Sherehe za Uhuru na Shida Zetu

Nov 5, 2013
16
2
Wanajukwaa naomba kutoa hoja: Kwa kuwa nchi yetu ni masikini na inakabiliwa na upungufu mkubwa wa huduma za msingi za kijamii wakati umefika kuondoa sherehe kama ya Uhuru na nyinginezo na gharama zake ili fedha hizo ziende katika kuboresha hospitali zetu ziwe na vifaa na wataalumu na pia ili kulipia gharama za umeme ili nchi hii itoke kizani. Hivi wakati huu bado tunahitaji kusherehekea siku ya Uhuru kwa gharama kubwa kwa staili hii? Kwa nini isiwe kuenzi siku hiyo kuwe tu na hotuba ya Raisi ktk Tv na vipindi vya kutukumbusha siku yenyewe hasa na mijadala ktk Tv na Redio badala ya tunavyofanya sasa kwa kila mwaka kuwa na gwaride, kuchapisha T-shirt na Mabango, gharama za kuwapeleka na kuwarudisha viongozi uwanjani, kusimamisha kazi za ujenzi wa nchi nk. Pili, hata sisi tukisherehekea namna gani leo haitokuwa sawa na siku ile yenyewe ilivyokuwa ni ya furaha na shangwe iliyowatoa machozi wananchi. Tuamue kuwa hatutosherehekea kwa staili hii mpaka nchi hii watu wake wapate matunda stahiki ya uhuru. Wanasiasi mliomo humu mlitafakari jambo hili kwa kuwa ni unafiki mkubwa kwa nchi yetu kusherehekea uhuru kila mwaka kwa gharama kubwa wakati tupo gizani na bado huduma za afya ni duni. Nini faida ya sherehe hii kwa mwananchi wa kawaida iliyegizani na anapoumwa hana uhakika wa tiba iliyobora?
Wapo wanaoweza kuhoji rai hii kwa kuipinga lakini kumbuka kuwa sherehe katika nyumba inayovuja wakati wa mvua ni sherehe ya kufuja mali kama hatutoziba nyumba isivuje na wakazi wake wakae kwa raha na salama.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom