Sheria inasemaje dereva anapofika kwenye zebra crossing?

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,157
Reaction score
166,119
JE NI WAKATI GANI NISIMAME KWENYE ZEBRA CROSSINGS AU JE NI AMRI KUSIMAMA KWENYE ZEBRA HATA KAMA HAKUNA MWENDA KWA MIGUU ANAYEVUKA? Sheria inasemaje?

Sheria ya usalama barabarani kifungu cha 65 kinahusu vivuko vya waenda kwa miguu, yaani pedestrian crossings.

Kifungu cha 65(1) kinamtaka mhandisi mkuu kusimika alama za vivuko vya waenda kwa miguu mahali panapofaa barabarani.

Kifungu cha 65(2) kinatamka kwamba mahali popote ambapo alama itakuwa imewekwa itachukuliwa kuwa imewekwa kihalali na itakuwa halali isipokuwa kama itakanushwa au kuthibitishwa vinginevyo.

Kifungu cha 65(6) kinamtaka kila anayetumia kivuko cha waenda kwa miguu kufanya hivyo kwa tahadhari kubwa na atumia kivuko hicho kuvuka barabara. Aidha kifungu cha 65(7) kinamtaka mtumiaji kivuko huyo kutokanyaga barabara ili avuke bila kuzingatia umbali na spidi ya magari yanayokuja

Kifungu cha 65(10) kinasema itakapotokea mtembea kwa miguu anatumia au anataka kutumia kivuko cha waenda kwa miguu, dereva wa gari atasimama kabla ya kivuko hicho ambacho hakiongozwi na taa za barabarani, ishara za barabarani au askari. [Hivi vivuko vinavyokuwa vimechorwa barabarani kwa mistari ya pundamilia ambapo mtu anavuka bila usimamizi wa askari au maelekezo ya taa]. Dereva ataendelea tu na safari ikiwa atajiridhisha kuwa hakuna mtembea kwa miguu anayetumia(anayevuka) au anakusudia kuvuka barabara.

HIVYO BASI, JIBU NI KWAMBA sio lazima dereva asimama kwenye kila zebra crossings hata kama hakuna anayevuka, dereva atapunguza mwendo na kuangalia iwapo kuna mtu anavuka au ananuia kuvuka, kama hakuna ataendelea na safari. Kwa hiyo, dereva atasimama kwenye eneo kabla ya zebra crossing pale wakati wote ambapo kuna mtu au watu wanavuka au wanakusudia kuvuka.

Ni matumaini yangu tumeelewana.
 
Tulipofikia sasa, ama ujue au usijue nini ni sahihi.....wakusanya kodi ndio wanaoamua; ukisema ndio, wanakwambia umekosea.....wanabofya vitu zao, wanakurudishia kipande chako.....haoooooo, washahesabu kamisheni yao!

Hizi tuziifadhi tu, pengine siku za usoni itawezekana.....
 
Leo nmebishana na askari hapo mlimani cty kwny round about nlikuwa naenda mwenge nmefika pale hamna mtu nikapita akanisamisha eti mbona sijasimama kivuoo cha waenda kwa miguu nikamwambia hamna mvukaji nikagoma kumpa leseni maana tungesumbuana sn,mwisho akaniambia ww nenda
 
Sasa Askari wetu Baadhi hawajui hii Sheria Unafika Eneo la Zebra unapunguza Speed unaangalia huku na huku hakuna mtu wa kuvuka unaamua kuvuka kumbe wao wamebana sehemu wanangalia ukivuka tu! Hao wanajitokeza kwanini? Hukusimama kwenye kivuko unawajibu nilipunguza mwendo nikaangalia pande zote hakuna wa kuvuka nikaendelea na safari wanakuambia na yule si mtu aliyesimama kumbe kaja baada ya wewe kupita anatumia hicho kigezo ili Umpe chochote kiukweli TAKUKURU wakiamua kuwakamata hawa jamaa kwa Rushwa watawazoa wote kuanzia DAR mpaka SIRARI Ni maoni yangu waungwana msijenge Chuki.
 
