Sheria ya Dhamana

Chapakazi

JF-Expert Member
Apr 19, 2009
2,874
310
Habari Wakuu,

Naomba mwenye reference ya wapi naweza kupata sheria ya dhamana atoe hapa, au kama anayo aweke hapa, maana nimesoma habari ya Lema na kushtuka pale hakimu alipogoma kukubali dhamana bila kutoa sababu yoyote. Je hiyo ni sahihi?
Hii inaweza ikawa point nyingine kwenye katiba....Haki wa kushtakiwa haraka au kupata dhamana!


 
Habari Wakuu,

Naomba mwenye reference ya wapi naweza kupata sheria ya dhamana atoe hapa, au kama anayo aweke hapa, maana nimesoma habari ya Lema na kushtuka pale hakimu alipogoma kukubali dhamana bila kutoa sababu yoyote. Je hiyo ni sahihi?
Hii inaweza ikawa point nyingine kwenye katiba....Haki wa kushtakiwa haraka au kupata dhamana!

Hakimu alikata kutoa dhamana au Lema alikataa kupewa dhamana?
 
Hakimu alikata kutoa dhamana au Lema alikataa kupewa dhamana?

MAHAKAMA YAMNYIMA DHAMANA LEMA

06andamanachadema.jpg
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe(kulia), Katibu mkuu, Dk Willibroad Slaa, mbunge wa viti maalumu Joyce Mukya, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Wilaya ya Arumeru, Nassari Joshua, wakiandamana kutoka Mahakama Kuu ya Arusha jana kuelekea katika Uwanja wa NMC kufanya mkutano wa hadhara, baada ya kushindikana kumtoa kwa dhamana mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema aliyeko mahabusu . Picha na Filbert Rweyemamu
Mussa Juma , Arusha.
MBALI ya jitihada kubwa kufanywa na maofisa wa juu wa Jeshi la Polisi nchini sambamba na Mwenyekiti wa Chadema taifa , mwishoni mwa wiki iliyopita kumshawishi Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema, kulegeza msimamo wake ili atoke mahabusu jana na mwanasiasa huyo kuafiki, suala hilo liligonga mwamba baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kukataa kutoa hati maalumu ya kumtoa rumande.

Jumamosi iliyopita ujumbe mzito wa Jeshi la Polisi ukiwa na makamishna wawili, kutoka Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam ulimtembelea Lema gerezani na kuzungumza naye kuwasilisha maombi maalumu ya kumtaka akubali kutoka mahabusu ili kurejesha amani na utulivu mjini Arusha.

Maofisa waliomtembelea mbunge huyo ni Peter Kivuyo, Simoni Siro na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, Leonard Paul.

Mbali na maofisa hao Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wenzake alimtembelea Lema gerezani hapo na kumsihi akubali kutoka kwa dhamana ili apate nafasi ya kwenda bungeni kuueleza umma wa Watanzania na jamii ya kimataifa, adha anazokumbana nazo katika utekelezaji wa majukumu yake.

Hatua ya mahakama hiyo kukataa kutoa hati ya kumwachia Lema ilifanya sakata la mbunge huyo kugeuka kuwa kama sinema au mchezo wa kuigiza, huku Jiji la Arusha na viunga vyake likiingia kwenye taharuki baada ya mamia ya wafuasi wa Chadema walioamini kuwa ataachiwa leo, kuamua kupiga kambi Viwanja vya Unga Limited wakishinikiza mwanasiasa huyo aachiwe huku viongozi wao wakitoa hotuba kali.

Wakati wafuasi hao wakishinikiza Lema afikishwe mahakamani kisha achiwe huru kwa dhamana, mahabusu waliokuwa wakifikishwa katika Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Arusha, nao waligoma kushuka kwenye karandinga na kusababisha shughuli zote za mahakama hiyo kusimama.

Licha ya shinikizo la wafuasi hao kutaka kuachiwa Lema kuwa juu, mahakama hiyo jana mchana ilipasua machungu kwa wanachama na wapenzi hao baada ya kutangaza kwamba mbunge huyo atatoka kwa dhamana Novemba 14 mwaka huu saa 2:30 asubuhi.

