Sheria inayoamrisha kutopiga picha katika kivuko cha Kigamboni iwekewe matangazo yanayoonekana kirahisi

ommytk

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
482
1,053
Wadau, kuna hii sheria ya kukatazwa kupiga picha katika kivuko. Wengi hatufahamu na imekuwa mtihani mkubwa ukikamatwa.

Inabidi kuwe na matangazo makubwa katika kila eneo itasaidia kuepusha yanayotokea baada kukamatwa.
 
Sheria hii ilitungwa fasta kuna kipindi watu walipiga picha kivuko kimejaza watu sana. Picha ilisambaa mno mitandaoni na marufuku ikapita hapo.
 
Iyo sheria inasemaje wengine tupo mikoani kama mjuavyo misimu ya kilimo kuja kushika siku ni mpaka msimu wa mauzo ndio tutajua dunia inaendaje kama hivi
 
Walishawahi kuwakamata wageni wangu wamisri waliokua wamefunga safari kutoka kwao kwaajili ya kuja Dar es salaa ,Zanzibar na Ngorongoro wakajikuta mikononi mwa migambo ya suma jkt wakiombwa hamsini elfu yaani kila kitu nilichoisifia hii nchi kilionekana ni umbea na mimi ndio nikaonekana msambazaji wa umbea huo
 
Unapiga picha kwa lengo gani hasa?
Unazipeleka wapi hizo picha?
Wewe ni raia halali wa Tanzania?
Wewe ni Chama gani?
Mjumbe ameomba tangazo la Katazo la kupiga picha liongezwe lisokeme kwa urahisi. Hayo maswali yanatoka wapi mkuu?

Nyie ndo wasimamizi wa mtihani wakipita karibu yenu wanashtuka na kuanza kuwaambia wanafunzi "wanafunzi tusikilizane, soma uelewe swali vzr"
 
Wadau, kuna hii sheria ya kukatazwa kupiga picha katika kivuko. Wengi hatufahamu na imekuwa mtihani mkubwa ukikamatwa.

Inabidi kuwe na matangazo makubwa katika kila eneo itasaidia kuepusha yanayotokea baada kukamatwa.
Wale Vijana wa SUMA JKT wakikuona unapiga picha hata kukufata wakuonye ila wanakusubiri ukishuka wakukalie kooonii
 
Wadau, kuna hii sheria ya kukatazwa kupiga picha katika kivuko. Wengi hatufahamu na imekuwa mtihani mkubwa ukikamatwa.

Inabidi kuwe na matangazo makubwa katika kila eneo itasaidia kuepusha yanayotokea baada kukamatwa.
Watu wahuni sana, hapo panavutia kupiga picha eti mijitu inazuia
 
Back
Top Bottom