Sheria inasemaje dereva anapofika kwenye zebra crossing?

Sheria inasemaje dereva anapofika kwenye zebra crossing?

JE NI WAKATI GANI NISIMAME KWENYE ZEBRA CROSSINGS AU JE NI AMRI KUSIMAMA KWENYE ZEBRA HATA KAMA HAKUNA MWENDA KWA MIGUU ANAYEVUKA? Sheria inasemaje?
Sheria ya usalama barabarani kifungu cha 65 kinahusu vivuko vya waenda kwa miguu, yaani pedestrian crossings.
Kifungu cha 65(1) kinamtaka mhandisi mkuu kusimika alama za vivuko vya waenda kwa miguu mahali panapofaa barabarani.
Kifungu cha 65(2) kinatamka kwamba mahali popote ambapo alama itakuwa imewekwa itachukuliwa kuwa imewekwa kihalali na itakuwa halali isipokuwa kama itakanushwa au kuthibitishwa vinginevyo.
Kifungu cha 65(6) kinamtaka kila anayetumia kivuko cha waenda kwa miguu kufanya hivyo kwa tahadhari kubwa na atumia kivuko hicho kuvuka barabara. Aidha kifungu cha 65(7) kinamtaka mtumiaji kivuko huyo kutokanyaga barabara ili avuke bila kuzingatia umbali na spidi ya magari yanayokuja
Kifungu cha 65(10) kinasema itakapotokea mtembea kwa miguu anatumia au anataka kutumia kivuko cha waenda kwa miguu, dereva wa gari atasimama kabla ya kivuko hicho ambacho hakiongozwi na taa za barabarani, ishara za barabarani au askari. [Hivi vivuko vinavyokuwa vimechorwa barabarani kwa mistari ya pundamilia ambapo mtu anavuka bila usimamizi wa askari au maelekezo ya taa]. Dereva ataendelea tu na safari ikiwa atajiridhisha kuwa hakuna mtembea kwa miguu anayetumia(anayevuka) au anakusudia kuvuka barabara.
HIVYO BASI, JIBU NI KWAMBA sio lazima dereva asimama kwenye kila zebra crossings hata kama hakuna anayevuka, dereva atapunguza mwendo na kuangalia iwapo kuna mtu anavuka au ananuia kuvuka, kama hakuna ataendelea na safari. Kwa hiyo, dereva atasimama kwenye eneo kabla ya zebra crossing pale wakati wote ambapo kuna mtu au watu wanavuka au wanakusudia kuvuka.
Ni matumaini yangu tumeelewana.
Asante kwa kuleta relevant provision of the law. Sikujua Kama polisi wanatoza faini kinyume na sheria, na imekuwa ikitozwa sana(widely practiced )!

Mwezi Dec 2017 nilitembelea Dodoma, Iringa, Mbeya, nilichogundua inawezekana kulikuwa na amri ya kitaifa kukamata watu. Kwa Mbeya hali ilikuwa mbaya kwani ilifikia madereva kuwekwa ndani. Madereva ikabidi wawe wanasimama kwa muda na kuwasha hazard. Ilitokea jam ya ajabu, wakaamua kufuta maandishi "Simama" mbele ya zebra ili kunusuru hali iliyokuwepo na kuacha kukamata madereva kwa maeneo ya mjini.

Upande wangu naona jeshi la polisi linatumia vibaya msukumo wa Rais wa kufuata sheria. Sababu wanajua Rais hana mchezo kwenye suala la kutofuata sheria, basi wanalazimisha kufanya mambo hata yasiyotakiwa kwa kivuli cha sheria.

Inapotokea ukubaliani na maamuzi yao watakwambia twende kituoni alafu mahakamani. Ni uonevu, kukosa busara, na kupalilia mazingira ya rushwa. Wanajua kiuhalisia ni watu wachache watakao afford kusucrifice muda kufuatilia aidha kwa wakubwa wao ofisini au mahakamani kubishia uamuzi ulio nje ya maelekezo ya sheria.
 
ningefurahi sana kama watu wengi wa geita wangesoma uzi huu. ni kweli waendesha vyombo vya moto hata waendesha baiskeli geita mjini wanajitahidi sana kujali vivuko hivi. Shida kubwa inakuja kwa waenda kwa miguu, hawa wakiiingia ndani ya zebra looh, ndio wanazidisha kunyata, anaanza kusoma na txt kwenye simu yake. nijuavyo mimi anatakiwa avuke kwa haraka na ikiwezekana atroti kabisa. wajameni wanageita tujifunze haya ili watuamia barabara tuwe salama wote
 
Back
Top Bottom