Sheria hii inalisaidia Taifa hili?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Date::4/21/2009
Serikali yatoa onyo kwa wabunge wanaoiba nyaraka za siri

Na Kizitto Noya, Dodoma

MBUNGE ambaye atakayebainika anatumia nyaraka za serikali kwa sababu yoyote ile atakabiliwa na hatua za kisheria bila ya kujali nafasi yake, Bunge la Jamhuri ya Muungano lilielezwa jana.


Lakini serikali imesema haijawachukulia hatua wabunge ambao wana nyaraka hizo na ambao wamejionyesha hadharani kuwa wanazo kwa kuwa inaelewa kuwa wana madhumuni gani.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti na Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Tabora Mjini, Siraj Kaboyonga aliyetaka kujua endapo Sheria ya Kinga na Haki za Bunge, inamruhusu mbunge kushika nyaraka za siri za serikali.


“Sheria hii haimkingi mbunge na wizi wa nyaraka za serikali hivyo kama ilivyo kwa watu wengine ni kosa la jinai mbunge kushika nyaraka hizo,” alisema Ghasia.


Alipotakiwa kueleza serikali imewachukulia hatua gani wabunge wanaokuwa na nyaraka hizo na ambao wamejionyesha hadharani, Ghasia alisema: “Tunawajua, lakini hatujawachukulii hatua za sheria kwa sababu tunaelewa wana madhumuni gani.”


Ghasia alisema kuwa wabunge hao wamekuwa wakiiba nyaraka hizo kwa lengo la kujijenga kisiasa na serikali inalishughulikia tatizo hilo kwa kuchunguza vyanzo vya upatikanaji wa nyaraka hizo.


“Sasa maadam wenyewe wapo leo na wanasikiliza mjadala huu, ninaomba wajirekebishe, kwani ukweli ni kwamba wanavunja sheria kama ilivyo kwa watu wengine,” alisema Ghasia.


Ghasia hakutaja majina ya wabunge ambao serikali inawajua kuwa wanamiliki au wanaiba nyaraka za siri za serikali, lakini kadri siku zinavyokwenda, vikao vya taasisi hiyo ya kutunga sheria vimekuwa moto kutokana na kashfa mbalimbali zinazoibuliwa dhidi ya viongozi wa serikali.


Wakati fulani, mbunge wa Karatu, Dk Willbrod Slaa alisimama bungeni na kuonyesha nyaraka alizonazo huku akisema kuwa sheria inayozuia kuwa na nyaraka hizo haihalalishi wizi, ubadhirifu wa mali za umma na mikataba mibovu na kudai kuwa yuko tayari kukamatwa.


Dk Slaa ambaye alikuwa akizungumza wakati Bunge lilipokaa kama kamati, alisema anaifahamu sheria hiyo lakini anazitafuta nyaraka za siri za serikali ili kutetea maslahi ya Watanzania.


Alisema kitendo cha kuwa na nyaraka hizo kinaonyesha ni kiasi gani mfumo wa serikali ulivyoanguka na akahoji ni nyaraka zipi anatakiwa azitumie bungeni na zipi asizitumie.


Miongoni mwa kashfa ambazo nyaraka zake nyingi zinaonekana kuvuja ni pamoja na wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ambayo taarifa za wizi wa zaidi ya Sh133 bilioni zilivuja hata kabla ya serikali kuanza kuchunguza.


Pia kashfa ya kampuni ya Meremeta kuwa ililipwa mamilioni ya fedha na Benki Kuu, huku kukiwa na kashfa nyingine ya utoaji wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kwa kampuni tata ya Richmond Development (LLC) na mradi wa umeme wa Kiwira.


Taarifa za siri za kashfa hizo zote zilivuja mapema na kutolewa ama bungeni au kwenye mikutano ya hadhara.


Katika swali lake la nyongeza, mbunge wa viti maalum, Rosemary Kiligini alitaka kujua endapo serikali bado inahitaji kuwachunguza wabunge hao wakati wanajulikana na akajibiwa:


“Pamoja na hali hiyo, bado tunahitaji utafiti wa namna wanavyozipata nyaraka hizo, kuna madai kwamba wengine wanazinunua kwa maafisa wa serikali lakina tunachowaomba wasirudie."


Alisema mbali na uchunguzi huo, serikali imeanza kuwabadilisha vitengo vya kazi maofisa wake inaowashuku kushirikiana na wabunge kutoa nyaraka hizo kabla ya kuwachukulia hatua zaidi za kisheria.


Mjadala kuhusu nyaraka za serikali, ulianzishwa na mbunge wa Matemwe Kheri Ameir, aliyetaka kujua katika swali lake la msingi kwa Wizara ya Menejimenti ya Utumishi ya Umma, endapo kuna watu waliokamatwa kati ya mwezi Januari na Desemba mwaka jana kwa tuhuma za kukutwa na nyaraka za siri za serikali.


Akijibu swali hilo, Ghasia alikiri kukithiri kwa vitendo vya wizi wa nyaraka za siri za serikali na kutumika isivyostahili, tatizo ambalo alisema kuwa haliwezi kupuuzwa na ambalo linastahili kuwekewa mkakati madhabuti kulimaliza.


“Nyaraka za serikali ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria mbalimbali... Sheria hizo ni pamoja na sheria ya Usalama wa Taifa namba 3 ya mwaka 1970, Sheria ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa namba 3 ya mwaka 2002, Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya mwaka 2002 na Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma,” alisema na kuongeza:


Sheria hizi zinaainisha mgawanyo wa majukumu baina ya vyombo mbalimbali vya dola na unatoa madaraka ya kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria, watuhumiwa wa wizi na nyaraka za serikali.”


Alitaja baadhi ya mambo ambayo tayari serikali imechukua kudhibiti tatizo hilo kuwa ni kuongeza kiwango cha elimu kwa kada ya watunza kumbukumbu, kutunga sheria mpya za utunzaji kumbukumbu na nyaraka za taifa na kuweka mfumo mpya wa utunzaji kumbukumbu unaodhibiti ufunguaji na utekeleaji wa majalada na nyaraka kiholela


Mjadala huo umetinga bungeni huku baadhi ya wabunge wakiwa tayari wamejitokeza bungeni kuhoji umuhimu wa nyaraka ya serikali kuwa za siri kama baadhi yake zinatumika kulihujumu taifa.


Tuma maoni kwa Mhariri
 
Aisee akina slaa walipambana,lakini pia kwa sasa naona wamefanikiwa kubana nyaraka za serikali,au ni kwamba wabunge wetu ndio sio wafuatliaji siku hizi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom