Nilisikia kwenye Chombo cha Habari kuwa; Kwa sheria ya ndoa ya Tanzania, baba ndio anatoa hela za kila kitu kwenye Familia na hela ya Mke haihusu familia......
1. Baba ana wajibu wa kulea na kutunza familia ikiwemo kujenga nyumba, kulipa ada na kila kitu cha familia yake. Nikaona hii ni ile Sheria iliyopo kwenye Biblia ikieelekeza kuwa, kazi ya mama (mke) itakuwa ni kuzaa na kulea familia ikiwemo kuangalia maadili mema ya Watoto
Kimsingi hii sheria ilikuwa inafaa miaka ya 70 ambapo wanawake walikuwa wanakaa nyumbani kazi yao ni kuzaa na kuangalia familia LAKINI maisha yamebadilika kiasi kwamba wamama wanatoka Kwenda kufanya kazi na jukumu la msingi la mama ambalo ni kulea watoto anafanya dada wa kazi (house girl)
Sasa kama mama anatoka Kwenda kufanya kazi na kuacha jukumu lake la msingi kabisa la kulea Watoto afanye House girl; kwa nini sheria isitamke kuwa; kwa wale wanawake wenye kipato (waajiriwa/wafanyabiashara); kipato chao atashirikiana na baba kuendesha familia? Dunia imebadilika sana; wapo wanawake wengi tu wenye vipato vikubwa kuliko wanaume zao....iweje sheria yetu iwatenge kuchangia maendeleo ya familia?
HUO USAWA (50/50) WANAO DAI KILA SIKU, KWANINI HAUHUSISHI KUSHIRIKIANA MAJUKUMU KWA USAWA??
2. Kiwanja cha nyumba cha Baba/Mama
Kuna watu wana oana mmoja wao akiwa na kiwanja
Kulingana na mabadiliko ya Dunia, nafikiri ipo haja ya kuweka sheria vizuri kuwa; kama watu wataoana (ndoa) na kuridhiana kwa pamoja kujenga kwenye kiwanja cha mmojawapo; basi kile kiwanja walicho amua kujenga sio cha mmoja wao tena, bali ni sehemu ya nyumba (familia). Ina maana, huko baadae ikitokea kuna haja ya kugawana; Nyumba itahesabiwa ni Pamoja na kiwanja chake na hakuta kuwa na mmoja wao kudai kuwa alikuwa na kiwanja kabla ya kuoana....
Nasema hivyo kwani mambo yamebadilika; kuna mamluki wanaweza kutumia hiyo gape ya Sheria yetu kulazimisha wajenge kwenye kiwanja chake akijua huko mbeleni atadai chukua nyumba uniachie kiwanja changu, huku akilindwa na sheria....
Nawasilisha...