mwangalizi
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 842
- 512
Kwakuwa wana siasa, haswa naongelea wabunge wa CCM wameamua kutufanya wapangaji katika nchi yetu kwa kutupitishia sheria kandamizi nyingi tu katika awamu hii ya tano; mojawapo ikiwa hii ya kutokumiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao moja, bila kuzingatia kuwa zote utakuwa umesajili kwa alama za vidole na hivyo ukiamua kufanyia cyber crime yao utabambwa tu! Bila kujali kuwa hawakuwahi, hawakupendekeza na wala hawatawahi kutuwekea vocha katika laini hizo, napendekeza tufanye yafuatayo ili kurudisha heshima yetu kama wananchi.
1. Kwa kuwa mwezi huu ndiyo tuliopewa wa kuchagua kati ya laini zako kadhaa za mtandao mmoja uchague utabaki na ipi, hivyo ifikapo mwisho wa mwezi huu wananchi wote tususie kutumia laini zetu kwa siku mbili mfululizo, yaani mwisho wa mwezi huu na mwanzo wa mwezi wa nane. Hii itatusaidia kuwajulisha sisi si wapangaji bali ndiyo Tanzania yenyewe.
2. Wabunge wote mazandiki waliopitisha upuuzi huu tuwaadhibu kupitia sanduku la kura, wasirudi tena bungeni. Hili liwe fundisho kwa wengine tutakao wapa dhamana ya kutuwakilisha, wawaze sisi kwanza kabla ya njaa zao.
3. Tuwatenge wabunge wote mazandiki katika jamii zetu, tusishirikiane nao kwa chochote, tusihudhurie misiba wala sherehe zao na jamaa zao; wajipendekeza kwenye huzuni na raha zetu tuwatimue bila staha, maana imeandikwa mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye na huzuni ya babaye. Zamani katika Israel wenye ukoma walitengwa na jamii, wala hakuna aliyekuwa anajipa ukoma mwenyewe; sembuse hawa mabaradhuli wetu walioyataka wenyewe!
4. Aliyesaini sheria hii mbovu na za kufanana na hii, asipewe uongozi, hata ngazi ya shina, hata katika familia yake! Na ili familia kulinda heshima yao yawapasa kumtenga nao, wamwone kama kituko, wajute kuwa nasaba moja naye, wailaani siku ile ambayo alizaliwa. Kinyume na hivyo nao waingizwe kwenye kundi la wabunge mazandiki.
KAMA WENYE NCHI UMEFIKA WAKATI SASA WA KUSITISHA SIASA ZA MAJI TAKA NA NJAA, WE WANT REAL, SCIENTIFIC POLITICS!