Sheria inasemaje kwa mtu yeyote aliyevunja katiba?

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Ndugu wa JF nimatumaini yangu kuwa wote amjambo.
Twende katika Mada,
Nachotaka kufahamu katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,ni vifungu vipi umtia hatiani mtu aliyevunja/Kukiuka katiba ya JMT?.
Nimeona visa vingi hasa katika hii Awamu ya Tano nitatoa mfano kidogo.
● Ununuzi holela usiofuata taratibu.
● Miradi mkubwa isiyofuata sheria za GPSSA.
● Watumishi wa Serikali kujihusisha na Siasa RC's,DC's,
● Vyombo vya Dola Jeshi,Polisi,TISS, kujihusisha na Siasa waziwazi ikiwa katiba imekataza waziwazi.
● Tume ya Taifa ya Uchaguzi kushindwa kutekeleza majukumu yake kama chombo cha kusimamia haki ya Mpiga kura.
● Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kuwa na ukiukwaji wa sheria na kanuni hasa katika upinzani!tuliona jinni ilivyoendesha swala last CUF.
● Spika wa Bunge huyo ndiyo usiseme kwani kila siku yeye anasigina katiba.

Ajabu hata Mhimili wakutunga sheria umezichoka sheria ambazo ulizitengeneza wenyewe!

Haya ni baadhi ya makosa ya makusudi ya ukiukwaji wa washeria za nchi.
Kwa hayo machache naomba kufahamishwa ni hatua zipi uchukuliwa kwa watu wanao kiuka katiba ya nchi?
Je nani anawajibika kulinda katiba?
Kama katiba.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Hakuna wa kumuwajibisha mwenzake wakati mfumo wote tiyari upo Corrupted na tuliyemtegemea kusimamia KATIBA ndio anaongoza kwa kuivunja vipandevipande
 
Hakuna wa kumuwajibisha mwenzake wakati mfumo wote tiyari upo Corrupted na tuliyemtegemea kusimamia KATIBA ndio anaongoza kwa kuivunja vipandevipande
Kwa hiyo tunafanyeje kama nchi au wananchi?
 
Cockroach anajulikana!
87659087.jpg
 
Back
Top Bottom