Hali mahakamani
Kuanzia jana saa 2:30 asubuhi, mamia ya wafuasi hao wa Chadema walikuwa wamefurika viwanja vya Mahakama kuu, wakiimba nyimbo mbalimbali za kuhamasisha umoja na mshikamano hali iliyosababisha adha kubwa katika eneo hilo la mahakama lenye Mahakama ya Mkoa, Mahakama Kuu na Mahakama ya Biashara.

Kadri muda ulivyokuwa ukisogea watu walizidi kuongezeka. Saa 3:30, lilifika Karandika la mahabusu na washtakiwa wengine lakini wote waligoma kushuka wakitaka kwanza Mbunge Lema afikishwe mahakamani na kupewa dhamana.

Hali hiyo, ilizua kelele katika viwanja vya mahakama na baada ya majadiliano kati ya maofisa wa mahakama na polisi, iliamuliwa karandika lirejeshwe gerezani na kesi zote za jana zitapangiwa siku nyingine.

Hata hivyo, kadri muda ulivyozidi kujongea harakati za kumtoa Lema zilionekana kukwama, ndipo viongozi wa Chadema, walimwita Mwenyekiti wa chama hicho mahakamani ambaye alikwama kufanikisha kumtoa Lema.

Saa 10 jioni, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu, walifika viwanja vya mahakama kufuatilia sakata hilo lakini waligonga mwamba.

Wakati wafuasi na viongozi hao wa Chadema wakihaha kumtoa Lema, mahakimu na watendaji wa mahakama walifanya kikao ofisini kwa Jaji Aisha Nyerere hali ambayo iliongeza jazba kutoka kwa wafuasi na wapenzi wa Chadema waliokuwa eneo hilo.

"Sisi tunamtaka mbunge wetu wao wanafanya kikao," walisikika walalamika wafuasi hao na baadaye walianza kuimba:, "Tunamtaka mbunge wetu..., tunamtaka mbunge wetu!"

Hata hivyo, baadaye kikao hicho kilimalizika na kupatikana barua rasmi iliyokuwa imetolewa mapema mchana kuwa mahakama imekataa kutoa dhamana kwa Lema hadi Novemba 14, mwaka huu saa 2:30 asubuhi atakapofika mahakamani na wadhamini wake.


Awali, Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Arusha iligoma kutoa hati maalumu ya kumtoa Lema mahabusu anayeshikiliwa katika Gereza kuu la Kisongo lililopo nje kidogo ya Jiji la Arusha.

Barua ya kuomba hati hiyo iliyoandikwa na Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, kwenda mahakamani kuomba mteja wake aletwe kwa ajili ya taratibu za dhamana, ilikumbana na kigingi hicho cha mahakama baada ya Hakimu, Judith Kamara, anayesikiliza shauri hilo, kuagiza wenye nia ya kumdhamini mbunge huyo kufika siku kesi itakapotajwa.

"Wadhamini wamshtakiwa wafike mahakamani siku ya kutajwa kesi tarehe 14/11/2011 Saa 2:30, asubuhi kwa ajili ya utaratibu wa dhamana kwa mujibu wa masharti ya dhamana iliyowekwa na mahakama," imeeleza barua ya mahakama kujibu ombi la wakili wa Lema.

Katika barua hiyo ya Novemba7, mwaka huu yenye kumb. namba RM/GC/Vol. 111/50, mahakama haikutoa sababu za kukataa kutoa hati hiyo ambayo ingefanikisha Lema kuwekewa dhamana na kuungana na viongozi wa kitaifa wa chama hicho kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika viwanja vya NMC.

Wadhamini waliojitokeza kumdhamini mbunge huyo aliyeamua kwenda mahabusu kwa hiari yake kupinga uonevu, manyanyaso na ukandamizaji wa Jeshi la Polisi dhidi yake, wanachama na wapenzi wa Chadema walitambuliwa kwa majina ya Sarah Mohamed na Halfani Rashid ambao walilazimika kuondoka mahakamani hapo Saa 9:30 alasiri baada ya kusubiri kutekeleza jukumu hilo tangu saa 2:30 asubuhi.

Akizungumzia suala hilo ofisini kwake jana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa Arusha, Charles Magessa, alisema kisheria hakimu habanwi na kifungu chochote kutoa hati ya kumtoa mahabusu gereza bali kinachozingatiwa ni mazingira ya kesi na ulazima unaojitokeza.

