokea katika chaguzi za marudio na kupelekea kupoteza maisha ya watu wasio na hatia kama ilivyotokea jimbo la kinondoni.
 
Mkuu ni kweli lipo tatizo katika chaguzi ndogo na suala la kuhama vyama kwa ujumla. Nakubaliana na mawazo yako kwa sehemu kubwa. Lakini napigana nawe katika na 1 & 2. Ukisema vitekelezwe hyo itakuwa ni kuvunja haki ya kikatiba-ya kisiasa kama ulivyo nukuu kifungu hcho hapo juu. Lakini suala la pili tafsiri ya kisheria ya 'sababu za kijinga jinga' sijui itakuwa ni zipi.
 

Pascal, kwa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa jumamosi, bado unadhani tunahitaji tume ya uchaguzi ya muundo uliopo sasa hivi??????
 
Nimefuatilia kwa karibu sana mienendo ya siasa za hivi karibu I nchini .kujiuulu ubunge,kuhama chama kishakugombea tena nafasi ileile.
Ifike wakati tubaini ukweli na hasara inayoliigia Taifa letu masikini lenye changamoto nyingi huku tukitegemea 40% ya budget yetu kuendeshea maisha ya kawaida kutoka nje kwa wahisani.Ni wakati muwafaka sasa wa kubana matumizi kwa kubadili sheria zetu .
Yaani Mbunge,diwani au Raisi akijiuzulu,basis chama husika kiteuembunge mpya bila ya kuitisha uchaguzi mwingine.
hii itaondoa kuna.ahama kiholela,kujiuzulu kiholela na endapo Mbunge au diwani atajiuzulu bila ya sababu zenye kukubalika,ashitakiwe kwa kosa LA kuliyumbisha taifa.Na pengine kuleta mtikisiko wa kisiasa.
Tutizame katiba za wenzetu Ethiopia,Zimbabwe,SouthAfrika.wote walipojiuzulu hapakuitishwa uchaguzi,Bali waliteua viongozi wapya.
NIMEFIKISHA NAOMBA IFIKE BUNGENI KAMA HOJA NA OMBI BINAFSI .ILI UCHAGUZI UJAO UWE NA USALAMA ZAIDI .
 
kulikuwa hakuna haja ya kuitisha uchaguzi mdogo wakati wawakilishi Wa wananchi wapo hai.Ni mbwembwe na ufahari tu wa kuchezea fedha.Hizo fedha zingeenda kwenye huduma za kijamii ingependeza sana.Michezo ya kisiasa ni mibaya sana
 
Kama Mbunge au Raisi au Diwani wakijiuzulu chama husika kingepewa jukumu la kuteua mtu mwingine pasi na kufanya chaguzi mpya ,basi YASINGETOKEA HAYA YA POLISI KUMPIGA RISASI MWANAFUNZI ASIYE NA HATIA,wala fedha za umma mamilioni yasigepotea bure, kwa chaguzi za marudio
Badala yake pesa hizo zingelisaidia sector nyingine muhimu za Taifa letu masikini.
LAKINI WAPI ?AFRIKA YETU IMEGUBIKWA NA UJI GA MAMBOLEO ,WATU FULANI KUJIMILIKISHA NCHI NA KUIFANYA NI MALI YAO WAO TUU.
Na hujisifu kuwa wao ni wapenda haki na wenye Kubana matumizi ya hovyo kwa kufuta baadhi ya sherehe za kitaifa au kuondoa posho za vikao NK. UNAFIKI MTUPU .UONGO ULAGHAI .NDIO SIASA ZA KIAFRIKA? AIBU YETU HII KARNE HII.
 
Amani kwenu:
Mimi si mwanasiasa, lakini ni mkeleketwa wa maslahi mapana ya nchi, ninaugulia na machungu ya ubadhilifu wa pesa za walipakodi pale zinapotumika isivyo. Kuna hari inayoendelea sasa ya viongozi wa kisiasa- waliochaguliwa na wanainchi hususani wabunge na madiwani kujiuzulu nyadhifa zao kwa kisingizio cha "kumuunga mkono raisi' na kisha kuacha hasara kubwa na si kwa wanainchi tu, bali kwa taifa zima.
Hasara hiyo ni gharama za uchaguzi kutumika tena kwa ajili ya kumpata mwakilishi wa wanainchi mwingine, ambapo binafsi naona ni:
1. Matumizi mabaya ya rasilimali pesa.
2. Upotevu wa mda kwa ajili ya kufuatilia tena masuala ya kisiasa na wanasiasa.
3. Kurudi nyuma kimaendeleo, kwa sababu za matumizi mabovu ya rasilimali fedha na mda.
Sasa maoni yangu ni kwamba wale wote wanaojiuzulu nafasi zao za kuchaguliwa na wanainchi sheria iwepo kwamba " LAZIMA KWANZA WALIPE GHARAMA ZA UCHAGUZI ZILIZOTUMIKA HAPO AWALI WAKATI WA KUMCHAGUA YEYE", ili basi gharama hizo zitakazofidiwa na wanaojiuzuru zitumike kwa ajili ya uchaguzi wa marudio. Ktk hili tunakuwa tumeokoa pesa nyingi ambazo zitatumika (a) kununulia madawa hospitalini (b) madawati mashuleni (c) pembejeo kwa wakulima n.k.
Kuna taarifa nyingi ambazo zinashabiana na uzi wangu kama vile:

Maoni: Chaguzi za Marudio zifutwe

Shilingi Bilioni 3 kutumika katika Uchaguzi wa marudio

Haya ni maoni yangu tu.
 
