Sheria ya Ardhi Na. 5 ya mwaka 1999 inasemaje juu ya fidia?

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
386
765
Tathmini ya maeneo ya Kata ya Nyatwali, Wilaya ya Bunda ilifanyika mwezi Januari, 2023 na wananchi kuahidiwa kuwa watalipwa siyo zaidi ya mwezi. Mpaka sasa malipo hayajafanyika licha ya ufuatiliaji wa muda mrefu.

Wananchi walizuiwa kulima kitu chochote katika maeneo hayo wakiahidiwa kuwa malipo yatatoka haraka na waweze kuhama. Kutokana na sheria ya Ardhi Na. 5 ya mwaka 1999 inasemaje kama muda wa miezi sita ukipita bila malipo.

Je, kuna utaratibu wa kupitia tena stahiki za wananchi ili mahesabu yapitiwe upya? Je, wananchi wana haki ya kwenda Mahakamani kudai haki zao?
 
Hawana hela ya kulipa Watu hao,serekali inanyanyasa watu bure,wanakijiji wa nyatwali wanateseka saana wemevuiwa shughuli zote za mawndeleo hawana chakula njaa kali pale nyatwali.
 
Back
Top Bottom