Sheria inasemaje ukitaka kumg'oa CAG?

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Naomba kujua sheria inasemaje ukitaka kumng'oa CAG?Hasa kwa aliyemteua kwa maana Rais,Je sheria inasemaje hapo kuhusu kumtoa katika madaraka yake?.
Maana naona kama kuna figisu! inanza na mimi naanza kuwaza kwa sauti!Ni kama Speaker anaweza kuwa yeye ni wakukoleza moto ila mwenye chungu ndiye kamtuma lakini yeye mwenye chungu haruhusiwi kukiepua!
Nawaza kwa sauti lakini!
 
Attachments

  • JPG.jpg
    JPG.jpg
    85 KB · Views: 48
CHEO CHA *Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali* NA MCHAKATO MZIMA WA *NAMNA YA KUMWONDOA MADARAKANI KWA MUJIBU WA KATIBA*

*Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano*

Sheria za 1979 Na.14 ib.11 Sheria ya 1984
Na.15 ib.43

*Article 143.-(1) CONSTITUTION OF UNITED REPUBLIC OF TANZANIA OF 1977 AS AMENDED FROM TIME TO TIME*

*Kutakuwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano.*

(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa najukumu juu ya mambo yafuatayo:

(a) kuhakikisha kwamba fedha zozote
zinazokusudiwa kutolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali matumizi yake yameidhinishwa
na kwamba zitatolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 136 ya Katiba hii, na iwapo atatosheka
kwamba masharti hayo yatatekelezwa ipasavyo,
basi ataidhinisha fedha hizo zitolewe;

(b) kuhakikisha kwamba fedha zote ambazo matumizi yake yameidhinishwa yatokane na fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali au fedha ambazo matumizi yake yameidhinishwa na sheria iliyotungwa na Bunge, na ambazo zimetumika,zimetumiwa kwa ajili ya shughuli zilizo husika na matumizi ya fedha hizo na kwamba matumizi hayo
yamefanywa kwa kufuata idhini iliyotolewa kuhusu matumizi hayo; na

(c) angalau mara moja kila mwaka kufanya ukaguzi na kutoa taarifa juu ya ukaguzi wa hesabu zaSerikali ya Jamhuri ya Muungano, hesabuzinazosimamiwa na watumishi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na hesabu za Mahakama zote za Jamhuri ya Muungano na hesabuzinazosimamiwa na Katibu wa Bunge.

(3) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu na kila mtumishi wa Serikali aliyeruhusiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu atakuwa na haki ya kuchunguza vitabu, kumbukumbu, hati nyinginezo zote zinazohusika na hesabu za aina yoyote iliyotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii.

(4) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atawasilisha kwa Rais kila taarifa atakayotoa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2) ya ibara hii. Baada ya kupokea taarifa hiyo Rais atawaagiza watu wanaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenye kikao cha kwanza cha Bunge kitakachofanyika baada ya Rais kupokea taarifa hiyo na itabidi iwasilishwe katika kikao hicho kabla ya kupita siku saba tangu siku ile kilipoanza kikao hicho.
Iwapo Rais hatachukua hatua za kuwasilisha taarifa hiyo kwa Spika wa Bunge (au Naibu wa Spika ikiwa kiti cha Spika ki wazi wakati huo au ikiwa kwa sababu yoyote Spika hawezi kutekeleza shughuli za kazi yake) ambaye atawasilisha taarifa hiyo kwenye Bunge.

(5) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa pia na
jukumu la kutekeleza kazi na shughuli nyingine, na atakuwa na
madaraka mengine ya namna mbalimbali, kama itakavyoelezwa na sheria kuhusu hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano au hesabu za vyombo vya Umma au hesabu za Mashirika.

(6) *Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wamasharti ya ibara ndogo ya (2), (3) na (4) ya ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hatalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu mwingine yeyote au idara yoyote ya Serikali, lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo hayataizuia Mahakama nayo kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ametekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii au sivyo.*

*Kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu*

Sheria ya 1984 Na.15 ib.43 Sheria ya 1995
Na.12 ib.19

*Article 144.-(1)*
Bila ya kuathiri masharti mengine yaliyomo katika ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Jamhuri ya
Muungano *atalazimikakuacha kazi yake atakapotimiza umri wa miaka sitini au umri mwingine wowote* utakaotajwa na Sheria
iliyotungwa na Bunge.

(2) *Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tukuondolewa katika madaraka ya kazi yake* kwa sababu ya
kushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi *au sababu nyingine yoyote)* au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa
Umma *na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wamasharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara hii.*

(3) Iwapo Rais anaona kwamba *suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu* kwa mujibu wa masharti
ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo
yatakuwa ifuatavyo:

(a) *Rais atateua Tume Maalum ambayo itakuwa naMwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopunguawawili.* Huyo Mwenyekiti na angalau nusu ya
*wajumbe wengine wa Tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji* au watu waliopata kuwa Majaji wa *Mahakama Kuu* au *Mahakama ya Rufani* katika nchi
yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola;

(b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoataarifa kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri lote na *itamshauri Rais kama huyo Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu aondolewe kazini* kwa mujibu wa
masharti ya ibara hii kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu
nyingine yoyote *au kwa sababu ya tabia mbaya.*

(4) Ikiwa *Tume* iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara
ndogo ya (3) *itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini* kwa sababu ya kushindwa
kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote
au kwa sababu ya tabia mbaya, *basi Rais atamwondoa kazini.*

(5) Ikiwa suala la *kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu* limepelekwa kwenye Tume kwa ajili ya
uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, *Rais aweza kumsimamisha kazi huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu,* na Rais aweza wakati wowote kufuta uamuzi huo wa
kumsimamisha kazi, na kwa hali yoyote uamuzi huo utabatilika
ikiwa Tume itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu asiondolewe kazini.

(6) Mtu ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu au
aliyepata kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hawezi
kuteuliwa kushika au kushikilia madaraka ya kazi nyingine
yoyote katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(7) Mashartiya ibara hii hayatatumika kwa mtu yoyotealiyeteuliwa kuwa Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
 
Asante sana sasa naanza kuelewa kwa nini anapelekwa Dodoma akajieleze inamaana alikuwa akisubiriwa au walimtegeshea mtego kwa mwandishi aliyemuuliza ili wakijua ataongea vile!Sasa naona kilichokuwa kikitafutwa kimepatikana sasa ni swala la muda tu!
 
Back
Top Bottom