Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 30 ya CWT yaahirishwa

Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 30 ya CWT yaahirishwa

Anasimamia upande wa siasa sio wa utaalamu.Vyama vyote vya kitaalamu kiwe Cha madaktari au wafamasia nk viongozi wao lazima wawe madaktari,Wafamasia nk

Chama Cha walimu wametia aibu kuweka Mhasibu walilewa walipochagua au walilogwa?
Hujui chanzo cha Huyo anayeitwa mhasibu Leo kuwa KM CWT, ungeuliza ukaeleweshwa Mkuu. Maganga ni Mwalimu by profession. Alisomea uhasibu akiwa kazini na alipohitimu akagombea ukàtibu Mkuu CWT. Amekataa uteuzi wa Samia kaanza kupigwa zengwe.
 
Kama mwanafasihi, mwanafalsafa, mwanasaiklojia, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii nimesikiliza kwa makini sana hii hotuba ya rais wetu ndugu yangu na mama yangu Leah Ulaya nimegundua yafuayayo:

Mosi, ni dhahiri shahiri kuwa mtu mmoja hawezi kussababisha Serikali yetu pendwa kulipiza kisasi hivyo tuna kila sababu ya kumwondoa mtu huyo ili taasisi yetu ibaki salama.

Mtu huyo anajulikana hivyo kinachofata ni kumwondoa kwa utaratibu wa vikao vyetu kabla chama hakijaharibikiwa.

Pili, sherehe hiyo isingeisha salama kama huko mwanza hilo viongozi wetu walikuwa wameishalinusa pengine uwanja wa CCM kilumba usingebaki salama pia.

Hii ni kwa sababu walimu tunaongozwa na Mhasibu na sio mwalimu mwenzetu.

Tatu, chama ni kikubwa kuliko mtu hivyo hatuna sababu ya kumkumbatia CPA.

Nne, si kwamba Mh. Rais Samia Suluhu amekosa mtu wa kumwakilisha ni kwa sababu bado mama yetu anatupenda na ametupa muda mwingine wa kujitadakari kwa nn tuanaendelea kuongozwa na mtu asiye na nidhamu, pengine angekuwa ameishachukuwa hatua stahiki ila mama ni mama bado anatupenda.

Tano, muda wowote kuanzia sasa lolote laweza kutokea kwenye chama chetu maana tumekuwa kama sikia la kufa.

Mwisho niwashauri viongozi wenzangu tupunguze upambe tuseme ukweli ili kukiokoa chama na tuepuke tutengenezeana ajari, wanaoendelea kumdanganya CPA wanamtengenezea ajari bila yeye kujua anaamini wanampenda na wanamkubali.

Tujitathmini na tuchukue hatua.
Maryam,
Kama walimu ni makini inawalazimu wakuogope kama ukoma. Jina la Rais uliyemuita mama kwenye uongozi na migogoro ya CWT linatoka wapi? Huyo CPA kipindi mnamchagua hamkujua kuwa si mwalimu? Au kama ni mwalimu wewe unataka mwal. wa taaluma ipi ndiyo awe kiongozi wenu? Inavyoonyesha CWT imeshaingiliwa na chawa wa CCM. Tunakoelekea CWT haitasimamia tena maslahi ya walimu bali litakuwa tawi dogo la CCM na serikali yake.
 
Ummy ni DR mbona anaongoza Wizara ya Afya? hakuna kitu kama hicho
Ndugu yangu, inaonekana haya mambo yanakupiga chenga. Tofautisha uongozi wa kisiasa na uongozi wa vyama vya kitaaluma. Kuanzia kwa Rais wa nchi, makamo, spika, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya nakadharika, mtu wa taaluma yoyote anaweza kuongoza. Labda nikukumbushe mfano mmoja, kipindi mnapiga kelele kuhusu elimu ya Makonda au Bashite, serikali kupitia kwa waziri wa Utumishi wakati huo Angela Kairuki aliwajibu na aliwaambia, mashariti ya uongozi wa kisiasa yanaitaji mtu kujua "kusoma na kuandika" tu.

Kwa hiyo usihoji taaluma ya Anna Makinda kuongoza bunge wala Ummy Mwalimu kuongoza wizara ya afya kama waziri. Hao ni viongozi wa kisiasa. Ni tofauti na viongozi wa vyama vya kitaaluma.
 
Sasa nimeanza kumuelewa Mpwayungu Village kuhusu baadhi ya walimu ni wajinga wajinga na watu wa kujipendekeza ndio maana wanaburuzwa na kuonekana ni kundi dhaifu la kulikandamiza na kulitumia watakavyo!
 
Huyo uhasibu kaupatia akiwa tayari mwalimu wa shule ya msingi.
Kama ni hivyo hawa wanaopiga kelele watakuwa wanatumiwa au wana maslahi binafsi ambayo huyo Maganga kawabania. Kwani ukiwa mwal. hairusiwi kusoma na kupata taaluma nyingine? Kwa walimu wanaojitambua nawashauri wapaze sauti kumtetea Maganga dhidi ya makucha na majungu ya hawa chawa wa serikali.
 
CWT imeshapoteza malengo yake zamani sana.kile sio chama Cha walimu tena Bali chama Cha wajanja wacheche.kwa mfano Kuna benki ya mwl lakini wanaonufaika sio walimu,nilitegemea riba ya mkopo kwa mwl iwe chini kidogo kwakuwa mwl ni mwanahisa,
Pili,michango kutolewa bila usawa ni tatizo kubwa Sana.Inakuwaje Wanachama wenye haki sawa wachangie michango inayotifautiana(asilimia) ? Just imagine wakitoa gawio la Kila baada ya miezi mitatu Kila mwanachama anapata kiasi kilekile hata kama Huwa anachangia zaidi ya wengine,halafu hili gawio la tsh 2000 ni la nini hasa?hivi kwanini chama kisiondoe makato kwa kutumia asilimia halafu waache kutoa gawio maana halisadii chochote,yani unikate 15000 Kila mwezi halafu urudishe 2000 baada ya miezi mitatu[emoji23].Chama kinahitaji reforms kabisa
 
Mtu kukataa uteuzi ni kukosa nidhamu?

Huo UDC alioukataa si wangempa Mwashambwa anayepiga mihayo humu kila siku kumsifia huyo bibi wa kizimkazi.

Maana UDC siku hizi ulishageuka kama Tom,Dick and Harry.
 
Ndugu yangu, inaonekana haya mambo yanakupiga chenga. Tofautisha uongozi wa kisiasa na uongozi wa vyama vya kitaaluma. Kuanzia kwa ais wa nchi, makamo, spika, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya nakadharika, mtu wa taaluma yoyote anaweza kuongoza. Labda nikukumbushe mfano mmoja, kipindi mnapiga kelele kuhusu elimu ya Makonda au Bashite, serikali kupitia kwa waziri wa Utumishi wakati huo Angela Kairuki aliwajibu na aliwaambia, mashariti ya uongozi wa kisiasa yanaitaji mtu kujua "kusoma na kuandika" tu.

Kwa hiyo usihoji taaluma ya Anna Makinda kuongoza bunge wala Ummy Mwalimu kuongoza wizara ya afya kama waziri. Hao ni viongozi wa kisiasa. Ni tofauti na viongozi wa vyama vya kitaaluma.
Maganga ni mwalimu hata juzi aliandikiwa barua ya kurudi shuleni na haikuandikwa kama Mhasibu, sijui unataka mwalimu wa aina gani? jamaa amewabana mafisadi pale CWT mnashindwa kupiga pesa.
 
Back
Top Bottom