Sheria inasema nini kuhusu hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria inasema nini kuhusu hili

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Freddy81, Oct 8, 2009.

 1. Freddy81

  Freddy81 Member

  #1
  Oct 8, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Habari ya leo ndugu wana jf,
  Mimi ndugu zangu napenda kusikia na kusoma maoni yenu kuhusu hili jambo ninalotaka kulizungumzia... Lahusu maeneo yanayopaswa kujengwa mabaa, misikiti na makanisa,
  Sheria inasemaje kuhusu hili? mana naona kama hakuna utaratibu mzuri unaosimamia mambo haya, siku hizi makanisa, mabaa na misikiti inajengwa katika makazi ya watu bila hata kujali jamii inayowazunguka.
  Kwa mfano hili la mabaa, tena utakuta wanafungua muziki mkuubwa hadi watu wanaona kero,lakini pia sio baa tu.. kwa mfano makanisa pia.. utakuta wamefunga maspika makuuubwa utadhani wanaendesha ibada ya mtaa mzima..hata misikiti pia nayo wameweka maspika yao na kila baada ya muda utasikia wakiswali..tena ile mbaya ni ile ya alfajiri..
  Sasa wadau embu niambieni hivi hawa wanaopima na kupanga miji huwa wanafikiria vitu kama hivi? au hawajui ni kero gani zinazotokea?
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,876
  Likes Received: 23,502
  Trophy Points: 280

  Mkuu ziraili hayuko mbali na wewe. Yaani unagroup pamoja bar na nyumba za ibada? Mbona hujachanganya magereji, filling stations nk? Piga magoti mwombe Mungu radhi. Makanisa na misikiti inatakiwa ijengwe sehemu yoyote ili watu wasicheze mbali na Mwenyezi Mungu.
   
 3. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kaka hii imani au ndo sheria inavyosema? Bila kua na mtu ka presda Kagame Bongo haiendi? Ki msingi bongo hakuna plani watu wanajifanyia ka watakavyo!!
   
 4. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,876
  Likes Received: 23,502
  Trophy Points: 280
  Imani binamu. Kwenye kumcha Bwana hamna kufuata sheria za wajingawajinga binadamu.
   
 5. Freddy81

  Freddy81 Member

  #5
  Oct 8, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sio kihivyo mjomba,
  Sasa kama mi nimelala halafu nikasikia muazana alfajiri na mimi si muisilamu hiyo si kero? au umepumzika ukasikia watu wanaimba kwa sauti sana kanisani na wewe si mkristo na unahitaji utulivu, si kero hiyo? Hiyo ni mifano tu..hayo magereji na filling station zote zinaingia kwenye mada hii... Je sheria inasema nini? achana na suala la imani
   
 6. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Misikiti na makanisa ninavyojua mimi inatakiwa ijengwe karibu na makzi ya watu ili watu waweze kuhudhuria kiurahisi. Mfano muislamu wa swala tano atawezaje kwenda umbali mrefu kutoka makazi au kazi yake kwa ajili ya ibada yake kila anapotakiwa kufanya hivyo? Ndiyo maana kila maeneo mapya yanavyogawiwa,huwa kunatengwa sehemu ya misikiti na makanisa.

  Ila hii isiwe sababu ya kuleta karaha kwa wakazi wengine. Makanisa yanatakiwa kuweka udhibit wa sauti za vipoza sauti vyao.

  Bar zinatakiwa kuwa mbali na makazi ya watu kwani mara nyingi zinafunguliwa usiku watu wakiwa wanapumzika majumbani mwao. Muziki bar tunategemea uwe mkubwa mara nyingi halafu zinachelewa kufungwa.
   
 7. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Sasa misikiti na makanisa yakijengwa mbali na makazi ya watu nani atakwenda huko kusali? Nafikiri tatizo si ukaribu wa nyumba za ibada na makazi ya watu bali matumizi ya vipaza sauti. Unakuta vipaza sauti vimefungwa mpaka nje na kuwahubiria hata wasiohusika. Hili ndilo tatizo. Vipaza sauti vilipaswa kufungwa ndani ya kanisa au msikiti ili kurahisha usikivu wa ujumbe kwa waliohudhuria ibada. Na si zaidi ya hapo.

  Watu wanapofunga vipaza sauti mpaka nje wanawakosea wale ambao hawahitaji ujumbe huo unaotolewa kanisani au msikitini. Kwani wenye haja na ujumbe huo ni hao waliofika kanisani au msikitini. Hao ndo wanaotakiwa kuhudumiwa na vipaza sauti vyenye kusikika ndani tu.
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Oct 8, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sheria ziko wazi isipokuwa utekelezaje wake ndugu yangu! Wabunge wetu huwa wanapata shida sana kutunga Sheria ambazo baadaye zinakuja kuwa hazina msimamizi! Sasa kama 75% ya Jiji la Dar es Salaam ina makazi holela (yasiyofuata Sheria za Mipango Miji), sasa jiulize kuna usimamizi wa Sheria hapo? Kuna maeneo yakishika moto au kuvamiwa na majambazi hakuna gari inayoweza kufika kutoa msaada. Hata uzoaji taka wa maeneo hayo ni mgumu mno! Hiyo ndiyo nchi yetu! Mimi simlaumu anayejenga msikiti, baa, gereji, n.k. kwenye makazi ya watu, wapo wa kulaumu!
   
 9. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,876
  Likes Received: 23,502
  Trophy Points: 280
  Eee Mungu, msamehe Mtumishi huyu kwakuwa hajui alisemalo. Anataka sheria za binadamu zitumike kuhamisha watumishi tusikuabudu katika maeneo uliyoyaumba wewe mwenyewe kwa uweza wako. Amesahau hata hizo sheria anazosema, zimetungwa na binadamu uliowaumba wewe mwenyewe kwa nkono wako. Halafu kwa kiburi ananiambia eti niachane na imani yangu juu yako ili nifuate sheria aliyotunga binadamu .Msamehe baba, saba mara sabini.

  Amina.
   
Loading...