"Kwa mfano, iwapo kuna ushahidi muhimu unatakiwa kutolewa na shahidi ana dharura ya safari nje ya nchi itakayomnyima kufika mbele ya mahakama siku iliyopangwa, hakimu anaweza kutoa hati ya kumtoa mtuhumiwa mahabusu ili ushahidi huo usikilizwe. Mengine yanayobaki ni busara ya mahakama ambayo haifungwi na jambo au nguvu yoyote kisheria," alisema Magessa.

Hakimu Magessa alisema kiutaratibu, maombi ya hati hiyo huwasilishwa kwake kama kiongozi kiutawala, naye huifikisha kwa hakimu anayehusika na kesi na ndivyo alivyofanya katika suala la maombi ya wakili wa Lema.

Gari la Mbowe chupuchupu
Katika tukio jingine, jana gari lililokuwa limebeba Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe lilinusurika kugongwa na gari la polisi lililokuwa likimzuia kiongozi huyo asikaribie eneo la majengo ya mahakama alipokwenda kuzungumza na uongozi wa muhimili huo wa dola, kujua kinachokwamisha hati hiyo ya kumtoa Lema gerezani .

Gari lilikimbizwa na kuzuiwa njia likiwa tayari limeingia ndani ya
uzio la mahakama baada ya Mkuu wa Idara ya Upelelezi Mkoa wa Arusha (RCO), Leonard Paul, kumwagiza dereva wa gari la polisi lenye namba za usajili PT 1178 kuzuia njia ili Mbowe asipite.

"Zuia hiyo gari...zuia hiyo gari, likimbize lisipite, fanya haraka
linapita," alisikika akitoa amri RCO Paul, amri iliyotekelezwa kwa
gari la polisi kulikimbiza gari la Mbowe ambalo tayari lilikuwa
imepita, hivyo kumlazimisha dereva wa gari hilo kusimama na kutishia kuligonga ubavuni upande wa dereva.

Hali tete iliyokuwepo mahakamani hapo jana ililazimisha uongozi wa polisi kuimarisha ulinzi ulioongozwa na RCO Paul, huku Kaimu Kamanda wa Mkoa, Akili Mpwapwa, akifanya doria ya kukagua hali ya usalama.

Uongozi wa polisi ulilazimika kuwaomba viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Slaa, Mbunge wa Singida Mashariki, Lissu na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro kufika mahakamani hapo kuwaomba wafuasi wa chama hicho kuondoka ili kuwawezesha majaji, mahakimu, mawakili na makarani waondoke.

Viongozi hao walifika na baada ya majadiliano na polisi na uongozi wa mahakama, ndipo Mbowe na Dk Slaa waliwaomba wananchi waliokuwa wamefurika eneo la mahakama kuondoka kuelekea uwanja wa NMC ambako kulikuwa na mkutano mkubwa wa hadhara.

Hatimaye, msafara wa wanachama hao ulioongozwa na Mbowe na Dk Slaa uliondoka mahakamani hapo manmo saa 9:30 alasiri hadi Uwanja wa NMC ambako licha ya mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha, watu waliendelea kusikiliza hotuba za viongozi hao kwa utulivu huku wakipaza sauti kuomba ruhusa ya kuchukua uamuzi mgumu wa kwenda kumtoa gerezani Lema kwa nguvu ya umma.

Dereva wa Lema adaiwa si raia
Dereva wa Lema, Rashid Shubeti ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema Kata ya Kati, jana alifikishwa mahakamani kujibu mashtaka matatu ya kuchochea vurugu, kuharibu mali na kufanya vurugu.

Shubeti ambaye alikamatwa tangu Ijumaa, pia awali analihojiwa na maofisa wa Uhamiaji Arusha kuhusu na uraia wake na jalada lake la uchunguzi linaendelea.

Akizungumza mara baada ya kupata dhamana jana, Shubeti ambaye tangu Jumatano wiki iliyopita alikuwa akilalamika kufuatwa na polisi nyumbani kwake kabla ya kukamatwa ,alisema maofisa wa polisi walimfuata nyumbani na kumpekua kisha kumfungulia kesi hizo.


