pambe samanini
JF-Expert Member
- Oct 27, 2015
- 368
- 169
Kwa miaka kadha sasa walimu wamekuwa wakilalamika kuhusiana na chama Chao cha cwt kuwa hakiwatendei haki hasa za kuwatetea kupata stahiki zao kwa mwajli ikiwa pamoja na kupanda daraja, mazingira bora ya kufanyia kazi nk.
Hata hivyo makato yasiyo wanufaisha wanachama wao wakati na baada ya kustaafu kazi yao, pia utumiaji mbovu wa mali za chama bila kushirikishwa wanachama na pia chama kinanuka rushwa, ufisadi nk
Hata hivyo siku hizi pamekuwepo na vyama vingine vya kutetea haki zao km CHAKAMWATA, CHAWAKAMA nk ambavyo vimeleta ushawishi mkubwa wa walimu kujiunga navyo ili waweze kuondoka CWT.
Hata hivyo CWT wanasema hata kama walimu hao watajiondoa CWT bado wataendelea kukatwa ada ya uwakala na CWT kwa sababu wao ndiyo wenye mkataba kisheria na siyo vyama vingine vya walimu suala ambalo litapelekea walimu hao watakaojiondoa cwt kukatwa jumla ya 3% ikiwa CWT ada ya uwakala 2% na 1% ya vyama vingine.
Pamoja na migongano hiyo ya kimaslahi baina ya vyama hivi kuonaonekana ni suala la kisheria ambalo linahitaji marekebisho ya sheria ndo walimu hawa waweze kujitoa kwenye CWT na kujiunga na vyama vingine.
Je kwa sheria za sasa walimu hawa hawawezi kujitoa kabisa CWT na kujiunga na vyama wanavyovipenda?
Au serikali ina ubia gani wa kisheria na CWT kuwafanya wao ndo mawakala wa makato hayo yanayodaiwa na walimu kuwa haramu?
Pia, je mwajiri anaweza kumkatalia mtumishi wake mwalimu kujiunga na chama kingine kwa kuwataka CWT kuwacha wanachama hao bila ya kuwakata ada ya uwakala 2% nk
Kwa maswali haya naomba msaada huo