Bujibuji, jaribu kuwaambia askari wa barabarani kutoka Mbeya hivyo kama hujazusha mengine.

Na sasa hivi wana viburi hao! kama mke wa mahiga alikamatwa, sisi ni nani.

Kama risasi ilipigiwa juu kumpa onyo Malima, sisi ni nani?
 
Sasa Askari wetu Baadhi hawajui hii Sheria Unafika Eneo la Zebra unapunguza Speed unaangalia huku na huku hakuna mtu wa kuvuka unaamua kuvuka kumbe wao wamebana sehemu wanangalia ukivuka tu! Hao wanajitokeza kwanini? Hukusimama kwenye kivuko unawajibu nilipunguza mwendo nikaangalia pande zote hakuna wa kuvuka nikaendelea na safari wanakuambia na yule si mtu aliyesimama kumbe kaja baada ya wewe kupita anatumia hicho kigezo ili Umpe chochote kiukweli TAKUKURU wakiamua kuwakamata hawa jamaa kwa Rushwa watawazoa wote kuanzia DAR mpaka SIRARI Ni maoni yangu waungwana msijenge Chuki.
issue sio kujenga chuki Ila uonevu umepitiliza
 
JE NI WAKATI GANI NISIMAME KWENYE ZEBRA CROSSINGS AU JE NI AMRI KUSIMAMA KWENYE ZEBRA HATA KAMA HAKUNA MWENDA KWA MIGUU ANAYEVUKA? Sheria inasemaje?
Sheria ya usalama barabarani kifungu cha 65 kinahusu vivuko vya waenda kwa miguu, yaani pedestrian crossings.
Kifungu cha 65(1) kinamtaka mhandisi mkuu kusimika alama za vivuko vya waenda kwa miguu mahali panapofaa barabarani.
Kifungu cha 65(2) kinatamka kwamba mahali popote ambapo alama itakuwa imewekwa itachukuliwa kuwa imewekwa kihalali na itakuwa halali isipokuwa kama itakanushwa au kuthibitishwa vinginevyo.
Kifungu cha 65(6) kinamtaka kila anayetumia kivuko cha waenda kwa miguu kufanya hivyo kwa tahadhari kubwa na atumia kivuko hicho kuvuka barabara. Aidha kifungu cha 65(7) kinamtaka mtumiaji kivuko huyo kutokanyaga barabara ili avuke bila kuzingatia umbali na spidi ya magari yanayokuja
Kifungu cha 65(10) kinasema itakapotokea mtembea kwa miguu anatumia au anataka kutumia kivuko cha waenda kwa miguu, dereva wa gari atasimama kabla ya kivuko hicho ambacho hakiongozwi na taa za barabarani, ishara za barabarani au askari. [Hivi vivuko vinavyokuwa vimechorwa barabarani kwa mistari ya pundamilia ambapo mtu anavuka bila usimamizi wa askari au maelekezo ya taa]. Dereva ataendelea tu na safari ikiwa atajiridhisha kuwa hakuna mtembea kwa miguu anayetumia(anayevuka) au anakusudia kuvuka barabara.
HIVYO BASI, JIBU NI KWAMBA sio lazima dereva asimama kwenye kila zebra crossings hata kama hakuna anayevuka, dereva atapunguza mwendo na kuangalia iwapo kuna mtu anavuka au ananuia kuvuka, kama hakuna ataendelea na safari. Kwa hiyo, dereva atasimama kwenye eneo kabla ya zebra crossing pale wakati wote ambapo kuna mtu au watu wanavuka au wanakusudia kuvuka.
Ni matumaini yangu tumeelewana.
Huku dodoma na singida ni tofauti sana ,kwenye zebra awepo au asiwepo mtu anayevuka au anayetarajia kuvuka madeeva wanasimama na kuwasha hazard kana kwamba kuna mtu anavuka ,tahadhari kama we ni dereva mgeni kuwa mwangalifu ufikapo kwenye zebra haswa kukiwa na gari mbele yako
 
Traffic wamegeuza zebra crossing kuwa ni mradi wao binafsi
 
Back
Top Bottom