Sijawahi kumuamini mtu huyo na sitamuamini , nikipata wasaa nitaku PM
Ukitaka kumbaini fuatilia maandishi yake humu jf siku chache kuelekea uchaguzi wowote ule ambao unashirikisha chama chake cha ccm , jaribu kufanya hivyo utambaini kirahisi sana !
Nasisitiza mimi sina chama kabisa bali najihesabu ni mmoja wa wazalendo wa kweli wa taifa hili.
Hivyo hili ni moja ya mabandiko yangu kabla ya uchaguzi ili kukipigania chama changu CCM.

Paskali
CChttps://www.jamiiforums.com/members/retired.376984/
Hapa nilikuwa nashauri sheria zibadilishwe ili chama changu CCM kiweze kuchaguliwa kitawale milele.
P.
 
Kumbuka Nissan na Noah + Wasiojulikana
 

Mapendekezo #1 and #2 huenda yanafanana na prescriptions za kutibu symptoms za ugonjwa na sio za kutibu ugonjwa wenyewe! Resignation na yote yanayofuata baada ya resignation ni matokeo ya ubovu wa sheria zinazohusika. Hata bila resignation, kiongozi anayetofautiana kimtazamo na chama chake anaweza kupoteza nafasi yake ya uongozi kwa kufukuzwa uanachama. Tumeshaona mifano mingi ya wahanga wa siasa kama hiyo, ndani ya upinzani na hata ndani ya chama tawala.

Pendekezo #3 lina changamoto kubwa, hasa kwa nchi zetu za Africa. Automatic succession, especially in the event of a leader’s death prior to the next election date, inaweza kusababisha 1st runner-ups wenye uchu wa madaraka kucheza michezo michafu, ikiwemo ya kwenda Bagamoyo kutafuta msaada wa nguvu za giza, ili wapate urithi wa viti vya uongozi bila kupingwa!

Mapendekezo #4 na #5 are potentially workable solutions, lakini yana changamoto kubwa! ...How do we get these done? Kubadilisha sheria inaweza kuwa kitu kigumu sana, kama sponsors wa hiyo sheria mbovu ndio tunaowategemea waibadilishe. We must first successfully install an amenable legislature! ...And this is where we can easily find ourselves entangled in a chicken-and-egg situation!
 
1.Kwanini serikali isiwape majimbo wabunge wa viti maalumu pale panapojitokeza either kifo, kujiudhuru, ugonjwa au sababu yoyote ile ili kuepusha gharama zisizoainishwa katika bajeti ya mwaka husika?

2.Hii itasaidia pia kupunguza matumizi ya fedha toka benki kuu kama katiba inavosema kuwa pale panapojitokeza uhitaji wa pesa isiyokuwa imeanishwa katika bajeti itolewe benki kuu

3.Kutojulikana kwa matumizi ya pesa tr 1.5 huenda pia chaguzi hizi za wabunge katika majimbo yaliokuwa wazi huenda kumechangia kwani naamini gharama zake hazikuwa katika bajeti husika ya mwaka 2016/2017

USHAURI

1.Tafadhali watunga sera mlione hili kwani ni tatizo na halina umuhimu wowote isipokuwa kuwapa wakaimu majimbo hawa wabunge wa viti maalumu katika majimbo husika

2.Pia wananchi wengi hawaoni umuhimu wa jambo hili kwasababu huwa hawajitokezi hata kupiga kura kwa chaguzi hizi ikilinganishwa na uchaguzi mkuu, mfano mzuri chaguzi za mwaka jana kulishuhudiwa vituo viko tupu hadi mawakala husika wa vyama vyasiasa kupelekea kusinzia vituoni paspo wapiga kura.

Nakaribisha maoni yenu wana JF
 
Kurudia chaguzi ni ulaji mpya uliobuniwa hivyo hawatakubali ushauri wako, kwanza kununua kuanzia madiwani ni ulaji na hata kupiga kura pia ni ulaji!
 
Leo Tunasikia Julius Kalanga aliyekuwa mb wa Monduli akihamia CCM. Na wengine wengi wamefanya hivyo huko nyuma wakidai kumuunga mkono JPM na kuchoshwa na mambo ya Chadema, cuf nk.
Ni haki yao kuhama lakini kinachowasumbua wananchi ni hizi chaguzi za marudio zinazoigharimu nchi mabilioni ya fedha bila sababu za msingi. It is justifiable kufanya uchaguzi wa marudio kama mbunge kafariki lakini hii ya kuhama vyama na kisha uchaguzi kurudiwa halafu anachaguliwa mtu yuleyule kwa sare za kijani kama ilivyotokea Kinondoni, mimi sielewi maana yake!
Wakubwa wanajifanya hawalioni hilo lakini hakika linawakera sana wananchi kwani ni usumbufu, kero, nonsensical na matumizi mabaya ya fedha katika nchi masikini kama Tanzania.
Katiba iangaliwe upya ili mtu akihama chama ahame na ubunge wake ili kuwatendea haki wananchi waliomchagua hapo mwanzo. Kinachoendelea sasa ni upuuzi mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…