Sheria ya kulipa mikopo katika taasisi za kifedha kabla ya muda kumalizika

creophace

New Member
Aug 17, 2022
2
2
Mimi ni mtumishi wa umma. Nilichukua mkopo katika taasisi ya kifedha inayoitwa Maboto. Kila nikiwaomba wanipe balance ya mkopo wangu ili niwalipe deni lao hawataki. Hivyo nahitaji msaada wenu nifanyaje
 
Katika mkataba wenu kulikuwa na kipengele kinachoruhusu kulipa deni lote katikati ya muda wa mkataba?
 
Mimi ni mtumishi wa umma. Nilichukua mkopo katika taasisi ya kifedha inayoitwa maboto. Kila nikiwaomba wanipe balance ya mkopo wangu ili niwalipe deni lao hawataki. Hvyo nahtaji msaada wenu nifanyaje
Watumishi kwanini mnachukua mkopo Kwa vijikampuni uchwara kama hivyo???

Waandikie Barua kupitia Kwa DED na hakikisha UNAKAZA maana hivyo vikampuni vinatoa sana rushwa Kwa Utumishi Ili kuwakamata watumishi wajinga
 
Una nakala ya mkataba wa mkopo, inayoonyesha terms and conditions?
  • Kupewa outstanding balance ni haki yako kisheria, kuna njia nyingi sana za kuwa-force wakupe ila the real issue ni inategemea wakikupatia balance then what? Kama lengo ni kufuta mkopo hapa inabd sana kabla ya kufanya decision u-rely kwenye hzo terms alafu uone kama kuna relief yoyote kwako kwa kulipa mapema au pengine kulipa mapema kunakufanya kuwa worse-off.
  • Hizi taasisi ndogo zinakuwaga na terms mbaya mnoooo na mwanzoni hazikuwa regulated na BOT kiivyo.
 
Mimi ni mtumishi wa umma. Nilichukua mkopo katika taasisi ya kifedha inayoitwa Maboto. Kila nikiwaomba wanipe balance ya mkopo wangu ili niwalipe deni lao hawataki. Hivyo nahitaji msaada wenu nifanyaje
Tazama salary sleep yako,au wambiye wakuoneshe daftari la marejesho.Haiwezekani wasikupe balansi.Vinginevyo wewe mtata.Nimeongea na watu wa maboto fata utaratibu.
 
Mimi ni mtumishi wa umma. Nilichukua mkopo katika taasisi ya kifedha inayoitwa Maboto. Kila nikiwaomba wanipe balance ya mkopo wangu ili niwalipe deni lao hawataki. Hivyo nahitaji msaada wenu nifanyaje
Nimewahi kukutana na scenario ya jinsi hii kwenye kulipa mkopo wa Solar system ndogo kwa ajili ya makazi yangu yaliyopo nje kidogo ya network za TANESCO. Solar panel yenye taa 3, betri na eneo la kuchajia simu 1 - bei kununua cash ilikuwa kama laki 3 na nusu, mkopo miaka 4 unalipia jumla kama laki 9 hivi! Unalipia kama 19,000 kila mwezi kwa miaka 4!

Baada ya miaka miwili tangu nikope, hali yangu kifedha ikaimarika kiasi nikataka nimalizane nao hasa kwa kuzingatia kwamba nimeshalipa zaidi ya thamani halisi ya huo mtambo mdogo wa Solar.....

Kiukweli ilikuwa shughuli pevu kuwaelewesha! Wao wanataka ulipe ile ile laki 9 kwa kuwa umekatishia mkataba njiani eti. Tulisumbuana sana sana....
 
Bank huwa iko wazi sana unapotaka kumaliza mkopo kabla ya mkataba unaruhusiwa ila kuna utaratibu wake.
 
Back
Top Bottom