Sheria ya kulinda taarifa zetu na faragha ipo wapi?

Tengeneza Njia

Senior Member
Jul 29, 2022
121
204
Baada ya kupita katika zoezi hili la sensa ya makazi na watu 2022 na kuona namna taarifa nyingi nyingi sana zinakusanywa kupitia maswali yanayoulizwa na karani, kwa kweli nimepata ukakasi na kujiuliza maswali mengi juu ya uhakika wa ulinzi na usalama wa mambo niliyoyaweka wazi “kwa nia njema kabisa kama raia” mbele ya karani.

Nadhani wenzangu mtakuwa mashahidi pia katika hili, kuna maswali mengine hata Karani mwenyewe alikuwa inabidi ajitete na kuweka maneno kama “pole ni mambo ya kiserikali” au “nivumilie aisee” n.k.

Sasa, nikafanya utafiti wangu mdogo kwa wadau wanaofahamu sheria na wenzetu nchi Jirani kuona kama kuna miongozo yoyote ya kisheria ambayo ipo hapa Tanzania ambayo itatupa uhakika kuhusu kila kilichokusanywa na baadae kitaenda kuchakatwa huko na kuhifadhiwa, hizi taarifa ni salama?

Serikali yetu ina mifumo imara ya kidigitali ambayo itatunza taarifa zote hizi kiasi cha kwamba hakuna wataalamu ambao wanaweza kusumbua au kudukua mifumo na kusababisha taarifa hizi kusambazwa?

Ukiachana na zoezi hili tu pekee ambalo huchukua miaka mingi kujirudia, katika maisha yetu ya kila siku, tunafanya usajili kwenye taasisi na makampuni mengi ki-analojia na kidigitali na binafsi nimeshapata matukio kadhaa ambayo yananionyesha kweli dalili za kutokuwepo kwa usalama na ulinzi wa taarifa zangu.

Makampuni na taasisi zenyewe zinaonyesha kuchukulia poa suala zima la kutoa taarifa zetu bila hata mteja kuulizwa/ kuridhia.

Mfano; Nimeshawahi kupokea meseji kadhaa mara kwa mara kutoka kwa namba ngeni zikitaka nitume hela kupitia namba hiyo, hili zoezi la sensa pia, meseji za sensa(sikuwahi kuridhia nashangaa tu naona “Mimi Samia…” nafahamu, niliposajili laini yangu nikakubaliana na vigezo na masharti kulikuwa na maeneo yamegusia kuwa endapo mamlaka itahitaji taarifa zangu kampuni itatoa.

Si sawa, ukizingatia Katiba ya nchi Katika Ibara ya 16 inapinga kabisa vitendo hivi, na hakuna mtu yeyote, hata mamlaka ambayo ipo juu ya sheria mama (tena Katiba).

Ibara ya 16 (Haki ya Faragha na usalama wa mtu)

(1). Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.

(2). Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yaweza kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii.

Nadhani ni wakati sasa watanzania tuamke na kuisihi serikali kupitia wadau mbalimbali kuchochea kuwepo kwa sheria ambayo italinda faragha na usalama wetu.

Wengi wetu tumekuwa wahanga na tutakuwa wahanga huko mbeleni wa kuangamizwa na taarifa zetu ambazo tumezitoa wenyewe.


Mambo kadhaa ya kujiuliza?

Kwanza, mipaka gani iliyopo kwa mtu anayeshea taarifa za kawaida na nyeti za mtu mwingine kidigitali au nje ya mtandao.

Pili, kuna mahali popote kwa kuripoti na kuweza kuchukua hatua endapo mtu anapata tatizo za taarifa zake kutumika kinyume na mategemeo na haki.

Tuelewe pia kuwa dunia ilivyo sasa, taarifa ni PESA! Taarifa zetu zote iwe ni jina, anuani, namba za simu, picha zetu, mahali mtu alipo, namba za vitambulisho na pasipoti, Imani, dini, jinsia, kabila, mitazamo ya kisiasa, hali ya kiafya , utaifa, fingerprints, IP address n.k.

Vyote hivi vinawezakutumika katika katika namna ambayo inaleta faida kwenye makampuni makubwa na taasisi na kuwapa faida na Mwananchi ukabaki bila kupata faida yoyote kwa sababu tu hujui umuhimu wa taarifa zako na pia hakuna miongozo ya kisheria.

Kwa leo ni hayo tu!

Myafikishe haya mahali husika.

It’s about time.
 
Mkuu haya uliyosema ni sahihi na yana ukweli sana. Hatujui hatma ya taarifa zetu tulizotoa kwenye sensa.

Baadhi yetu kutambua umuhimu wa privacy ilibidi nidanganye hasa kwenye majina ya familia nzima na kutotoa nida namba kabisa nikijidai sina.
 
Back
Top Bottom