Kinga ya corona kivuko cha Kigamboni bado changamoto

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
LICHA ya serikali kuwataka wananchi pamoja na taasisi kunawa mikono ikiwa ni njia mojawapo stahiki ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona, katika usafi ri wa vivuko kuelekea na kutoka Kigamboni- Dar es Salaam jitihada zilizochukuliwa dhidi ya ugonjwa huo sio za kuridhisha.

Gazeti hili limefanya ufuatiliaji wa kina kwa takribani saa moja kwa kuanzia upande wa kutoka Soko la Feri kuelekea Kigamboni ambapo limebaini utekelezwaji hafifu wa agizo la serikali hasa lile linalotaka uwekwaji wa maji ya kunawa mikono au vitakasa mikono kwa watu wanaoingia kupata huduma za usafiri.

Akizungumzia hali hiyo, Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema ameshaagiza kila sekta ya uchukuzi kuchukua hatua stahiki itakayosaidia kukabiliana na kusambaa kwa ugonjwa wa Corona hivyo hata katika vivuko hivyo changamoto hizo zitatatuliwa. Aliwataka viongozi wote wa vivuko nchini kuchukua tahadhari haraka ili kunusuru maisha ya watumiaji wake.

Katika usafiri huo ambao unakusanya fedha nyingi kwa siku, kuanzia katika geti la kuingia kuelekea kwenye sehemu ya kukatia tiketi hakuna maji ya kunawa wala vitakasa mikono. Gazeti hili liliingia moja kwa moja hadi katika sehemu ya kukatia tiketi kisha kulipa nauli kabla ya kupatiwa tiketi na kwenda moja kwa moja hadi kwenye mashine za kugusishia tiketi hizo ili mashine ya kupitia ifunguke kuelekea sehemu ya kungojea kivuko, sehemu zote hizo hazina vifaa vya kujikinga.

Pia hakuna matangazo ya tahadhari isipokuwa ya kukata tiketi, kutopiga picha, kutotupa takataka na kushuka katika magari pindi kivuko kikiwa kinaondoka. Upande wa pili wa kutoka Kigamboni kurudi soko la Feri nako hakukuwa na ndoo ya maji ya kunawa wala vitakasa mikono badala yake watumiaji wa usafiri huo kama kawaida walikuwa wamerundikana kwa wingi wakikata tiketi karibu na eneo la kungoja kivuko.

Chanzo: Habari leo
 
Back
Top Bottom