Sheria mpya ya mafao inatubana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria mpya ya mafao inatubana

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by flower, Jul 29, 2009.

 1. f

  flower New Member

  #1
  Jul 29, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani wanajamii forum nilikuwa nataka ufafanuzi zaidi kuhusu sheria mpya ya mafao yaani severance allowance.jamani tuijadilini naona inatubana walala hoi.
   
 2. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu fafanua vizuri ili tupate kwa undani unachomaanisha bado watu wako gizani toa sababu kwanini unasema inaumiza ndio mjadala utakuwa hot na wengi wataelimika kwa mada uliyoianzisha
   
 3. f

  flower New Member

  #3
  Jul 30, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwamba mtu anapofikia umri wa kustaafu au kama kazi ni ya mkataba ukiisha siunapewa mafao yako(yaani kiinua mgongo),sasa sheria ya mafao ya zamani ilikuwa unapewa 5% ya gross pay x number of months,ila ya sasa hivi unapewa mshahara wako wa wiki moja tu kwa mwaka mzima x number of years tena isizidi miaka kumi.
   
 4. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Mimi Nitaanza kulipwa mafao Yangu ya Kustaafu ya Kila mwezi Julai 2014! Naona Ni Mbali sana na hela Yenyewe Wakati Huo Itakuwa Mbuzi tu na Sitaki Usumbufu ninaouona Sasa Hivi kwa Wazee Wangu Unipate! Naombeni Anayeweza Kuunganisha mambo Nikapata Senti Zangu Hivi Sasa Anishitue! 'Maongezi' yapo kwa Atakayefanikisha!:);)
   
  Last edited: Sep 12, 2009
 5. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Wajameni, hakuna Yeyote Mwenye Connection na Miungu Wetu Wanaotuwekea Akiba Zetu????
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Sep 15, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Utalipwa ikifikia 2014? Mbona sijaelewa, kwa nini usianze kulipwa mara unapostaafu?
   
 7. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kulipwa mafao unahitaji connection? Nilidhani kwa vile ni haki yako bsai ni easy tu, kiasi cha kupeleka documents na kupata chako. Namna hiyo aliestaaf si atakufa mapema kwa pressure za kufuatilia hayo mafao? Kesho,next month,mwezi ujao,tommorow,kesho kutwa,next week etc.
   
 8. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...Mkuu Buchanan, Asante! Iko hivi. kwa mujibu wa jamaa wa ppf unapostaafu kama hujafikisha umri wa kustaafu rasmi kwa maana ya kwamba labda ni ridandansi, ugonjwa ama vinginevyo unapewa nusu ya mafao yako unayopaswa kulipwa kisha ile nusu nyingine utaanza kupewa kila mwezi pale utakapofikisha miaka 55/56 ambayo kwangu mimi ni miaka 6 ijayo!
  Ninapoangalia wazee wangu wanavyohangaikia kupata visenti vyao kichele kila mwezi na ninapoona kuwa hivyo visenti nitakavyopata kila mwezi wakati huo vitakuwa kikia cha Mbuzi mno, naona I'd rather have them Now than in 2014!
  For that, One Needs Connections....!
   
 9. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Mimi nadhani mtu anapaswa kilipwa mafao yake mapema iwezekanavyo ili yanfae katika maisha. Huku kucheleweshwa ni mbinu za hao wenye waliopewa dhamana ya kuakikisha kilamtu anapata haki stahili yake, kuwa na matumizi ya hizo pesa kinyeme na taratibu.Yawezekana wamezitumia hizo pesa wenyewe katika shughuli zao, au wamezichukua na kuwakopesha watu, au kweny utawala kama wa sasa, zinatumiwa na mafisadi either kwenye kampeni au kufidia/kuzibia mapengo ya fedha ambazo zilishatolewa na serikali kwa ajili ya jambo fulani, na pesa hizo zikatuwa vinginevyo. Kwa sababu kama hizo na njinginezo, ndo maana wanasumbua ili wapate muda wa kufuatilia walikokopesha au warudishe walizotumia (Viongozi husika) au kama zilitumiwa kwenye kweny kufanikisha ufisadi wao. kwa sababu hizo na nyingine nyingi ikiwa na pamoja na wao kutokuwa na kumbukumbu sahihi,kulindana kwa wahusika zinasababisha hayo ya Kesho,kesho kutwa, wiki ijayo,mwezi ujao, nk. Mbaya zaidi kama kipato chako ni kidogo, hautafuatilia kwani gharama za kufuatilia zinakuwa kubwa kuliko unachofuatilia, la sivyo tegemea kufilisika au shinikizo la damu, kufa mapema au vyote pamja.
   
Loading...