Polisi wataka amani.
Idadi kubwa ya polisi ambao jana walikuwa wamefurika katika viwanja vya mahakama, waliomba vyombo vya habari visaidie kuweka wazi mgogoro wa Arusha ili amani ipatikane.

"Jamani tusaidieni leo tumekaa siku nzima hapa na jambo hili litaendelea sasa hali hii itaendelea hadi lini, Arusha ni mji wa kimataifa unataka amani andikeni kila kitu msimuogope mtu ili amani irejee Arusha," alisema polisi mmoja kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.

Source: Mwananchi.
 
haya...vifungu chenyewe hivi hapa. Nime-highlight vile nilivyoona vinahusika. Ijapokuwa kifungu hakisemi wazi kuwa ni lazima kwa mahakama kutoa maelezo, lakini ni wazi kuwa kwa ajili ya kifungu cha 149 kufanya kazi, ni wazi hiyo mahakama lazima itoe sababu za kugoma kutoa dhamana. Chadema wangepeleka watu wengine High Court kuendelea na hii process huku wakiendelea na kukesha kwao.



148.-

(1) When any person is arrested or detained without warrant by
an officer in charge of a police station, or appears or is brought before a
court, and is prepared at any time while in the custody of that officer or at
any stage of the proceedings before that court to give bail, the officer or
the court, as the case may be, may, subject to the following provisions of
this section, admit that person to bail; save that the officer or the court
may, instead of taking bail from that person, release him on his executing a
bond with or without sureties for his appearance as provided in this section.

(2) The amount of bail shall be fixed with due regard to the gravity and
other circumstances of the case, but shall not be excessive.

(3) The High Court may, subject to sub-section (4) and (5) of this section,
in any case direct that any person be admitted to bail or that the bail
required by a subordinate court or police officer be reduced.

(4) Notwithstanding any thin,, in this section contained no person shall,
for such period as the court shall consider necessary in the circumstances
of the, case concerned, be admitted to bail, either pending trial or pending
appeal, if the Director of Public Prosecutions certifies in writing that
it is likely that the safety or interests of the Republic would thereby be
prejudiced.

(5) A police officer in charge c f a police station, or a court before whom
an accused person is brought or appears, shall not admit that person to
bail if-
(a) that person is accused of reorder or treason;
(b) it appears that the accused person has previously been sentenced
to imprisonment for a term exceeding three years;
(c) it appears that the accused person has previously been granted
bail by a court and failed to comply with the conditions of the bail
or absconded;
(d) the accused person is charged with an offence alleged to have been
committed while he was released on bail by a court of law;
(c) the act or any of the acts constituting the offence with which a
person is charged consists of a serious assault on or threat of
violence to another person, or of having or possessing a firearm or
an explosive;
(f) it appears to the court that it is necessary that the accused person be
kept in custody for his own protection or safety.

(6) Where a court decides to admit an accused person to bail, it shall
impose the following conditions on the bail namely-
(a) surrender by the accused person to the police of his passport or any
other travel document; and
(b) restriction of the movement of the accused to the area of the town,
village or other area of his residence.
su(b7s)e Act icoonu r(t6 m), aiym, pino saed daintiyo no ntoe tohre mmoarned aotfo rthy ec ofonldliotiwoninsg p rceosncdriibtieodn isn,
namely-
(i) requiring the accused to report at specified intervals to a police
station or other authority within the area of his residence;
(ii) requiring the accused to abstain from visiting a particular locality
or premises, or association with certain specified persons;
(iii) any other condition which the court may deem proper and just to
impose in addition to the preceding conditions,
which appear to the court to be likely to result in the appearance of the
accused for the trial or resumption of the trial at the time and place
required or as may be necessary in the interests of justice or for the prevention
of crime.

149. Where in connection with any criminal proceedings a subordinate
court has power to admit any person to be it, but either refuses to do to
or does so or offers to do so on terms unacceptable to him, the High
Court may admit him or direct ins admission to bail or, where he has been
admitted to bail, may vary any conditions on which he was so admitted
or reduce the amount in which he or any surety is bound to discharge any
of the sureties.
 
Back
Top Bottom